"Nimesema kuna mengi nayafanya, lakini nikimaliza kipindi changu nataka watu wanikumbuke kwa mambo nane... waseme Mungu amrehemu, yule bwana acha tu, amefanya kitu."

- Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kupitia mpango wa Kilimo Kwanza,
- Matumizi bora ya mbolea,
- Dawa za kilimo,
- Kutoa wataalamu na maofisa wengi wa kilimo.
- Kusaidia upatikanaji wa masoko kwa mazao ya wakulima,
- Kusimamia uwepo wa bei bora za mazao,
- Kuimarisha barabara ili wakulima waweze kusafirisha mazao kutoka vijijini
- Kuachana na jembe la mkono kutumia matrekta makubwa na madogo
Akasema, mengi yanahitaji misaada ya wahisani, yamo ujenzi wa barabara na miundombinu ya kisasa ya maji. Ndipo akapata na fursa ya kugusia malalamiko ya safari zake nyingi za nje ya nchi.
Alisema: "Wapo wanaosema nasafiri sana, sasa ningekaa pale nyumbani kwangu nikamwangalia mke wangu Salma halafu nimwambie aisee ulivyopendeza, Watanzania wangekufa njaa na Wajapani wanaotaka kusaidia, leo hii wasingeijua Kaliua... "Sasa kuyapata yote haya, lazima nisafiri. Nilikuwa Marekani, nikakutana na wahisani mbalimbali; wenyewe wananiuliza wanataka wanisaidie wapi, mimi nasema hapa na hapa na pale... kuna watu wanapesa nyingi tu."
Soma habari nzima katika gazeti la Mwananchi


RSS Feed