Picture
image : VOANews.com/swahili
Orodha hii imeandaliwa na mwandishi wa habari, bwana Francis Godwin na ameorodhesha katika toleo alilolichapisha kwenye blogu yake hapo tarehe 22 Oktoba 2010, baada ya hapo sijui zimeongezeka ngapi. Mimi binafsi nilianza kuzihifadhi kwa kila gazeti ninalosoma, mwishowe nilishindwa (lost track), nadhani ikiwa zipo zimesahaulika, tafadhali ziweke kwenye maoni, huenda zitatufaa ndani ya miaka 5 hii kuulizia "vipi tekelezo la ahadi zetu" kwa yeyote atakayepata ridhaa ya wananchi kuiongoza Tanzania 2010 - 2015.

Dk. Mohammed Shein (CCM)

  1. Kuboresha maisha ya wavuvi-Chakechake Pemba
  2. Kusomesha wafanyakazi-Mnazi mmoja
  3. Kipaumbele katika elimu -Unguja na Pemba
  4. Kipaumbele katika afya-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.
  5. Kuulinda Muungano- Wawi kisiwani Pemba
  6. Kuleta mabadiliko Zanzibar-Pemba na Unguja
  7. Kuboresha Bandari ya Zanzibar kwa kuijenga upya-Kibandamaiti
  8. Kuboresha Maendeleo Zanzibar- Jimbo la Wete, Pemba
  9. Ujenzi wa maktaba kubwa na nzuri Kisiwani Pemba- Mtambwe
  10. Kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu Zanzibar- Kijiji cha Kambini Mchangamdogo
  11. Kuimarisha miundombinu Kisiwa cha Pemba- Kijiji cha Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba
  12. Kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Pemba katika miradi mbalimbali-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.
  13. Ahadi eneo la Micheweni kuwa maeneo huru ya uchumi- Micheweni Kaskakzini Pemba
  14. Kumaliza matatizo ya maji mkoani -Mkoani
  15. Kujenga Bandari ya kisasa katika eneo la Mpiga Duri Unguja- Mkoani
  16. Kuiamrisha makazi bora kwa Wazanzibar- Mkoani

Dk. Slaa (CHADEMA)

  1. Kujenga nchi isiyo na ufisadi
  2. Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
  3. Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
  4. Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais5.Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
  5. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
  6. Kutoa huduma bora za afya bure
  7. kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
  8. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
  9. Kubana matuzi Ikula (Yuko tayari kula mihogo)
  10. Elimu bure kuanzia Chekechea hadi Kidato cha Sita
  11. Katiba mpya ndani ya miaka mitano

Profesa Lipumba na Maalim Seif (CUF)

  1. Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
  2. Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
  3. Kuunda Serikali shirikishi
  4. Kusimamia rasilimali
  5. Kuimarisha miundombinu
  6. Kusimamia na kuboresha afya
  7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
  8. Kurudisha chakula cha bure mahospitalini

Maalim Seif (CUF)

  1. Zanzibar kuwa kama Hong Kong – Unguja
  2. Kuendeleza mashamba ya Karume- Kibanda maiti
  3. Kubadilisha katiba na kuunda katiba mpya ya muungano na Zanzibar- Pemba
  4. Kubadilisha mfumo wa uteuzi makamishna wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)- Unguja
  5. Kuwaunganisha Wazanzibari ili kujenga umoja, udugu na ushirikiano-Pemba
  6. Kuwasilisha hoja ya kubadili katiba ya Zanzibar na ya Muungano-Viwanja vya Kibanda Maiti
  7. Kuondoa bajeti ya ZEC isiwe chini ya waziri kiongozi na badala yake kuwa inajitegemea yenyewe- Pemba
  8. Kuondoa ulazima wa mwenyekiti wa tume kuwa jaji na badala yake awe mtu anayejua sheria-Unguja
  9. Serikali kuundwa na vyama vyote vilivyopata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi- Unguja
  10. Kujenga jamii yenye maelewano na umoja -Pemba
  11. Kutokochagua kiongozi kwa urafiki bali kwa uwajibikaji na uadilifu -Unguja na Pemba
  12. Kudhibiti vyombo vya dola vinavyofanya kazi kwa matakwa ya watu binafsi -Kibanda aiti
  13. Kukomesha rushwa-Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba
  14. Kuhakikisha ununuzi wa zabuni unakuwa wazi na wananchi kuruhusiwa kuhoji kuhusu zabuni-Jimbo la Dole Pemba
  15. Kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi Sh150,000-Mkanyageni Pemba
  16. Kubadili vikosi vyote vya usalama na kulipwa mishahara kima cha chini kulipwa Sh 180,000-Chakechake Pemba
  17. Kubadilisha kikosi cha KMKM kuwa kikosi cha mwambao-Wawi
  18. Wazee kupanda daladala bure na wale wasiokuwa na watoto kulelewa bure-Majimbo ya Chakechake
  19. Kufuta michango yote ya shule za msingi na sekondari, kila mwanafunzi kuwa na kompyuta na badala ya kuishia darasa la saba sasa kuishia kidato cha sita-Hoteli ya Bwawani
  20. Kutoa kitambulisho cha kila Uzanzibari na kufuta cha Mzanzibari mkaazi- Uwanja wa Hospitali ya Mnazi Mmoja
  21. Kila Mzanzibari kupata pasi ya kusafiria- Hoteli ya bwawani Zanzibar
  22. Kuanzisha shirika la ndege Zanzibar -Viwanja vya Kibanda Maiti
  23. Kupandisha uchumi wa Zanzibar kutoka 6.8 hadi 15 kila mwaka kwa Zanzibar -Unguja
  24. Kutoa uhuru zaidi kwa vyombo vya habari pamoja na kusaidia uanzishwaji wa Baraza la Habari Zanzibar-Unguja na Pemba
  25. Kuweka hadharani nambari yake ya simu - Viwanja vya Kibanda Maiti
  26. Kubadili sheria ya uwekezwaji-Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
  27. Kila mwanafunzi kuwa na komputa yake-Viwanja vya Kibanda Maiti
  28. Akiwa rais hata waziri au mkewe atafungwa akiwa ametenda kosa-Viwanja vya Tibirizi Kisiwani Pemba
  29. Kujenga bandari ya Mkokoto na Pemba ili kuweka usafiri wa haraka wa boti ziendazo kasi-Tibirizi Kisiwani Pemba
  30. Ahadi kudhibiti kuvuja kwa mitihani- Unguja

Kikwete (CCM)

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hatia ya kuua albino- Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  21. Kulinda Muungano kwa nguvu zote-Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  28. Kununua "bajaji" 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za Sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu- Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa mpaka Singida-Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  44. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  45. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  46. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  47. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  48. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  49. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  50. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  51. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  52. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  53. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  54. Kutokomeza malaria 2015-Bunda, Mkoa wa Mara
  55. Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo, Iringa
  56. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  57. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  58. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  59. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  60. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbamba-bay Ruvuma
  61. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) –Ruvuma
  62. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  63. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  64. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  65. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  66. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  67. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha


 


Comments

Mwamvita M
24/10/2010 10:37

huyu kikwete, sijui nani anampigia kura kusema kweli. ukimpigia kura umelewa na wewe. duh ahadi mia moja?
(comment edited)

Reply
Kenny
24/10/2010 10:44

Ha haaaaaaaaaaaaa! Kuna wataalamu wamepiga mahesabu kuwa kila ahadi moja ya Kikwete inabidi itimizwe ndani ya siku 26 katika miaka mitano atakayokuwa maadarakani, Je itawezekana? ataacha kusafiri sana nje? Tusubiri.

Reply
Mpaka October 20 alikuwa na ahadi 70.
24/10/2010 12:31

Umefanya vizuri kuziorodhesha nyingi ya ahadi zake ambazo meneja wake wa Kampeni (A. Kinana) amekiri nyingi ni ahadi binafsi. Kwa mtu mwenye akili timamu lazima aelewe kuwa Mzee JK anatudanganya wazi wazi.

Reply
Duh
24/10/2010 12:33

Amewahi kutoa ahadi ya kupambana na wala rushwa? Tafadhali nikumbushe ni wapi na lini?

Reply
Wajinga ndio waliwao
24/10/2010 13:21

Duu hapo mzee mzima kachanganyikiwa, kama wanasema hela za elimu bure hawana sasa za kutimiza ahadi zote hizo atatoa wapi??? Mzee mzima acha usanii, tumeelimika sasa.....

Reply
Stan
24/10/2010 13:50

C'mon son! watanzania wameelimika sasa siasa za kijinga tunaomba mziache bana zinatukasirisha tu.Ahadi 67?? na sio sera! Mi-meli,mahospitali,Mi-airport,barabara,reli,bajaj,madeni,bandari....you name it! sio kamba kweli? manake Hospitali ya muhimbili hata kuondoa mazalia ya mbu ilibidi wajapan watoe msaada yani nilisikitika sana...

Reply
24/10/2010 14:11

Hapa shida ni ahadi zimezimzidi umri mgombea mwenyewe.

Reply
Kenny
24/10/2010 16:04

Katika ahadi za Dr. Slaa ipo moja kubwa nimeipenda; "kuweka Mwenge kwenye jumba la Makumbusho" Hii itakuwa poa maana wananchi wanachangishwa sana michango ya kupokea Mwenge kila mwaka

Reply
24/10/2010 17:48

Kenny,kama ni mwenge basi uwe mwenge wa kuwamulika mafisadi. Mwenge wa uhuru umeshindwa kumulika mafisadi zaidi ya kuendelea kutafuna jasho la walala hoi na walipa kodi.

Reply
Duh
24/10/2010 18:40

huo mwenge ni takataka unachochea maambukizi ya magonjwa!

Reply
mwantumu
25/10/2010 03:01

Angalia wasomi wote walivyoweka ahadi zao, yaani Dr. Slaa na Professa Lipumba, ziko chache, zilizobeba maana nzito za kiutaalamu na zinazopimika na kutelezeka. Hiyo ndiyo maana ya shule. Ukiangalia za CCM, utaona porojo, ukosefu wa utaalamu katika upangaji wa maendeleo na ubabaishaji. Si ajabu chini ya uongozi wao nchi imekuwa masikini wa kutupa maana wanaonyesha hawaitaji kutumia utaalamu katika uongozi na mipango ya maendeleo.

Reply
popomix
25/10/2010 03:17

Hizi ahadi za JK ni ngumu kutekelezeka kama amesema elimu bure haiwezekani basi ni wazi watanzania watambue kuwa hizi ahadi zote ni POROJO,MAFISADI ameshindwa kuwachukulia hatua za msingi kuonyesha msimamo uchungu kwa wananchi wake wanaonyonywa bila kupata huduma za msingi.

Tunahitaji Mabadiliko.

Reply
25/10/2010 04:33

Hizi ahadi, ni nyingi sana maana hawezi kuzitekeleza zote, ndani ya miaka mitano, hapo na nyingine hazija tajwa maana nilisikia na alisema kujenga bandari @bagamoyo sina uhakika sana maana si unajua porojo za siasa tena, hizo ahadi ukizipigia hesabu ni ndani ya zaidi ya miaka kama 20 na zaidi, sasa ahadi 67 duh hii noma, hizo ahadi zote kama atazitimiza itabidi wananchi wa hali ya chini itabidi tutumie nusu dora kwa sikumoja, watt wasiende shule, maana kwasasa matumizi ya mwananchi wa kawaida tu kwasiku ni noma je hizo ahadi zote hiyo pesa ya ghafla itatoka wapi? kama siuongo huo yeye aseme tu vile vinavyowezekana ni sawasawa mtu mwenye kilo 25 akabeba gunia mbili za mahindi ya kilo 100. never, hata mtt wa miaka mitano atakukatalia, inaonesha kwamba umeishiwa sera ila unalazimisha kupita,

Reply
leo
25/10/2010 07:25

Waliomshawishi JK agombee hawaipendi nchi hii. Na nchi hii inaweza kuendelea kubaki nyuma na kuzangumzia maendeleo ya nchi nyingine kwa sababu ya ujinga wetu. Alishaishindwa nchi zamani sana, lakini bado yupo. Hapa anataja vitu ambavyo hata 10% hawezi kuvitekeleza na anajua hilo. Lakini kwa sababu wapiga kura wengi huko vijijini uelewa wao ni mdogo, watampigia kura at the end of the day, nchi inaendelea kubaki masikini. IONEENI HURUMA NCHI YETU JAMANI

Reply
Marcely Madubi
28/10/2010 11:05

Watanzania inatubi tubadilike na kuzinduka kiakili na kifikra vinginevyo kuendelea kwa nchi yetu toka dunia ya tatu itabakia kuwa ndoto ya mchana. Ni vyema tukachagua viongozi kwa kuangalia wenye uwezo na uchungu na nchi hii. Mtazamo uwe ni Maslahi ya taifa na sio chama. HIVI wewe mwananhi wa kawaida chama kinakusaidia nini? Tuige mataifa yaliyoendelea mf. China, Marekani, Uingereza na mengineyo.

Reply



Leave a Reply