Serikali ya Afrika Kusini imeongeza ahadi ya kiwango cha mshahara kwa zaidi ya milioni kwa wafanyakazi wa umma waliogoma. Rais Jacob Zuma alitoa wito wa kuanza upya mazungumzo baada ya mgomo huo wa wiki mbili kusababisha shule na hospitali nyingi kusimamisha shughuli zake. Baada ya kuwa na mjadala mzito usiku kucha, wawakilishi wa serikali wameongeza malipo hayo kwa asilimia 7.5. Vyama vya wafanyakazi vimekuwa vikitaka ongezeko la asilimia 8.6 na wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumanne usiku kuamua wakubali ongezeko hilo au la. Zwelenzima Vavi, katibu mkuu wa shirikisho kuu la vyama vya wafanyakazi, Cosatu, aliiambia BBC kuwa walipambana vilivyo katika mazungumzo hayo ili kuishinikiza serikali iongeze mshahara kwa asilimia nane. Alisema ni uamuzi wa wanachama iwapo watakubaliana na ongezeko hilo. "Jana usiku tulipambana vilivyo na mpaka kufika asubuhi haikuwezekana.. Nahisi itabidi mgomo kama huu wa takriban wiki moja au mbili ufanyike ndio Serikali itakubali matakwa yao." "Swali ambalo wanachama wetu wanatakiwa kujibu kwa sasa ni: je ni muhimu-ukizingatia masuala yote hayo- au ni hatua ya ushindi katika kipindi tulichofikia sasa?" Mgomo huu umeathiri zaidi mahospitali, ambapo wauguzi wa kijeshi na watu waliojitolea wakiendelea kuwahudumia wagonjwa. Takriban wafanyakazi wa umma milioni moja waligoma. Raisi Zuma amekuwa akikosolewa na wafanyakazi waliogoma kuwa alikuwa katika ziara ya kibiashara huko China, il hali wauguzi, walimu na wafanyakazi wengine wa umma apo mitaani wakitaka ongezeko la mishahara. Ilimbidi Raisi Zuma arejeshe mahusiano mazuri na vyama hivyo, ambavyo ni ngao muhimu, kabla ya kuwepo mkutano wa sera wa chama tawala, the African National Congress, katika kipindi cha wiki tatu. credit: BBC Swahili Najiuliza... ...ikiwa somo limeeleweka kwa Wafanyakazi wa Umma wa Tanzania na kwa Wananchi wasio Wafanyakazi wa umma lakini wanaotumia huduma za umma.. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed