Dawa za Serikali huibwa barani Afrika 02/09/2010
Matokeo ya utafiti yamethibitisha kuwa dawa za kutibu ugonjwa wa Malaria, zinazotolewa kwa nchi kadhaa barani Afrika, huibwa na kisha kuuzwa katika mahospitali na maduka binafsi ya madawa. kwenye ripoti iliyochapishwa na jarida moja la matibabu, watafiti kutoka Marekani na Uingereza walinunua dawa kutoka miji kumi na moja barani Afrika na kugundua kuwa dawa moja kati ya ishirini ilikuwa ni mali ya zahati na hospitali za Serikali. Wataalamu wengine wamethibitisha kuwa matokeo ya utafiti huo ni ya kweli. Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni moja hufa kila mwaka barani Afrika kwa ugonjwa wa malaria. credit: BBC Swahili YATOKANAYO Nami ingawaje sijafanya utafiti wa aina yoyote, ninaafiki matokeo ya utafiti huu kutokana na tetesi na vitendo vya kutilia mashaka ambavyo vimekuwa vikitendwa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu katika hospitali, zahanati, bohari za madawa na vitengo kadhaa katika Wizara husika. Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa Serikali inahujumiwa il hali dawa hizo zimetengwa kwa ajili ya kumsaidia mwananchi ambaye, mtumishi wa Afya na Serikali atamtegemea awe na afya njema ili aweze kuzalisha na kumwezesha yeye kupata ujira wake, kwa kufanya kazi ya kuelimisha na kuboresha afya za wananchi. Inasikitisha zaidi kuona kuwa akili zetu zinatutuma kujiibia sisi binafsi, kwani kuiba toka Serikalini ni sawa na kujikata vidole vya mikono, hatimaye viwiko vitakuwa kigutu na kuishia kuwa mzigo tegemezi. Tunapohimiza Serikali na viongozi kutimiza wajibu wao, nasi tukumbuke kuwa tunalo jukumu la kutenda kazi zetu kwa uaminifu. Pale tunapokosa ujira na malipo yanayoendana na nguvu kazi tunayotoa, basi tuidai panakostahili kwa taratibu zake badala ya kuhujumu Serikali kuendeleza rushwa katika Taifa. Tutajatolea hesabu matendo yetu. Natumai faili lako litakuwa safi siku litakaposomwa. Tubadilike! CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed