Brenda Msangi kwa ushirikiano na Dina Marios alifika katika kituo cha redio CloudsFM kwa lengo la kuwahamasisha wakina mama wenye fistula kujitokeza popote walipo ili kutbiwa.
Picture
Brenda Msangi, Mkurugenzi wa Programu ya jamii CCBRT
Fistula ni tatizo linalojitokeza kwa wakina mama wanaopatwa na tatizo wakati wa kujifungua ambapo kwa bahati mbaya njia ya kibofu cha mkono chaweza kupata tundu au njia ya haja ndogo kuchanika kiasi cha kuungana na njia ya haja kubwa na hivyo kusababisha mama kushindwa kuzuia haja ndogo, madhara ambayo husababisha kutokwa na haja ndogo mfululizo bila ya kuweza kuizuia.

Tatizo la fistula inatibika ikiwa mhusika atafika hospitali.

Kutokana na asili ya tatizo hili, akina mama wengi hupatwa na soni na kushindwa kutafuta matibabu, hivyo ninaungana na Brenda, Dina na wengine wote katika kuwahimiza ndugu, jamaa na rafiki kuwashauri na kuwasaidia akina mama wenye fistula kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu.

CCBRT inajitolea kugharimia usafiri, malazi, chakula na matibabu bure kabisa.

Ikiwa unalo tatizo, au unamfahamu yeyote mwenye tatizo hili, basi piga simu namba 0752 678263 POPOTE ULIPO na utaelekezwa jinsi ya kupata usafiri wa kufika hospitali ya CCBRT, Msasani, Dar es Salaam.

credit: Dina Marios blog

 


Comments




Leave a Reply