UPDATE : Audio ya mdahalo kama nilivyoahidi awali, hii hapa. Bofya kifute cha play kusikiliza.

Videos za mdahalo wa kambi ya upinzani Bungeni 2010 uliofanyika siku ya Jumamosi, Novemba 26, 2010 kati ya Freeman Mbowe wa CHADEMA na Hamad Rashid wa CUF zinapatikana kwenye ukurasa wa videos.

Kwa wale wasioweza kutizama video za Youtube, vuteni subira, audio nitaiweka punde nitakapokamilisha kukorofisha mitambo na kuunga hivyo vipande vinne toka kwenye video. Ukishindwa kutizama video na audio, eh, usinilalamikie tena jama, nimejitahidi nilivyoweza, nakupa pole tu.

Mtu yeyote anayetaka kutizama ITV online (na TV nyinginezo za Tanzania na Afrika), tayari nilishaelekeza kuwa waweza kufanya hivyo kupitia TV4Africa.com kwa kufuata masharti yao (bofya hapa kurejea maelekezo hayo), na kwa kufanya hivyo, ikiwa una haraka, basi TV4Africa itakuondolea usumbufu wa kusubiri au kuomba mtu akuwekee video/audio, pengine mtu huyo ametingwa na shughuli zake chungu mzima au anakula hamsini zake, utalalamika weee...! Haya, tutegemeane jama, lakini tusiwe tegemezi ukaishia kutegemea tu fulani ataleta, fulani ataweka, hebu nawe leta ili tufaidi pamoja, raha ya TEKNOHAMA ni "nipe nikupe" atii, sasa wewe upewe tu? aaah, ukupe huo sasa, kukuruka mwanangu.
 


Comments

chali
29/11/2010 01:10

mbona inaniuliza user name and password ?

Reply



Leave a Reply