TBC walikata mitambo yao, sasa leo narudia tena na hapa hukuna mitambo sijui watakata nini - Marando 02/09/2010
Akihutubia mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa Ubunge wa Chadema katika Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam Halima Mdee, Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando aliwaasa wakazi wa Kawe kutochagua wagombea wa CCM na NCCR Mageuzi kwa kuwa hawatakuwa na msaada wa kimaendeleo kwenye jimbo hilo.
Kuhusu Mgombea Ubunge kupitia NCCR Magezuzi James Mbatia, Marando alisema ndiye aliyesababisha yeye kukihama chama hicho. “Mimi ni mkazi wa jimbo hilo, maendeleo ya jimbo hili yananihusu, nilimwambia Mbatia kama atagombea Ubunge katika jimbo nitakihama chama hicho kwa kuwa yeye hana uwezo wa kuongoza na amekiua chama hicho,” alisema Marando. Alisema amekihama sababu anajua mgombea huyo kupitia NCCR Mageuzi hana uwezo wa kuongoza kutokana na kushindwa hata kufuatilia matatizo makubwa ya ardhi yaliyowakumba wakazi wa eneo hilo huku akiwa kama mwenyekiti wa chama hicho na mkazi wa jimbo hilo. Marando alirudia kauli hiyo aliyoitoa katika Viwanja vya Jangwani kwa kusema kuwa bado anaamini kuwa mafisadi wa kweli hawajafikishwa mahakamani. Katika mkutano huo, Marando alisisitiza kuwa watu waliofikishwa mahakamani si mafisadi, bali ni matawi ya ufisadi. Huku akishangiliwa na umati wa watu Marando alisema; “ Nilipozunguzia hili wakati wa kufungua kampeni TBC (Shirika la Utangazaji la Tanzania ) walikata mitambo yao, sasa leo narudia tena na hapa hukuna mitambo sijui watakata nini,”alisema Marandu na kucheka. “Niliwaambia kumfunga Liyumba, kumshitaki Maranda na wengine ambao kesi zao ziko mahakamani kwa sasa siyo suluhisho la ufisadi hapa nchini, nasema hivyo sababu wale waliofikishwa mahakamani ni matawi tu na mafisadi ni mti mkubwa ambao unatakiwa kung’olewa. Mafisadi halali ni wale waliotajwa na Dk.S laa waziwazi katika Viwanja vya Mwembe Yanga, alitaja majina yote na kuonyesha Watanzania wote kuwa kumbe wizi uko hata (BOT) mahali ambapo Watanznaia hata siku moja hamukuamini kama kuna wizi unafanyika,” alisema Marando. Akifafanua maana ya ufisadi alisema; “Mafisadi maana yake ni viongozi wanaotumia nafasi zao kuchota fedha za umma zilizotengewa kwa ajili ya ujenzi wa huduma za kijamii kama shule, zahanati, barabara n.k na kuzitumia wao binafsi na marafiki zao.” credit: Na Elvan Stambuli/GPL Commentsshafiq 02/09/2010 12:44pm
Uwepo wa mbatia kwenye kinyang'anyiro ni advantage kubwa sana kwa CCM..sipendi kawe iendelee kuwa chini ya CCm lakini nahisi wapinzani wanawapa zawadi chama tawala.
Reply
jk mvumi 02/09/2010 8:59pm
Mdee atapata ubunge, huyo mbatia akashughulike na chama chake
Reply
SEMENI 02/09/2010 11:38pm
CHADEMA WABABAISHAJI. WANACHANGIA KUUA UPINZANI. HOW COME UNASIMAMISHA MGOMBEA MWENZA DARASA LA SABA? THINK RAIS AKIFA AU KASAFIRI. THINK RAIS YUKO BUSY NA MAKAMU ANATAKIWA UN KUMUWAKILISHA PR.?????????? CRAZY!!!!
Reply
Asifiwe 03/09/2010 2:31am
Kwa kuwa na wapinzani wawili wenye nguvu tumewapa zawadi mafisadi
Reply
kuna mwaka watu wawili walibambwaga sehemu ya faragha.mzee wa kiraracha akataka kuwataja.tena walikuwa viongozi wa juu wa chama fulani.mungu atustiri na atusamehe.je zile tabia wameacha? au wanatuzuga?????hivi Wakichaguliwa hao,mungu hatatuadhibu jamani? au mmesahau.
Reply
Nicholas 03/09/2010 9:12am
@husna,tukumbushe basi hao watuu
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed