Kocha wa timu ya mpira wa pete (netball) kwa wanawake Tanzania Bara, Simone McKinnis na kocha wa timu ya soka ya wanaume Zanzibar, Stewart Hall wamewasili nchini tayari kutumikia vibarua vyao.
Kocha wa timu ya netiboli ambaye ni raia wa Australia ataifundisha timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili, wakati kocha wa timu ya soka na raia wa Uingereza atatumikia mkataba wake wa kipindi cha miaka mitano.