Ndege yaanguka mjini Sumbawanga 01/09/2010
Watu watatu akiwamo Rubani wa ndege na Mkuu wa wilaya wa zamani wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Hussein Mashimba wamenusurika kifo baada ya kuanguka mita chache wakati ikiwa imeruka katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mkoani Rukwa. Ajali hiyo imetokea leo katika eneo la SIDO majira ya saa 10:00 alasiri ikiwa ni umbali wa mita 15 kutoka ukingo wa uwanja wa ndege wa mjini Sumbawanga na kuhusisha ndege aina ya CESSINA 206 NO. 5H-TCC mali ya kampuni ya Flight Link ya mkoani Arusha. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa Bw. Isuto Mantage ndege hiyo ilikuwa ikitokea mjini Sumbawanga na kuelekea JIJINI Dar es salaam ambako ilikuwa ikimsafirisha Mkuu huyo wa wilaya wa zamamni wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya. Kamanda Mantage amesema kuwa ndege hiyo ilianguka ikiwa pia na Mganga mmoja wa hospitali ya mkoa wa Rukwa Dkt. Laswai na Rubani aliyefahamika kwa jina moaja la Navele. Kwa mujibu wa Mganga wa hospitali ya mkoa wa Rukwa Dkt. Gasper Nduasinde hali za majeruhi inaendelea vizuri na hadi sasa ni Mashimba pekee ambaye bado yuko hospitalini hapo kutokana na kuumia mguu wake wiki iliyopita alipokuwa mjini Sumbawanga na kulazimika kuletewa ndege hiyo kwaaajili ya kupelekwa Dar es salaam kwa matibabu zaidi. Dkt. Nduasinde amesema katika ajali hiyo ya ndege Mashimba aliumia kidogo katika sehemu ya mgongo wake lakini sio jeraha kubwa na hali yake inaendelea vizuri. Mashimba anadaiwa kuvunjika mguu mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuanguka bafuni katika nyumba mmoja ya kulala wageni mjini hapa alikuwa katika msafara wa kampeni wa CCM akimnadi Rais Kikwete. credit: Sammy Kisika, Sumbawanga via DulloNet CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed