Leo tena nimejifunza jambo toka kwa KK, kwamba zaidi ya bwawa la Mtera kuwa chanzo kikuu cha nishati ya umeme nchini Tanzania, bwawa hilo pia hutumika kama kivutio cha utalii kwa wageni.
Picture
Pichani ni baadhi ya watalii na wanavijiji wakiwa katika usafiri wakitalii bwawani. Mdau wa tembeatz blog, Tom wa Kimasafaris anasimulia kuwa safari huanzia kwenye mkokoteni unaosukumwa na punda. Hii ni muhimu kwani kina cha maji pembeni mwa bwawa la Mtera ni kifupi hivyo maboti hayawezi kufika pembezoni mwa bwawa na kuchukua abiria. Baada ya kufikishwa katika eneo lenye kina kirefu cha maji ambapo boti imetia nanga, ndipo watalii hushuka na kupanda kwenye boti tayari kwa ziara ya kutalii bwawani.

Ili kuona picha zaidi, mtembelee KK katika blogu yake ya tembeatz.blogspot.com
Picture
 


Comments

Aisee
30/09/2010 18:11

Bora wa Mtera wajichukulie fedha za utalii manake umeme unazaliwa kijijini kwao na wao hawaupati wanaishia kuona nguzo kwa mbali

Reply
Mnoko makini.
01/10/2010 00:32

Du!bw Aisee nilikuwa sijui kama wakazi wa mtera hawapati umeme.Hivi akili zetu zimechakachuliwa?Sasa wanashirikishwaje hata katika utunzaji wa mazingira ktk catchment area ya mtera if at all hata manufaa yenyewe hayaoni.

Reply



Leave a Reply