
Pia ninapenda utambue kuwa habari hii iliyopewa nafasi ya mbele katika gazeti la Tanzania Daima la Septemba 30, 2010 huu ndiyo ambayo imeonekana watu hata wale ambao ni rafiki zangu wakubwa na viongozi wangu ninao waheshimu zaidi kuninyoshea vidole na bila uchunguzi wakinituhumu kuwa mimi ni CHADEMA.
Japo si dhambi kuwa CHADEMA wala chama chochote cha siasa kwa Mtanzania, ni vema watambue kuwa mimi ni kada wa CCM na nimepata kugombea ubunge kupitia CCM na ni mjumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Iringa Vijijini.
Taaluma yangu haina chama, dini wala kabila.
(Endelea kusoma zaidi katika blogu yake - bofya hapa)
Yatokanayo...
wavuti.com inakemea na kulaani vikali tishio lolote kwa raia yeyote wa nchi hasa kwa wanataaluma, hususan, wanataaluma ya habari ikiwa habari wanazoziandika ni za ukweli. Tumeshuhudia waandishi wengi wa habari toka Afrika, Asia, Ulaya na Urusi, wakitiwa katika misukosuko na wengine wao wakipoteza uhai, kwa kuwa tu wameripoti na kuchapisha habari zisizopendwa na baadhi ya watu.
Tunakemea jambo hili na kuwakumbusha wale wote wenye mawazo ya kuficha ukweli kwa vitisho kuwa kamwe haitawezekana kuuzuia ukweli. Kutisha au kuua mtu si suluhisho. Watanyanyuka wengine. Waliotishwa na hata kuuawa, haikuwa mwisho wa kuripoti habari. Watakapoondoka hao, watainuliwa wengine na kuchipua. Ni roho iliyo hai. Kamwe haifi, bali hunyanyuka kwa mwingine. Hilo mlifahamu.
Pole sana Francis Godwin kwa usumbufu unaoupata.
Inshaallah, twashukuru kuwa hukumu ya haki hutoka kwa Mwenyezi Mungu.


RSS Feed