Kwa nini Makamba alifukuzwa Ualimu? 02/09/2010
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA Dk Willibrod Slaa, amesema kuwa vigogo wa CCM hawana ubavu wa kumnyooshea kidole kuhusu maisha yake binafsi. Akihutubia wananchi katika mji wa Babati, mkoani Manyara, Dk. Slaa alisema iwapo wataendelea kuacha masuala ya kitaifa na kujihusisha na maisha yake binafsi, naye atawavaa na kuwavua nguo mmoja baada ya mwingine, kwani anawajua. ![]() Willibrod Slaa akihutubia Babati, Manyara Na kwa kuanzia, alimtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, awaeleze Watanzania kwa nini alifukuzwa ualimu wa shule ya msingi. Dk. Slaa alisema yeye hakufukuzwa Upadri, kama Makamba anavyodai; bali aliamua kuacha kwa kufuata sheria za kanisa, na akapewa kibali kutoka Vatican kinachomruhusu kuwa mlei na kuoa. Alisema iwapo Makamba atadanganya Wananchi kuhusu kilichosababisha afukuswe ualimu, Dk. Slaa atamuumbua. Wajuzi wa mambo wanajua kuwa Makamba alifukuzwa Ualimu (Mkuu) wa shule kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba mtoto wa shule. Naye Mkuu wa msafara wa Dk. Slaa, Suzan Kiwanga, alimtolea uvivu mke wa rais, Salma Kikwete, akisema anatumia pesa za umma kuzunguka nchi nzima anafanya kampeni huku akijua kuwa hatambuliki katika ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kauli ya Kiwanga iliongezewa uzito na Dk. Slaa aliyesema: "Nchi hii ina rais mmoja, ni Kikwete. Mke wa rais si rais. Anatembea kwa msafara wa magari 21 huku akilindwa na kupewa heshima zote na viongozi wa serikali; kama nani? Na raisi mwenyewe atatumia magari mangapi? Lakini hii yote ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi, na huu ni ufisadi," alisema huku akishangiliwa na umati uliokusanyika katika uwanja wa Kwaraha mjini Babati. Ilisemekana kwamba, asubuhi ya leo, kabla ya mkutano wa Dk. Slaa, Salma alitaka kuuteka uwanja huo na kuutumia kwa mikutano yake ya hadhara, lakini wananchi wa Babati wafuasi wa CHADEMAwalimtolea macho na kumfukuza uwanjani hapo. Hali hii ndiyo ilisababisha kauli ya Kiwanga, ambaye alisema: "Laiti ningemkuta hapa, sementi hii (sakafu) ingegeuka vumbi." Akasisitiza kwamba kama Salma angekuwa anataka kufanya siasa, angechukua fomu agombee urais kama mumewe ili apate fursa ya kuzurura na kufanya mikutano. Lakini si vema kutumia pesa za Ikulu au za asasi yake ya WAMA kufanya siasa. credit & copyright of this cross post goes to Ansbert Ngurumo "Utakapojua hujui ndipo utakapojua" blog Commentsmpekenyuzi 02/09/2010 7:49pm
hahahahaha, makambaaa mim niliambiwa kitu kimoja na mzee wangu usipende kumzungumzia mtu vibaya waka na wewe unatenda mabaya
Reply
@mpekenyuzi, thx for sharing. Umenipa funzo na kumbushio. Kurusha mawe kwenye nyumba za wenzio wakati nawe unaishi kwenye nyumba za kioo...
Reply
bobby 02/09/2010 10:17pm
looh sasa naona kazi ni moja tu... ukimwanga ugali, mi namwaga mboga kabisa!
Reply
Nicholas 03/09/2010 12:20am
Mweh! lololooooo!
Reply
j 03/09/2010 4:08am
s
Reply
Mohamed 03/09/2010 4:11am
Wadau naombeni nihoji hasa kuhusu suala la bi.salma. Je mgombea slaa akipita kuwa raisi, mkewe atakuwa akiendeshaje misafara yake?? jibu ni kuwa naye atakuwa na wapambe kama alivyo bi.salma. mkewe hawezi kuzunguka kwa gari moja hata siku moja. ni lazima apewe heshima ndio maana wake wa raisi hupewa jina la first lady.
Reply
PIUS MMANDA 03/09/2010 4:55am
Ni jambo la aibu kwa watu wanazielewa sheria kuzivunja kwa makusudi kama mke wa rais anavyo tumia fedha za serikali kwa kampeni.Taifa lenye DEMOKRASIA kama TANZANIA linatakiwa liwe mstari wa mbele kwa kujali kodi za wananchi au ndo wamechukulia literally ile story ya ANIMAL FARM kwamba wanyama wote ni sawa ila kuna walio zaidi ya wengine.Dr Slaa ndiye right HERO japo bado watanzania wamefumbwa macho na sera mbovu za CCM
Reply
rich 03/09/2010 4:56am
@mohamed. Kuna tofauti ya ulinzi na magari 21. Kuna tofauti kati ya kufanya kazi ya WAMA na kufanya kampeni ya wazi
Reply
Vuvuzela 03/09/2010 6:54am
Reply
Vuvuzela 03/09/2010 6:55am
Nilikuwa najaribu ili nije kiuweli
Reply
Kenny 03/09/2010 1:34pm
Makamba acha kufuatilia maisha ya watu, kumbe nawe document zako zote wajanja wanazo.Mwacheni Dr. Slaa aingie Ikulu Urais ni wa Watanzania wote
Reply
Mohamed 03/09/2010 8:55pm
@rich. kaka nakubaliana nawe kwamba kati ya mambo uliyoyataja tofauti inapatikana. ila hoja hasa ni kwamba sio rahisi mke wa raisi kuzunguka bila ulinzi, ni kitu kisichowezekana, fedheha yoyote ikitokea huoni kama dunia nzima itatushangaa???. yeye kama mke wa raisi naye yuko ktk harakati zake za maendeleo kama kuteuliwa kwake kuwa mwenyekiti wa WAMA. sio kwamba natetea CCM au ninakataa kwamba huo ni ubadhirifu, ila nachotaka kusema hata kama mke wa nani atapita as long as ni mke wa raisi basi heshima zote atapewa. ni kitu kilichowazi. sidhani kwamba Dr. Slaa atakapopita atamuwacha mkewe azunguke nchini bila ya ulinzi na msafara. Ahsante.
Reply
wam 03/09/2010 9:38pm
nadhani ni vema kabisa kufanya kampeni bila kuchafuana, maneno ya kuvuana nguo watu wazima mbele za watu sijambo jema na la busara, hakuna aliyesafi hatammoja. ukimchunguza bata huwezi kumla, kila mwanadamu anaouthaifu na uzuriwake elezeni ni kitugani mtatutendea mkiingia madarakani siyo malumbano na vitimbwi. Fanyeni nchi hii kuwa nchi ya baraka siyo ya balaa na laana mpendane, mheshimiane mvumiliane wacheni uhuni.
Reply
Friends of Life 03/09/2010 11:03pm
Salma=WAMA=UFISADI=WIZI WA MALI YA UMMA.
Reply
kash 03/09/2010 11:21pm
me naona Mh.Makamba huna jipya bali una mtazamo finyu kwa hapa mjini hakuna mtu anayeweza kushindwa kuona ukosefu wa dira ulionao hizo kampeni zako kazifanye huko vijijini kwa wenye mtazamo kama huo make huko ndo mnawadanganya wananchi kwa kuwapa vitenge na khanga T shirt na kumbuka siku moja hawa watu watafunuliwa na huo ndo utakuwa mwisho wenu
Reply
Waache watoone wajinga maana anatumia jasho letu kwa manufaa yao sijaona mke wa rais awe na msafara wa kampeni hizo pesa za kodi zetu au yeye alipewa ruzuku na serikali kwa ajili ya kampeni, kama angetaka kupiga kampeni aongozane na mumewe gharama zingepungua.Mimi sijaona ili kama mnakumbuka Baraka Ombama mkewe akufanya kampeni kama Salma kikwete na ukizingatia Marekani uchumi wao mkubwa pia hata kule Uingereza haijawai kutokea.
Reply
ARTHUR MTAFYA 05/09/2010 5:12am
Brother Mohamed muelewe Rich hajasema mke wa wa rais asipate ulinzi swala ni idadi na aina ya magari yanayofanya msafara na yote ni STK STG n.k. Mama Mkapa alituhumiwa sana lakini si show off za kijinga kama za huyu mama wa sasa. Hatukuwahi kusikia first lady wa awamu ya kwanza na hata ya pili japo ya pili ilikuwa na mikasa ya biashara chafu lakini si ya wazi ya kuwakoga wenye mali (wananchi)kama afanyavyo huyu dada
Reply
Ng'wanaMwamapalala 05/09/2010 5:31am
Dr Slaa ameanza kuingia kwenye mtego wa kampeni za CCM. Hicho ndicho CCM wanakitaka. wanataka badala ya kutumia muda kunadi ilani ya uchaguzi ya CHADEMA kwa wananchi awe anatumia muda mwingi kujibu shutuma za maisha yake binafsi na elimu ya mgombea mweza. CCM wamegundua CHADEMA haijajipanga vizuri katika swala zima la kampeni. maswala kama haya madogomadogo majibu yangepatikana kwa kampeni manager au Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na ukiangalia sana, anarumbana na Katibu mkuu wa CCM wakati mgombea wa CCM yuko kimya akielekeza nguvu katika kuuza ilani ya uchaguzi ya CCM.
Reply
Mangi 06/09/2010 12:06am
Dr. Slaa, acha kujibu maneno ya vijiweni. Wewe eneza sera za chama chako. Ona sasa mda wote mmeutumia kuongelea makamba na mke wa Jakaya ambao si wagombea uraisi. Mwigeni Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amekaa kimya akiendelea kumwaga sera za Chama chake.
Reply
Conna 22/09/2010 4:21am
Kuhusu first lady basi tuone kama anakula kwa urefu wa kamba yake. Muda wake wa mrs president ukiisha basi hata hayo matumizi mabaya ya kodi zetu yatasitishwa. Lakini kingine ni kwamba acha hao wazee walumbane tungejua lini habari zao kwamba mmoja alibaka na kugawa mimba na kwamba huyo mwingine alikuwa padri. Walumbane tupate faida.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed