Freeman Mbowe atakiwa aiombe radhi Zanzibar 01/09/2010
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ametakiwa kuomba radhi kufuatia kauli yake kuwa Rais mstaafu wa Zanzibar, marehemu Idris Abdul Wakil, alishika nafasi hiyo akiwa na elimu ya darasa la saba. ![]() Idris Abdul Wakil - R.I.P Kauli hiyo ilitolewa na CCM Zanzibar jana kupitia Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Vuai Ali Vuai. Vuai alisema kauli ya Mbowe ni upotoshaji kwa Watanzania kwani Rais huyo mstaafu alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri aliyepata Shahada ya kwanza Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda. Alisema CCM imeshitushwa na kauli hiyo na kumtaka Mbowe awaombe radhi Watanzania na wanafamilia kwa vile kiongozi huyo alikuwa ni wa kitaifa. Hata hivyo, alisema CCM haifikirii kuchukua hatua zozote za kisheria, lakini kiungwana lazima wahusika wakubali wamefanya makosa kutangaza jambo kinyume na ukweli wake. Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za CHADEMA wiki iliyopita katika viwanja vya Jangwani, Mbowe alisema marehemu Abdulwakil alikuwa na elimu ya darasa la saba lakini aliweza kumudu vyema uongozi kwa vile ni hekima na busara. Aliyasema hayo baada ya wanachama wa CCM kudai kwamba mgombea mwenza wa urais wa Muungano kupitia Chadema ana elimu ya darasa la saba. Hatahivyo, Mbowe akizungumzia suala hilo alisema anatafakari hatua hiyo ya CCM na kama itathibitika marehemu Abdulwakil alikuwa na elimu ya chuo kikuu sio makosa kwa yeye kuomba radhi. “Hilo nalitafakari na kama kweli ikithibitika kiungwana sio makosa kuomba radhi”, alisema. credit: Nipashe/IPP Media Commentssieme 02/09/2010 11:27pm
CHADEMA NI WAPOTOSHAJI SIKO ZOTE.
Reply
baba T 03/09/2010 3:23am
Sieme, nadhani ishu hapa si udarasa la saba, ishu hapa ni Freeman kuomba radhi, na pia sidhani kama una haja ya kuwa na wasiwasi hkuhusu elimu ya mtu huyu kwani elimu ya ueledi na uongozi huwa ni vitu viwili tofauti sana. Kumbuka bado kuna watu wamemzunguka kutoa ushirikiano wao kikazi.....we wape tu kura yako.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed