Nadhani ilipaswa isomeke, "Abiria toa hela" lakin pengine maneno sahihi ni "Abiria lipa nauli", kwa maana ukimwambia abiria atoe hela bila makubaliano maalumu, anaweza kushindwa kuelewa atoe pesa ngapi.

Picha hii imenaswa na kamera ya McKepha akiwa ndani ya daladala, Tanzania.
Picture
 


Comments

Frank
19/10/2010 01:59

Hili ni tatizo la kielimu kubwa lililopo Tanzania kwa kuwa wachoraji(sign writers) wengi tulionao wameishia darasa la saba.

Hapa ni kwamba ameshindwa kujua kuandika neno sahihi la 'abiria' na 'hela' na hata angeandika maneno hayo bado inakuwa ni command language na neno sahihi lingekuwa 'abiria lipa nauli' kama mwandishi wa habari hii alivyoshauri.
Hii inaonesha kuwa elimu ya darasa la saba bado haimsaidii mtanzania kukabiliana na maisha yake ya kila siku.

Inabidi sasa mfumo wa elimu ubadilike na elimu ya kidato cha nne iwe ya lazima kwa kila mwanafunzi.Inabidi tufanye uamuzi sahihi hapo oktoba 31 kwa kuchagua viongozi bora na si vyama vyao.

Reply
19/10/2010 13:11

Bwana Frank - inawezekana pia siyo tatizo la elimu bali ni athari ya lugha ya mama katika uzungumzaji wa Kiswahili Sanifu. Kwa mfano sisi Wasukuma tuna shida sana na kimadende [r]. Badala yake tunatumia kilainishi [l]. Wakurya ni kinyume chake (kura tumekura pa kurara je?).

Wahaya (ni watani zangu!) wana shida kubwa na irabu hasa zinapokuwa mwanzoni mwa maneno; na [h]. Kwa hivyo sitashangaa kama aliyeandika hili tangazo ana mojawapo ya haya matatizo - na usishanga kama akiwa ni "msomi" aliyebobea.

Kwa habari zaidi tembelea kiungo hiki:

http://matondo.blogspot.com/2010/09/hili-tangazo-ni-lazima-limeandikwa-na.html

Reply
Eddo
19/10/2010 14:08

@Masangu Matondo Nzuzullima naomba uwatafute wataalamu wa lugha wakutofautishie kati ya maneno ya lugha ya kuandika na jinsi unavyotamka.

Mimi huwa nawasikia watu wengi jinsi wanavyotamka,unaweza usielewe na ukimwambia akuandikie alichokuwa anatamka atandika vizuri tu.Tatizo hapo ni shule hakuna neno na kiswahili linaloitwa 'Ela',utatamka 'Ela' ila atakuandikia 'hela' hilo neno 'Ela' au 'kura' linawaathiri wasukuma,wahaya au wakurya wanapokuwa wakiyatamka na sio katika kuandika.Akiandika 'Ela' muulize elimu yake.FANYA UTAFITI.
Mbona hujajadili kama angeandika neno ‘Abiria toa hela’,huoni hiyo ni command language,hela ipi ada,nauli,kodi au?
Kama watanzania wote wangekwenda shule hadi kidato cha nne kusingekuwa na hayo makosa.Nimeona mabango mengi yenye maneno yaliyoandikwa kama yanavyosomwa.Kama mtoto amefundishwa maneno 'kula chakula' atatamka 'kura chakula' na ataandika 'kula chakula'.
Mtu anasikia Msemo wa 'Njaa haina umri' na anakwenda kuandika jinsi alivyosikia kwa kuwa aliyesema neno 'haina' herufi 'h' haisikiki hapo na yeye anakwenda andika 'njaa aina umri'.Muulize mtu huyo ameishia darasa la ngapi?.FANYA UTAFITI. TATIZO HAPO NI SHULE TU,kuna umuhimu elimu ya kidato cha nne iwe ya lazima.

Reply
19/10/2010 14:21

Bwana Eddo;

Sijaikataa kabisa hoja ya elimu ndogo. Nilichokuwa ninajaribu kusema ni kuangalia pia uwezekano mwingine.

Mimi nimesomea Isimu (Linguistics) na japo Isimu Jamii (Sociolinguistics) siyo uwanja wangu, ninachojua ni kwamba lugha ya kuzungumza na lugha ya kuandika zinaweza kuingiliana; na hili siyo jambo la kushangaza. Siyo kweli mara zote kwamba mtu anayetamka "ela" ukimwambia aandike ataandika "hela". Pengine nawe nikuombe UFANYE UTAFITI KIDOGO.

Pengine huioni athari hii katika maandishi rasmi lakini ukisoma maandishi ambayo hayajachujwa kama maoni katika blogu ya Michuzi, utaliona tatizo hili kwa ubayana sana.

Sijazungumzia "command language" kwa sababu sijui hasa lengo la mwenye tangazo hili ni nini. Pengine mwenyewe alitaka kuonekana "siriazi" kwamba hataki mchezo na ni lazima kutoa hela. Siyo rahisi kujua muktadha na lengo la mwandishi kwa kuangalia maneno matatu kama haya. Huwa sipendi kutoa hukumu za papo kwa papo bila kujua undani wa jambo. Na lugha ni msitu mnene ambao wakati mwingine unahitaji kurunzi makini ili kuelewa hasa lengo la mwandishi ni nini....Tuendelee kuelimishana

Reply
Muhd
19/10/2010 17:21

Tatizo ni kuwa hao waiokuwa hawajua matamshi mazuri ya Kiswahili wakiweza kuchoropoko kidogo na kufanya utafiti kwa kutumia lugha zao mama na wakapata PhD basi husema wao Kiswahili ni lugha yao mama. Nakumbuka kuna mama mmoja yuko US yeye utafiti wake kafanya kwenye Kichaga, na kapata PhD, naam. Lakini sasa anadai kuwa yeye Kiswahili ni lugha yake mama. Na anawaona waswahili kuwa hawajui lugha yao. Pia huthubutu kusema kuwa Kiswahili hakina mwenyewe.Lugha ya vitabuni ina tabu sana.

Reply
Mnoko makini
20/10/2010 06:47

Bw Masangu Matongo,
Nadhani tatizo hapo ni elimu ya mwandikaji zaidi kuliko athari za lugha mama(mother tongue).
Katika neno la kwanza "abilia" nakubaliana nawe kwamba baadhi ya makabila ya pwani na wasukuma wana tatizo hilo( r na l).Lakini tatizo la mwandikaji halikuishia hapo-akaandika "ela" badala ya "hela".Makosa yote mawili katika sentensi fupi kiasi hicho hayawezi ikawa ni effect ya mother tongue.Ishu hapo ni shule.
In social Linguistics-Unaweza ukajua elimu ya mwandishi,social status na sex(Jinsia) kwa kuangalia tu aina ya lugha mwandishia anayotumia,Misamiatiu,mwandiko, na hata mileu-(I mean eneo alilochagua mwandishi kufikisha ujumbe wake).Kwa mfano unaweza kuingia vyoo vya public ukakuta maandishi yameandikwa tena kwa kinyesi-'"Msolopa alikuwepo" hapa-Sasa ukiona hivyo si utajua tu elimu na tabia ya mwandishi?.Lakini kung'amua hilo ni rahisi zaidi kwenye spoken language kuliko kwa maandishi.

Reply



Leave a Reply