Serikali imesema kuwa bado haijakamilisha mkakati utakaowezesha Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupiga kura hivyo watakosa haki hiyo katika uchaguzi mkuu utakoafanyika Oktoba 31, mwaka huu. Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe alisema kuwa, kwa sasa bado wanalishughulikia suala hilo lakini hawawezi kupiga kura kwa sababu mchakato huo bado. “Hawawezi kupiga kura watanzania wanaoishi nje ya nchi, kwa sababu suala lao bado linafanyiwa kazi, hivyo basi hawawezi kupata nafasi ya kushiriki kwenye uchaguzi huu,”alisema Membe jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, Serikali bado inaendelea kuweka mazingira yatakayowezesha watu hao kupiga kura waweze kushiriki katika uchaguzi wa mwaka 2015. Alisema pindi mchakato huo utakapokamilika, Sserikali itauweka hadharani ili wadau wote wafahamu namna utakavyotekelezwa kwa kuweka mazingira huru yenye lengo la kupanua demokrasia. credit: Patricia Kimelemeta/Mwananchi CommentsKISUSI NYANDA 22/08/2010 2:54pm
Basi tunashukuru sana kwa taarifa hizo! Lakini tunaiomba Serikali ya nchi yetu kuwa makini na mambo ya muhimu yanayohusu haki msingi za raia wake (kwa namna ya pekee, uchaguzi wa Viongozi wa nchi). Naomba kuwasilisha!
Reply
samwel mtuwa 22/08/2010 4:23pm
Hizo siasa tuuuuu, kwani swala hili linachelewa nini mi naona ni usanii kama vitambulisho vya Taifa ni yale yale ... tume ya uchaguzi nayo imelala tuuu.... hili swala ni muhimu kuliko hata ununuzi wa VX 8 au GX 6...
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed