Matokeo ya utafiti huu pia yametamkwa katika taarifa ya habari ya TBC, ya saa mbili usiku leo, "tafiti huo ulifanywa katika mikoa 15 ya Tanzania bara, uliwahusisha watu 3047 na lengo la utafiti halikuwa kuonesha taswira halisi ya matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 31, bali kuwasaidia wagombea kujua maeneo zaidi ya kujikita katika kampeni kwa muda uliobaki kabla ya uchaguzi" - imesema sehemu ya Taarifa hiyo ya TBC.

Akizungumza na waadishi wa habari Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam idara ya Uchumi Dk. Vicent Leyaro amesema malengo ya TCIB ni kutoa msukumo kwa wananchi kushiriki katika harakati za kulinda na kendeleza misingi ya Demokrasia, Kutoa fursa kwa wananchi katika kutoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali katika maisha na kujenga uwezo wa wananchi kwa njia ya tafiti na elimu katika nyanja za Serikali, siasa, Mambo ya Kimataifa, ulinzi, elimu na maadili.
Aidha Dk. Vicent Leyaro amesema washiriki katika kura hii ya maoni ni 3047 wenye wasifu wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto chini ya darasa la saba, elimu ya Sekondari na elimu zaidi ya Sekondari ambapo katika utafiti huo asilimia kubwa ya vijana wamemuunga mkono mgombea urais wa CHADEMA Wlibrod Slaa na asilimia kubwa ya wazee wameonesha kumuunga mkono mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete.
Amesema Dk.Willbod Slaa ameongoza kwa asilimia kubwa katika mikoa ya Kilimanjaro 71%, Arusha 60.4%, Manyara79.8%, Iringa 58.2% na Dar es salaam 42%
Ambapo raisi wa sasa wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameongoza kwa asilimia kubwa katika mikoa ya Dodoma 59.3%, Morogoro 56%, Mbeya50%, Rukwa54.3% na Ruvuma 55%.
Akihitimisha wakati akijibu maswali kwa waandishi wa habari Dk. Vicent Leyaro amesema utafiti haukuangalia wala kupendelea sehemu ambazo mtu anapendwa sana kuliko sehemu nyingine na uchambuzi wa matokea kimkoa yanaonyesha kuwa wagombea wawili Jakaya Kikwete na Dk. Willbrod Slaa wanachuana vikali baadhi ya mikoa na mikoa mingine kufanya vibaya.
Hata hivyo utafiti huu wa kura ya maoni kuhusu wagombea Urais haukufanyika kwa upande wa Zanzibar japokuwa wananchi wa Zanzibar wanashiriki katika kupiga kura ya kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
PS: Deus Steven Msechu alimwakilisha mkurugenzi wa TCIB.


RSS Feed