Picture
Wilbrod Slaa (katikati) akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum. Kushoto ni Said Mzee Said (mgombea mwenza).
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Dini inayosimamia masuala ya Rasilimali na Maadili, Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora, na viongozi wengine wa dini waliokutana na CHADEMA wamekiasa chama hicho kufanya kampeni kwa misingi ya haki, utulivu na kukubali na kuheshimu matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, 2010.

Viongozi hao wa dini walisema kuwa kukataa matokeo ni chanzo kikubwa cha uvunjifu wa amani na husababisha nchi kuingia kwenye matatizo makubwa kisiasa. 

Wakawaomba viongozi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kushambuliana majukwaani, badala yake wanadi sera na Ilani za vyama vyao.

Dk. Slaa akizungumzia maombi ya viongozi hao wa dini kuwa wakubali matokeo yatakayotangazwa na Tume, alisema “tuliwaambia vurugu baada ya uchaguzi zinatokana na matokeo, nasi tumesema wao wasitwambie tu tupokee matokeo, ila wahakikishe taratibu za haki zinafuatwa katika kupata matokeo”.

Tume hiyo imekuwa ikuzungumza na viongozi wakuu wa vyama vya siasa katika kipindi hiki cha kampeni za Uchaguzi Mkuu na tayari wameshakutana na Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na uongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Willibrod Slaa na John Mnyika.
Picture
Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati (kushoto) na viongozi wa juu wa CHADEMA (L-R) = Freeman Mbowe, Willibroad Slaa na John Mnyika. (credit photo: Bashir Nkromo)
 


Comments

Mtanzania
30/09/2010 07:11

Du! hii kazi sasa!!! CCM pia imeashauriwa kama hawa wanavyoshauriwa?? maana mi naona ni kama kuwapa nguvu chama tawala!!!!! kwani kwa kusema hivi basi matokeo yoyote yatakayotoka yakubaliwe yaani hata kama ikisemekana kwa mfano raisi amepita kwa asilimia mia tukubali jamani?? awe wa chama cha upinzani au CCM! kuna matokeo mengine ambayo hayawezi kuingia akilini hivo inakuwa siyo sahihi kukubali. Na inavyotokea kutokukubali tusidhani mtu anakaa tu anaamua nisikubali! sababu lazima zinakuwepo. Hili la kusema tukubali matokeo yoyote yatakayotangazwa mi sikubali na sitakubali. La msingi kama alivyomalizia dr. slaa ni kwamba taratibu na haki zifuatwe basi. Kutokuwepo na haki ndiko kunaleta matatizo mara zote!!! Wakati wa kura za maoni tumeona vihoja vingi kwa mfano ndani ya ccm tu! matokeo ya kura za maoni yanatoka kwa shida na yasiyo ya haki au mnabisha??? kwa mfano kule A town kama wenyewe wanavyoita, wilaya ya arusha sijui, ambako kuna mkongwe mmoja nasikia anaitwa elisa ameshikilia kiti mpaka......matokeo ya kura za maoni this time hayakutoka hadi wananchi walivyoamua kulala hapo halmashauri kuhakikisha hamna kura zinazoongezwa lakini nasikia hata hivyo ziliongezwa japo malengo hayakufikiwa.....hiyo ilikuwa ni CCM kwa CCM. Je, inapokuwa na upinzani itakuwaje?? kwa hiyo matokeo yatakayotangazwa yakubaliwe?? sitaki na sitaki kama haki na taratibu hazijafuatwa!!! tutafakari!!! hivi hakielimu mpo??? bado mnaendeleza jaramba au sirikali inazidi kuwatisha....najua kazi yenu imetulia na mnasemaga ukweli ndo maana wanawaletea so......hakuna kurudi nyuma tanzania ni yetu na siyo ya watu baadhi! ni yetu sote lazima tuseme. na siku wanavijiji watafikiwa vya kutosha wakapata elimu ya kutosha kama hakielimu inavyojiathidi basi itakuwa babu kubwa!! tusiwe na ushabiki na hii itatusaidia!!! tafakari kabla!!

Reply
davia
08/10/2010 05:23

Tusiwe watu wa kupelekwa watanzania wa sasa si wale wa mwaka 47,si kila jambo tukubaliane nalo hata kama linaonekana halikwenda katika njia sahihi,Hapana kikubwa uchaguzi ufanyike kwa haki bila kukandamiza au kuegemea pande moja,na isitumike hila wala yeyote,jinsi watanzania watakavyo piga kura na matokeo yawe hivyo.

Reply



Leave a Reply