UPDATE 2: 
Orodha ya Baraza la Mawaziri na Manaibu wa Wizara 26 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2010 - 2015

  1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora - Mathias Chikawe
  2. Waziri wa Nchi, Oisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu - Steven Wassira
  3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma - Hawa Ghasia
  4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Muungano - Samia Suluhu Hassan
  5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Mazingira - Dk. Terezya Luoga-Hovisa
  6. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge - William Lukuvi
  7. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji - Mary Nagu
  8. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - George Mkuchika
  9. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (i) - Aggrey Mwanri
  10. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ii) - Kassim Majaliwa
  11. Waziri Wizara ya Fedha - Mustapha Mkullo
  12. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (i) - Gregory Teu
  13. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (ii) - Pereira Ame Silima
  14. Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Shamsi Vuai Nahodha
  15. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Balozi Khamis Suedi Kagasheki
  16. Waziri wa Katiba na Sheria - Selina Kombani
  17. Waziri Wizara ya Mambo ya Nje - Bernard Membe
  18. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje - Mahadhi Juma Mahadhi
  19. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi
  20. Waziri Wizara yaMaendeleo ya Mifungo - Dk. Mathayo David Mathayo
  21. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Mifungo - Benedict Ole Nangoro
  22. Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia -  Profesa Makame Mnyaa M'barawa
  23. Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia - Charles Kitwanga (almaaruf Mawe Matatu)
  24. Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Profesa Anna Kajumulo-Tibaijuka
  25. Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Goodluck Ole Medeye
  26. Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii - Ezekiel Maige
  27. Waziri Wizara ya Nishati na Madini - William Mghanga Ngeleja
  28. Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini - Adam Kighoma Ali Malima
  29. Waziri Wizara ya wa Ujenzi (Barabara na Viwanja vya Ndege) - Dk. John Pombe Magufuli
  30. Naibu Waziri Waziri Wizara ya wa Ujenzi - Dk. Harrison Mwakyembe
  31. Waziri Wizara ya Uchukuzi - (Reli, Bandari, Usafiri wa Majini) - Omary Nundu
  32. Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi - Athuman Mfutakamba
  33. Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara -Dk. Cyril Chami
  34. Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara - Lazaro Nyalandu
  35. Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Dk. Shukuru Kawambwa
  36. Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  - Philipo Mulugo
  37. Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dk. Haji Hussein Mpanda
  38. Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dk. Lucy Nkya
  39. Waziri Wizara ya Kazi na Ajira - Gaudensia Kabaka
  40. Naibu Waziri Wizara ya Kazi na Ajira - Dk. Makongoro Mahanga
  41. Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Sophia Simba
  42. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Umi Ali Mwalimu
  43. Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - Emmanuel John Nchimbi
  44. Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - Dk. Fenela Mukangala
  45. Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki - Samuel John Sitta
  46. Naibu Waziri  Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki - Abdallah Juma Abdallah
  47. Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Profesa Jumanne Maghembe
  48. Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Christopher Chizza
  49. Waziri Wizara ya Maji - Profesa Mark James Mwandosya
  50. Naibu Waziri Wizara ya Maji - Gerson Lwinge


NB: Nakala ya orodha hii iliyotolewa Ikulu inapatikana hapo chini ya picha ya Rais, (vipande  vitatu) bofya kuvikuza ili kuweza kusoma majina ya Mawaziri na Manaibu wao na Wizara watakazoziongoza).

UPDATE 1:
Audio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akitangaza Baraza jipya la Mawaziri linalotarajiwa kushika hatamu kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015. Mheshimiwa Rais alianza kuzungumza ilipotimu saa sita na nusu (EAT).

Pleya zipo mbili lakini ni audio moja, zimewekwa mbili ili kuongeza uchaguzi wa ile itakayosikika katika kompyuta yako. Bofya kifute cha play kumsikiliza...
Player 1

Player 2

Baraza linatangazwa sasa, nitakuwekeeni "audio" punde atakapomaliza kuzungumza Rais.
Tizama video katika ukurasa wa video kwa kubofya hapa (au kwenye picha)
Picture
Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akitangaza baraza la Mawaziri
 


Comments

DAVID MWAKA
24/11/2010 13:07

ongera mzee kikwete,sasa fanya kazi, mpe nafasi zaidi mzee magufuli akufanyie kazi nzuri, pia mwandae aje kuwa rais wetu kupitia ccm baada ya wewe kumaliza, ccm itashinda kwa kishindo,fanya kazi mzee tuko nyuma yako,kuwa mkali pambana na ufisadi rudisha heshima ya ccm

Reply
Patrick Sanga
24/11/2010 13:28

Baraza kwa ujumla ni zuri sana, tunawatakia uwajibikaji na ufanisi mzuri katika utekelezaji wa majukumu yenu. Nimefurahishwa na Magufuli kurudi kwenye barabara. Hongera Rais, Mungu awape nguvu na hekima katika utendaji wenu siku zote.

Reply
Mtui
24/11/2010 13:32

Hongera kwa aliyekushauri na hongera kwako pia kwa kusikiliza kwa makini na kutenda. Baraza ni zuri. Lakini ujue watu wanasema ni zuri (sana sana kwa sababu umemweka Magufuli mahali stahili), basi umlinde atachape kazi. This is one of the few good things you have done to Tanzanians. Lead the way and walk the talk. God Bless you

Reply
MBAKILE ROBERT F.
24/11/2010 13:38

Iapriciate the new baraza la mawaziri 2010

Reply
MATEPWENDE WOMAN
24/11/2010 13:58

yote kwa yote ni MAGUFULI KWA BARABARA NA BARABARA KWA MAGUFULI.MUNGU akubariki sana kwa hilo.yaani sasa tuna uhakika wa magari yetu kufika mpaka vijijini kabisa.

Reply
Juama H. Seif
24/11/2010 14:00

Baraza hilo ni zuri sana na hasa kuturejeshea Dr. John Pembe Mgufuli katika ujenzi. Ahsante sana Mhe. Rais.

Reply
24/11/2010 14:02

Hongera kwa kuwaacha mafisadi ila ulichelewa kumpa Mwakyembe wizara sasa big up sana kama Prof. Tibaijuka, Magufuli j. Pombe na Mkulo umewaweka sehemu muafaka. Chapeni kazi ili 2015 tusipate taabu tena mpaka tuchakachue. Big up bro.

Reply
Kingu
24/11/2010 14:03

Baraza la kawaida sana halina jipya, watu walewale, so no changes will be expected

Reply
veda
24/11/2010 14:04

Big up baraza kwa mfano prof. Tibaijuka, Magufuli J. Pombe, Mkulo umewafix sehemu mwake kabisa. Big up bro chapeni kazi sasa sio 2015 tena tuchakachue ndio tushine.

Reply
Hassan Ahmed.
24/11/2010 14:06

YAANI MACHOZI YANANITOKA SI KWA JINGINE LOLOTE ISIPOKUWA NI KWA FURAHA KUBWA ISIYO NA MFANO ILIYONIJAA KWA KITENDO CHA MHE. RAIS KUTUREJESHEA DR. JOHN PEMBE MAGUFULI KATIKA WIZARA YA UJENZI. YAANI MOYO WANGU UMEFARIJIKA MNO. AHSANTE SANA SANA SANA MHE. RAIS.

Reply
Valerian
24/11/2010 14:07

kuna mawaziri wa tano watafanya vizuri sana wengine tumewazoea

Reply
Veda
24/11/2010 14:08

Ila mkuu ameniacha hoi mbona katangaza haraka haraka sana au alikua na safari ya nje? Kwani ameshaanza ziara za nje??????? Mmmmmmmmm! utangazaji huu kwa kweli unatisha. Kwa anaogopa nini na yeye ndio mkuu wa nchi dola zote ziko chini yake sasa kulikoni haraka vile?

Reply
Abinoam
24/11/2010 14:11

Tutegemee nini chenye mantiki kwa umma ikiwa mawaziri walokuwepo awamu iliopita ni walewale na utendaji wao wa kazi wajulikana.

Sitegemei mambo makubwa kupitia baraza hili.

Reply
24/11/2010 14:12

Asante sana mheshimiwa kikwete kwa baraza zuri.Kweli kabisa unastahiki pongezi za dhati kwa kazi yako makini iliyotulia.Huu sasa ni mwanzo mzuri unaoashiria kuonekana utendaji mzuri wa 2010-2015.

Nimefurahi sana kumbadilisha Jumanne maghembe kutoka wizara ya Elimu,na kumuweka E.Nchimbi.Huyu mheshimiwa namtambua kiundani zaidi na nafahamu sana shauku yake katika elimu,siku za nyuma nilikimsikiliza sana speach zake,ni mtu anayeonekana yuko tayari kuleta sura mpya katika uwanja wa elimu na michezo.Na hii nafasi aliyopewa anafiti sana.hongera sana jk na sasa tumegundua kwanini balaza la mawaziri lilicheleweshwa kutangazwa,ni ili kupata mawaziri wanaostahiki na wenye viwango vizuri vya utendaji kazi katika nyazifa hizo.na baada ya kutimia hilo ukatangaza.wanasema wenyewe :MAMBO MAZURI HAYATAKI HARAKA.HUU MSEMO UMEONEKANA LEO KWETU TANZANIA.

Reply
Kiliwasha
24/11/2010 14:19

no changes but 4coming back Magufuli,da next Presdent

Reply
Chib
24/11/2010 14:20

Thanks, tumepata mahali pa kunukuu. Ila baraza bado kubwa ati!

Reply
moses
24/11/2010 14:20

bareza zuri only tunategemea uwajibikaji na usimamizi mzuri chini ya Rais aliyeliunda!!
Kama kutatokea kotokuwajibika katika wizara husika basi waziri husika awajibishwe na si kufumbiwa macho kama baraza lililopita.
Pamoja tutafika.

Reply
24/11/2010 14:22

magufuli na tibaijuka ni chapa kazi nzuri, ila mbona kina mama mlisema watapewa nyadhifa,naona kama wako 9 tu kama sijakosea, 50 yote wamama 9 ndo wanaweza? hapo tumedanganyika

Reply
DAVID MLYUKA
24/11/2010 14:28

MAGUFULI IS THE RIGHT CANDIDATE, NIMEFURAHI KUPINDUKIA- SASA BARABARA ZITAJENGWA KWA SPEED ISIYO YA KAWAIDA.

AHSANTE RAIS WETU

Reply
Emmy
24/11/2010 14:33

Baraza ni zuri kwani kuna wachapakazi hasa lakini sophia simba mmmmmhhh haya labda ataacha kusutana safari hii

Reply
Aggey Mrindoko
24/11/2010 14:33

mawaziri ni wengi mno, garama zao kubwa ukizingatia wengine si watendaji kihivyo.na hiyo no.ya wamama ni kidogo mno, au hakuna wamama wenye sifa waliochaguliwa wabunge,hata wa viti maalum, au hawana elimu, labda tuelimishwe.mlisema spika ni mmama na mnataka nyanja nyingi zishikwe na wamama,yako wapi, au ilikuwa janja ya kumtoa sita uspika?

Reply
mbise
24/11/2010 14:36

Asante sana rais JK kwa kutuletea Magufuli tena. Tunawaombea Mungu awape utendaji ulio distinction. Keep up our President tupo nyuma yako!!!!

Reply
Veda
24/11/2010 14:36

Kweli Maadam Anne mmedanganyika. 50 kwa 50 haitawezekana labda mrudi tena Beijing mkadai usawa. Ila namjua mheshimiwa atafidia hilo kwa kuwaweka ukuu wa wilaya na nyazfa nyingine. Usilalamike muundo wa serikali bado hili ni balaza la mawazili tuu bado sehemu nyingi za utendaji zinakuja nafikili 50 kwa 50 zitafika tuu.

Reply
JN The 1
24/11/2010 14:36

Magufuli, Tibaijuka, and Mwakyembe its PERFECT!

Reply
ANTANAMSU LYATUU
24/11/2010 14:38

Mheshimiwa Kikwete umefanikiwa kuwa kati ya mawazo ya wengi. Hamna wa kukosoa sana wala sio kupongezwa sana, baraza limelenga mawazo ya watu walau kwa zaidi ya 50%. TIBAIJUKA BIG UP, MAKUFULI SAFI, NDO WIZARA ZAO HIZO. TULITEGEMEA UWATUPE VIONGOZI WENYE TUHUMA ZA UCHAFU, HONGERA SANA KAWAACHA KWANZA WAJISAFISHE. LAKINI BARAZA BADO KUBWA JAMANI.

Reply
Sam Taifakubwa
24/11/2010 14:38

Hakika nimekuwa na imani na serikali yetu MHE. RAIS KUTUREJESHEA DR. JOHN PEMBE MAGUFULI wizara ya Ujenzi akisaidiana na Dk. Harrison Mwakyembe HAKIKA barabara zetu hazita chakachuliwa tena mjini hata vijijini na ninaamini makazi yetu yataboreshwa chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Profesa Anna Kajumulo-Tibaijuka MHE. RAIS YOUR THE MAN!

Reply
Veda
24/11/2010 14:39

Hivi mheshimiwa Sita hapo vipi panamfaa kweli? Au danganya toto tuuu? Mi nilitegemea apewe sheria au mambo ya ndani akatoe uozo ulioachwa na wakina mashiiiiiiiiiiiiii!

Reply
Mzeee wa Shamba
24/11/2010 14:41


Baraza zuri ila kachafua sehemu moja tu- kamrudisha Mahanga , halafu kamwacha pROF.Mwakyusa.

Reply
Asimwe
24/11/2010 14:43

Hongea Kikwete kwa hilo baraza ulilochagua, hasa kwa Magufuli na S. Sitta umepatia. Lililopo wawezeshe kuchapa kazi ili kurudisha heshima ya chama iliyopotea, ili waimu ijayo msije kuchakachua tena bali mshinde kihalali.

Reply
Dogo Jani
24/11/2010 14:44

A good cabinet. now we want to see them performing. Hasa hasa waziri wa wizara hii nyeti ya mambo ya ndani ya Nchi, Hapo nina mashaka, kwani mara zote iliposhikiriwa na wenzetu kutoka Z'bar, performance ilikuwa ni "absolutely poor" Sasa sijui kama huyu anaweza kuonyesha tofauti. As the head of the state, you have to pay a special attention to the minister of this ministry to ensure his performance and accountability.

Reply
veda
24/11/2010 14:44

Kiukweli amepunguza balaza maana lililopita walikuwa 60 sasa hivi ni 50 amejitahidi kazi ni nyingi jamani akipunguza sana kazi zingine zitalala. angeweza weka hata 30 lakini je unajua ukubwa wa nchi yetu na idadi ya watu wake? Mi nafikiri hao wanatosha kuwaombea tu afya na uzima kwa mwenyezi mungu ili wachape kazi na mwisho watuletee maendeleo ya mtu mmoja mmoja, familia na taifa kwa ujumla.

Reply
Sam Taifakubwa
24/11/2010 14:45

Samahani Mhe. RAIS umemsahau PRO.DAVIDI MWAKYUSA kwani si ndio yeye alimaliza matatizo ya migomo ya madaktari nchi hata akaokoa maisha ya watanzania wengi?

Reply
Dismas
24/11/2010 14:49

sitegemei kipya sababu timu ni ile ile tofauti ni wachezaji waliokuwa kwenye benchi wameingia uwanjani isitoshe naodha wake ni yule yule.

Reply
B Chacha
24/11/2010 14:51

Kiujumla baraza ni zura na binafsi nimefurahia kwa Mh. Rais kumrudisha Mr Magufuli wizara ya ujenzi na naibu wake akiwa mpambanaji Mwakyembe.Hii inaashiria kuwa mwanzo wa mwisho wa wale walozoea kufanya kazi kwa uzembe,ufisadi hasa wakati wa kutoa tender za ujezi wa barabara umefika.

Ila sijaelewa vizuri kuhusu hizi wizara zinazohusu elimu naona kama nyingi na zinachanganya.

Nevertheless, I ve been impressed by the new cabinet.

Reply
24/11/2010 14:54

baraza zuri only tunategemea uwajibikaji na usimamizi mzuri kutoka kwa Rais aliyeliunda baraza hilo!!
Kama kutatokea kotokuwajibika katika wizara husika basi waziri husika awajibishwe na si kufumbiwa macho kama baraza lililopita.
Pamoja tutafika.



Reply
Ntamobwa.
24/11/2010 14:56

NAPENDA TU NIWAKUMBUSHE KUWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LINA JUKUMU KUBWA. PAMOJA NA MAMBO MENGINE MUHIMU PIA WASIMAMIE AHADI ZA MH. RAIS KAMA NILIVYOZIREKODI HAPA CHINI.

AHADI ZA Kikwete KWENYE KAMPENI 2010 - 2015.
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hatia ya kuua albino- Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
21. Kulinda Muungano kwa nguvu zote-Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
28. Kununua "bajaji" 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za Sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
36. Kulinda haki za walemavu- Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa mpaka Singida-Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
44. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
45. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
46. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
47. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
48. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
49. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
50. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
51. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
52. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
53. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
54. Kutokomeza malaria 2015-Bunda, Mkoa wa Mara
55. Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo, Iringa
56. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
57. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
58. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
59. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
60. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbamba-bay Ruvuma
61. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) &n

Reply
Ntamobwa
24/11/2010 15:01

62. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
63. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
64. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
65. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
66. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
67. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Reply
Leonard Cheyo
24/11/2010 15:05

Hongera kwa kazi nzuri, baraza zuri sana japo bado ni kubwa mno. Ni lazima tufikie sehemu tubane matumizi. Tukumbuke kuwa, wapo pia makatibu wa wizara n.k ambao bado wanawasaidia mawaziri majukumu mengi sana, hivyo sioni sababu ya baadhi ya wizara kuendelea kuwa na manaibu mawaziri wawiri. Kikubwa ni kuwa awekwe waziri mwenye msuri na akili na pia awekwe naibu msaidizi mzuri9 mmoja tu na kazi itakwenda vizuri. Lingine ni kuwa hebu tufikie sehemu tuwe na wizara ya elimu/sayansi na teknolojia endelevu. Sioni sababu ya wizara hizi kuwa zinapokea mabadiliko ya mara kwa mara. Huu ni mhimiri wa nchi.
Mwisho ni kuwa tufikie sehemu tuwe na wizara zisizobadilikabadilika ili kubana matumizi ya ubadilishaji wa nyaraka mbali mbali. Mfano kama mwaka huu tuliandika na kuchapisha nyaraka kwa nembo ya wizara fulani, miaka michache baadaye idara hiyo inahamishiwa kwingine, hii inatugharimu pesa nyingi

Reply
vicky
24/11/2010 15:06

hongera mheshimiwa kikwete kwa baraza zuri la mawaziri magufuli hakuna shida hapo safi!mwakyembe,tibaijuka lakini tunasubiri uwajibikaji usiwafumbie macho wakiharibu!

Reply
omox
24/11/2010 15:08

ongera dk.maghufuri ume represent well wasomi wa Udsm wizara inakufaa sana hiyo

Reply
madale danie
24/11/2010 15:08

hongera mkuu wa nchi,yote tisa ila SITA umemchakachua. Hongera kwa JOHN POMBE hapo ndo pahala pake.

Reply
Ntamobwa
24/11/2010 15:08

PIA YAPO MAZURI YA KUCHUKUA KWA WASHIRIKA WENZA. MSIYASAHAU!!

Dk. Slaa (CHADEMA)
1. Kujenga nchi isiyo na ufisadi
2. Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
3. Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
4. Kutoa huduma bora za afya bure
5. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
6. Elimu bure kuanzia Chekechea hadi Kidato cha Sita
7. Katiba mpya ndani ya miaka mitano

PROFESA LIPUMBA (CUF)
1. Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
2. Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
3. Kuunda Serikali shirikishi
4. Kusimamia rasilimali
5. Kuimarisha miundombinu
6. Kusimamia na kuboresha afya
7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
8. Kurudisha chakula cha bure mahospitalini

Reply
Mtanzania
24/11/2010 15:09

Tafadhali ukifanya reshufle uwaondoe hawa: Sophia Simba, Emmanuel Nchimbi, Makongoro Mahanga, Prof. Jumanne Maghembe, Shukuru Kawambwa (huyu hana neno sana ila kalala mno)na Aggrey Mwanri (Muongeaji zaidi ya Mtekelezaji).

Reply
Sam Taifakubwa
24/11/2010 15:12

Nashukuru sana ndugu Ntamomba kwa kutukumbusha hizo ahadi za MHE. RAIS pia niwashauri watanzania wenzangu yatupasa kuwaombea hawa viongozi wetu ili watende mema kwa watanzania wote pasipo kujali udini, ukabila na tofauti ya vipato.

Reply
NIALI, HASSAN
24/11/2010 15:15

Baraza ni zuri,Magufuli, Tibaijuka, Mwakyembe BIG UP SANA!

Reply
Suleiman
24/11/2010 15:18

Kwa kweli "I AM EXTREMELY HAPPY" kwa John Magufuli kurejeshwa tena katika Wizara ya Ujenzi maana ni mchapakazi ile mbaya. Kama asingebadilishwa wizara hiyo leo hii barabara zetu zingekuwa mbali sana kiuzuri na hata wingi wa kujengwa na kukarabatiwa. Tunakushukuru sana Mhe. Rais kwa kuturejeshea mtu wetu katika Wizara ya Ujenzi. Welcome back MAGUFULI, kwa kweli tuliku-miss sana.

Reply
Muyif
24/11/2010 15:20

Umejitahidi mzee

Reply
musira amin
24/11/2010 15:25

hongera kwa baraza la mawaziri, lakini nini hiki wizara za elimu mbili?
wizara ya mambo ya ndani inahitaji mtu wa bara huu ni wakati wa kuwa serious ,yes tunaubeba muungano but remeber charity starts at home!

Reply
KULYEMBA WA SASAWALA
24/11/2010 15:28

Hongera sana Mheshimiwa rais Kikwete kwa kuturejeshea Dk. Magufuli katika Wizara nyeti ya ujenzi wakisaidiana na mwanasheria, Dk. Mwakyembe, kwani tunahakika kuwa the so-called "Mtwara corridor" will come into reality very soon.

Reply
Ignas
24/11/2010 15:32

Kila la kheri, we need changes and not words katika kazi. Mabadiliko katika maendeleo ya nchi yanawezekana endapo viongozi wa juu watapunguza matumizi yasiyo ya msingi na kuangalia zaidi suala zima la maendeleo ya nchi.

Reply
24/11/2010 15:54

Mbona wana siasa wengi umejaza? nilitegemea watendaji kama magufuli na Sitta,,hata Tibaijuka atasaidia kwa uzoefu wake! tuombe mungu na tuweke majungu na visasi pembeni tujenge nchi yetu

Reply
Samwel
24/11/2010 15:56

Kwa kweli baraza ni zuri hasa kwa kurudishwa kwa mh John magufuli katika nafasi aliyokuwa nayo mwanzo tunampongeza rais kwa uteuzi huo wa baraza jipya sasa tuone mabadiliko na maendeleo ya kweli

Reply
msyani
24/11/2010 15:56

Kwa upande wangu ukiachilia mbali Magufuli na Tibaijuka baraza lake halina jipya kwani ndani wamesheheni vihiyo (wenye vyeti feki)ambao wameshindwa kutafuta vyeti kwa kusoma badala yake wame nunua na kubadili majina.Je kuna jipya hapoooooooo!

Reply
mmasai olesai
24/11/2010 15:57

Hongera kwa barza jipya, tunaona vijana na tunaamini watchapa kazi,dr nangoro mmasai kwa ng,ombe umempatia, anna,, na maghufuli pake. sita sinahakika ngawa ni mchapakazi na mwadilifu angepewa sheria au mambo ya ndani aondoe uozo uliachwa. Mungu ibari Tanganyika na watu wake

Reply
Buswelu
24/11/2010 16:02

Uteuzi ndo huo!I see hongera nyingi sana ni kwa magufuli, even m namkubali na baadhi yao kama mwakyembe.

Reply
nguvu
24/11/2010 16:05

Ni dhahiri maendeleo chini ya uongozi wako kama Rais wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa CCM yanawezekana. Baraza hili ulilolitangaza leo linathibitisha hilo. Hongera Mh. Rais kwa uteuzi huu mzuri na kwa kukata kiu ya watanzania wengi. Tafadhali wasimamie kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi ili kutekeleza yote yaliyoko kwenye ILANI ya Uchaguzi ya CCM na kuiletea nchi maendeleo zaidi. Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika!

Reply
wado sam
24/11/2010 16:09

Kwa upande wangu baraza la mawaziri ni zuri. Tunampongeza mh Rais kwa uteuzi huo tunategemea kuona mabadiliko katika utendaji kwa awamu hii.

Reply
Duh
24/11/2010 16:17

Hili baraza ingawa kweli lina wachapakazi lakini ni kubwa sana.
KWA MFANO hakuna umuhimu wa kuwa na wizara mbili zinazoshughulikia usafirishaji. Rais amevunja ile wizara ya maendeleo ya miundombinu (Infrastructure devpt) na kutengeneza mbili: Wizara ya Ujenzi (Works) na Wizara ya Mawasiliano na uchukuzi (transport). Haiingii akilini anawaza nini hapa. Tunahitaji wizara moja itakayounganisha vyombo vyote vya usafiri kwani vinategemeana. Hapa ndio anatengeneza barriers kwa watendaji wake. Kwa mfano uakiangalia sera ya usafiri wa tanzania (Transport Policy) inahusu nyanja zote za usafiri. Ntaendelea kuwalaumu washauri wake kwani wanamshauri Rais vibaya. Tunahitaji wizara moja tu ya usafirishaji tena iongozwe na Magufuli. Labda angeweka manaibu wawili ningemwelewa kidogo. Lakini aaaagr, kuna tatizo hapo. Jamani sio kila mtu awe waziri.....na hawezi kumfurahisha kila mbunge kwa kumzawadia uwaziri.

Reply
Mwangomo W.J
24/11/2010 16:58

Mheshimiwa Rais, nakupongeza kwa uteuzi wa Baraza zuri la mawaziri hasa kwa kumteua nd yetu Pombe Magufuri.Nina hakika kila Mtanzania amefurahi sana. Pamoja na uteuzi huo vipi Prof.Mwakyusa umemruka katika kumtaja ama vipi !! ?

Reply
issa
24/11/2010 17:04

am not expecting wonders, they will do "madudu" as normal believe me. Hao madaktari (PHDs)have done nothing compared to their education. Magufuli hawezi kuzuia mikataba mibovu ya wakandarasi na barabara, madaraja kuwa chini ya kiwango- Mfano; Daraja ni jipya lakini halina sehemu ya watembea kwa miguu, mengie magari mawili hayawezi kupishana kwa wakati mmoja.

Reply
mvuvi
24/11/2010 17:09

nimesikitika sana kuona sector ya uvuvi ikiburuzwa tena safari hii sijui inarejea tena kwenye mali asili na utalii na sijui kwanini iliondolewa huko awali. Nayasema haya maana athari zake kiutendaji ni kubwa sana. Huu mchezo wa kubadili muundo wa wizara utazamwe upya. sisemi zibakie kama zilivyo kuwa lakini tufanye utafiti wa kina kabla ya mabadiliko ili yawe yenye tija

Reply
Byaeta Oboo MWNEMBUKA
24/11/2010 17:13

I think the cabinet is large. The ministers with their deputies along should not reach fifty. Imagine Western countries are comparatively well-off, but, the composition of their ministerial cabinets is smartly smaller.

Reply
E.T. Mbunda
24/11/2010 17:24

hongera sana mheshimiwa rais kwa baraza jipya la Mawaziri hasa kwakuwateuwa mgufuli na mwakyembe kushika wizara ya ujenzi

Reply
issa
24/11/2010 17:25

Byaeta, yes-the cabinet is large and the country also is large. What did you think, twenty?

Reply
LEKAMU
24/11/2010 17:27

Hongera sana RAIS WETU maana umefanya kazi kubwa kwa kuunda BARAZA ZURI;na hasa nimefurahi sana kutuletea WAZIRI PROF. ANNA TIBAIJUKA. MUNGU AMTIE NGUVU KATIKA KUIENDESHA WIZARA HII NYETI NA HASA KATIKA KUPANGA MIJI. BIG UP

Reply
24/11/2010 17:38

Nashukuru sana kwa Magufuli kurudishwa katika Wizara Nyeti ya Barara, kwa kweli wananchi wengi wanaimani na Magufuli, Hizi kampuni feki feki Zinazochakachua Mabarabara yetu zikae macho. au zifutwe kabisa. Wasomi Engineers tutarudishiwa heshima yetu. Big up Rais JK. upo juu kama Matawi

Reply
BIGOBIGO WA MPANDA
24/11/2010 17:42

Big up president! tunauhakika ujenzi wa barabara ya tunduma-sumbawanga hadi mpanda itakamilika ndani ya miaka 2 badala ya 3 na barabara zote zilizotajwa kwenye mpango wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya miaka 10 zitakamilika-MUGUFULI NA MWAKYEMBE NI MAKINI

Reply
Bernad Matinda
24/11/2010 17:54

I am so impressed by your cabinet your excellency.Its full of intellectuals people who can bring changes in our nation.
Meanwhile i wish you successfully implementation of your promises which i believe they are implementable under the new cabinet.

Reply
Dogo Jani
24/11/2010 18:07

Mh. Rais, hivi unayasoma haya? Kwa macho ya watanzania wengi unaowaongoza na wanaotoa maoni yao hapa, cha maana ulichokifanya ni kumteua J. P. Magufuli, Sitta na mwakyembe. Na ndiyo maana ya hongera na pongezi zote hizo. Hivyo kwa hao wengine ni ziro, hatutegemei mabadiliko. Hivyo usidhani baraza lote ni safi.

Reply
Dogo Jani
24/11/2010 18:08

Mh. Rais, hivi unayasoma haya? Kwa macho ya watanzania wengi unaowaongoza na wanaotoa maoni yao hapa, cha maana ulichokifanya ni kumteua J. P. Magufuli, Sitta na mwakyembe. Na ndiyo maana ya hongera na pongezi zote hizo. Hivyo kwa hao wengine ni ziro, hatutegemei mabadiliko. Hivyo usidhani baraza lote ni safi.

Reply
jaka
24/11/2010 18:08

kwa kiasi umejitahidi ila siwezi kusifia tusubiri utendaji wa hao mawaziri but sitta huko ulikomtupa sio kabisa ungempa sheria na katibu or mambo ya ndani na simba na baadhi ya wenzake hawastahili kurudi serikali kwani wametuchosha vilevile watanzania tumechoka tunataka katiba mpya. mawaziri ni wengi so bado matumizi ya serikali yatakua makubwa so hatuwezi kusonga mbele kwa staili hii

Reply
wazee wa one way
24/11/2010 18:13

baraza bado kubwa sana mzee kikwete

Reply
ten ten house embassador
24/11/2010 18:39

ok. let us see

Reply
kingkitia
24/11/2010 18:56

kazi ipo tunaamini Makufuli amepewa funguo mwandosya kazi anayo, ila mwakyembe wamem bania kwa kweli kwanini wamemficha pale wakati anao uwezo wakuongoza wizara kibao tuu, okay kila la kheri nchimbi ndoto zako zimetimia ila je utatutimizia sisi vijana

Reply
obadia bishoge
24/11/2010 19:35

Baraza la mawaziri lina mwelekeo ila tu katika wizara ya elimu sina hakika na mawazili walioteuliwa kushika nafasi hiyo maana ni wizara inayoitaji utaalamu zaidi ili kuendeleza elimu maana ndiyo msingi na kiongozi wa wizara zote.
Nashangaa pia kusikia jina la Mr Lukuvi kupewa wizara huku pia ni mkuu wa mkoa wa Dar, nashauri achague upande mmoja maana huwezi kutumikia mabwana wawili wakati mmoja.
Kwa Dr Magufuri amewekwa katika nafasi yake. Nafikiri barabara zitajengwa kwa ufasaha na Prof.Tibaijuka anaweza katika wizara aliyopewa.
Sasa kazi kwao walioteuliwa kutumikia wananchi bila unafiki

Reply
Steven Kwembe
24/11/2010 20:19

Me sina kinyongo na baraza jipya,kwani naona lina watu makini na wasio na sifa mbaya. Ila wasiwasi wngu ni kwa Mheshimiwa Mkulo,kwani matumaini ya kurejesha Shirika la Bima la Taifa(N.I.C)katika hali yake ya zamani iko mikononi mwake,hivyo naomba Mungu awe mzalendo zaidi.

Reply
bube
24/11/2010 20:21

kiukweli ni mawaziri wachache katika baraza hilo watafanya vizuri pia mwakyembe na sita hawakustahili kuweka katika nafasi hizo bali wangepewa wizara nyeti kwani ni watenda kazi wa kweli

Reply
Selya
24/11/2010 20:31

Watanzania tuna matumaini makubwa kuwa mawaziri hawa hawatakuwa marafiki wa mafisadi na ufisadi.

Reply
Kajuna ramson
24/11/2010 20:34

Am anxiety to see wather they'll be with commited 2 their duty given but why to entitle lukuvi with two posts

Reply
halima
24/11/2010 21:04

Rais wetu tunakushukuru sana kwa baraza lako la mawaziri lakini huyu Sophia Simba mswahilli sana anaweza kazi moja tu ya vidole juu huyu. Ana Kilango vipi baba?? MAGUFULI/MWAKIEMBE fanyeni kazi na mawaziri wengine waige, msicheke na makandarasi 10% is out of order now jamani!!

Reply
kiseru
24/11/2010 21:15

Mambo yote yameenda vizuri ila ingefaa kama Mama Gaudensia Kabaka angebaki kwani wote wakiwa wageni kwenye hiyo wizara itawapa shida sana kwa wanafunzi kwani ni idara nyeti sana katika nchi hii, hasa ukizingatia wanafunzi wa elimu ya juu.

Reply
christopher
24/11/2010 21:49

Baraza ni zuri hasa kumwondoa maghembe elimu lakini sijajua kawambwa mikakati yake itakuwa ni ipi.But big up president

Reply
Jina
25/11/2010 00:48

Hongera ni nyingi kama za 2005 lakini mtaishia kulalama siku ya mwisho.

Reply
Kishuri
25/11/2010 01:48

Shukrani sana muheshimiwa Rais kwa kuunda baraza hili la mawaziri lenye wachapa kazi. Hongera sana engineer NUNDU kwa kuaminiwa na rais Kikwete.

Reply
Ng'wanamvanga
25/11/2010 06:08

Baraza ni kubwa sana kwa nchi yenye deficit ya bajeti kama TZ. Otherwise, hongera kwa kuangalia taaluma na uwezo wa baadhi ya uliowachagua.

Umetibua hali ya hewa kwa kumrudisha Sofia Simba, Makongoro Mahanga, Maghembe, na Nchimbi na kumwacha Prof. Mwakyusa. Uhamuzi ni wako na chama chako maana madudu yataongeza wapinzani bungeni 2015.

Reply
Lenga
25/11/2010 06:59

Natoa pongezi kwa uteuzi wako wa Baraza la Mawaziri. tunataraji kuwa watendaji wetu watasoma alama za nyakati kwa kuelewa mahitaji ya Watanzania. nakupa BIG UP SANA

Reply
Jonh Kimeta
25/11/2010 07:45

Hongereni sanaana wana CCM kwakujipanga upya na Serikali yenu mpya...sasa kikubwa kwa Mh Rais husia wangu kwako najua siku za nyuma tayari uliliona ilo...MAWAZIRI wako wengi wao km walikua wako LIKIZO,safari hii usikubali kabisa yatokee km yale ya kipindi kile...huo ndio husia wangu.KAZA BUTI

Reply
Hanti
25/11/2010 08:28

magufuli hakuna wizara ya kumshinda, mtampeleka kokote lakini kazi ni moja tu aliyonayo kichwani mwake ambayo ni mabadiliko ya kweli...huyo hata ukimpata ikulu, namaanisha urais, atamudu tena kwa kiwango cha hali ya juu...ccm tusifanye makosa mwaka 2015, iwe kumtoa katika ngazi ya chama atakapoomba kupitishwa na chama kugombea urais ktk ngazi ya taifa, au kutomshauri agombee kama yeye hataonekana mapema kutotaka kufanya hivyo...tuombacho ni uhai toka kwa muumba tu basi...vinginevyo tuwakabithi wapinzani nchi maana watu kama dr.slaa anaonekana kuweza hiyo kazi...wapo wazuri kiutendaji kama magufuli na tusiipoteze tunu hii bila kuitumia kwa ngazi ya urais

Reply
Lameck NFFI
25/11/2010 08:36

Hongera rais but kumbuka muwe makini na utoto wa mama,kwani hiyo tumeizoe kwa serikali yetu.swali uvuvi mbona haikonekani wakati ndo kitovu cha watu wa kanda ya ziwa?

Reply
MAMA JOSHUA
25/11/2010 09:06

Nawapongeza washauri wa Raisi kwa kumshauri asiwarudishe wale wa Richmond na Rada, Rais usiangalie sura angalia nch inataka nani,

Reply
ERICK JK
25/11/2010 09:21

Nakupa Pongezi kwa uteuzi wako wa baraza la mawaziri na Manaibu Mheshimiwa Rais tunatarajia mabadiliko,utendaji kuwa bora na kuleta maendeleo kwa watanzania.Hongera Sana.BIG UP!!!!!!

Reply
Mtanzania
25/11/2010 09:33

Jamani,upinzani si kupinga kila kitu.

Hili baraza ni bomba. Dr.Kikwete, kwa kusema ukweli amefanya kazi kubwa sana katika awamu yake ya kwanza, na tuna imani kubwa naye kwa awamu yake ya mwisho.
Hongera kwa uteuzi makini wa baraza, na ninyi mawaziri msimwangushe Rais wetu tafadhali.

Reply
Mpenda nchi.
25/11/2010 09:39

Jamani,sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Huyu Dr.J.P.Magufuli anafaa, na ni hazina yetu sisi wapenda CCM.Namaanisha, Urais 2015!

Sisi ni kumwombea tu kwa Mungu.Ameni!

Reply
erick
25/11/2010 09:54

kwa kumteua mama Anne Tibaijuka wizara ya ardhi nafikiri kutakuwa na mabadiliko ya tija msukumo usiwe kupima na kugawa viwanja tu.kama ilivyo sasa ila kujenga makazi bora.nadhani kwa uzoefu wa huyu mama alioupata shirika la makazi tutarajie sera bora za makazi.brovo jk .pia pale ujenzi umefanya poa.pombe na bro harrison.patamu!tanroad wamezoe kula kodi zetu.

Reply
Katundu, Kyaka
25/11/2010 09:55

Nampongeza Kikwete, lakini umefanyaje kumwacha mama yangu Asumputa ambaye alikuwa kwako Ikulu? Si unajua aslimia 50 kwa 50?? Asumpta Ofisi ya Rais uratibu wa safari za rais na ukaifanya wizara mpya? Maana bado hatujaona mapya katika baraza lako bado ni kubwa, bora ungeunda hata hiyo ya kuratibu safari zako za nje.

Reply
Obeid
25/11/2010 10:03

Ni baraza la kujifunza zaidi kuliko kutenda kazi,lakini kwa mawaziri kama watano hivi ni safiiii saaana!

Reply
25/11/2010 10:11

Hakuna jipya, hakuna mkakati, mipango ya miaka mitano mitano haitatufikisha popote, baraza la kunyamazishana,za Sitta kupewa wizara ni RUSHWA. Kama ni mwanasiasa aliyekomaa asingekubali uteuzi huo, lakini kwa vile anaendekeza njaa, aliupokea kwa mikono miwili nadhani.

Kwa jinsi hii tanzania yenye neema itaishia midomoni mwa wana siasa tu.

Reply
MAMA VP
25/11/2010 10:12

nakupa pongezi kwa uteuzi wako kwa ajili ya waziri magufuri,Sita na Mwakyembe ila kwa issue ya Sophia Simba Umechemsha!!!wapo mawaziri kama mama Sitta angefaa hiyo position! kwa mpango wa barabara za hewani sasa zitajengwa mkimwezesha waziri Magufuri,na kama hazijengwi basi lilikuwa changa la macho kwa wananchi kwa serikali iliyopita na sio kwa waziri husika Magufuri tunajua ni muwajibikaji muwezesheni jamani..

Reply
Mwanachi
25/11/2010 10:18

Baraza linaweza likafanya kazi nzuri,ila isirudiwe ile ya 2005 baada ya kuunda baraza zuri,baadae akaanza kuchomekea wazee na mafisadi hadi mambo yakatufika yaliyotufika.Mimi naliona ni zuri ingawa kuna vichwa viwili kavisahau ma prof.wawili wa awamu iliyopita sitawataja kwa majina,ila wanatoka nyanda za juu kusini.

Reply
Makyami Tenga
25/11/2010 10:29

Mheshimiwa Dr. Kikwete. umefanya uteuzi wa busara kwa kumrudisha Dk. John Pombe Magufuli kwenye wizara yake ya zamani ya ujenzi na barabara kwani anaimanage ipasavyo. Mungu akutie Nguvu zaidi Dr. Magufuli.Tuna Imani na wewe.

Reply
CHRISTIAN C.M.
25/11/2010 11:33

BARAZA HILI LAWEZA KUFANYA VIZURI, ILA KUNA VICHWA TULIVITEGEMEA KUVIONA, MFANO MZURI NI PROF MWAKYUSA, WENGINE NAWEZA KUMPA KIKWETE BIG UP,ISIPOKUWA KABAKA JAMANI SIMPENDI, HASA ALIPOSHINDWA KUHANDLE MGOMO WA CHUO NA ALIPOTOA TAARIFA CHAFU YA KUWARUDISHA WANAFUNZI CHUONI, WASOMI MLIOKUWA VYUO MTANIUNGA MKONO. NAFIKIRI HABARI HIZI AKIZIPATA ATAJIREKEBISHA KWA WIZARA MPYA ALIYOPEWA

Reply
MUSHI
25/11/2010 11:40

Akiweza kuwa serious na hii timu aliyoiteua ndugu yetu Kikwete anaweza kukijengea CCM jina jipya., ila ndugu kuwa makini na ahadi ulizotoa, watanzania hatutaki mbwembwe, USIPOTIMIZA, utampa wakati mgumu sana ajae nyuma yako.. kwani sielewi kama ataweza kuongea na watanzania wenye machungu ya maisha bora. umeona maeneo ya town tulivyokukana kama hatukujui vile,.

Reply
Manumbu D
25/11/2010 11:46

Napongeza raisi kwa uteuzi huo na nimefurahishwa sana kwa kumteua bwana Pombe Makufuri kwa kumpa wizara ambayo aliweza kuimudu kwa kipindi cha nyuma, zaidi nategemea uwajibikaji mzuri kwa mawaziri ili tuweze kuijenga nchi yetu kwa miaka mitano ijayo, tuache tofauti za kisiasa, kwani kazi ni moja tu kuijenga nchi yetu.

Reply
Lucky
25/11/2010 12:00

Baraza ni zuri ila umekosea sana kumwacha Mwakyusa, labda umepata sumu kwa wale wasiopenda maendeleo ya nchi na kutokubaliana na misimamo ya Mwakyusa. Nakupa pongezi kwa kumpiga chini Msolla hana sifa nzuri katika jamii iliyo karibu naye hivyo hakufaa kabisa kuwa katika ngazi ya juu ya uongozi katika nchi, ninahakika wengi wamefurahiya uamuzi wa kumtoa katika baraza la mawaziri.

Reply
Lucky
25/11/2010 12:07

Hongera mama Tibaijuka, tunategemea kuona mabadiliko makubwa katika masuala ya makazi kutokana na international experience ulionayo.
Jitahidi sana kutoa ushauri , mapendekezo na kusimamia mikakati inayowekwa katika suala zima la makazi bora kwa watanzania. Sualal la kuwabomolea nyumba watu na kuwapa fidia wakajenge wanakojua muachane nalo maana walio wengi hushindwa kujenga na kuishia kurudi katika makazi duni kuliko waliokuwa nayo. Ushauri wangu ni kuhakikisha pale ambapo ardhi inabidi kubadilishwa matumizi kwa faida ya nchi basi hao wanao hamishwa wajengewe nyumba na kukabidhiwa na si kupewa pesa maana waliowengi huongezewa umaskini wa makazi na kuharibiwa "livelihood" yao

Reply
Mama Iku
25/11/2010 12:55

Rais umeweza kwa Magufuli na wachache wengine, ila Mwakyembe na Sita in changa la macho. Maumivu umetuma kwa kumuacha Prof Msola na Dr Mwakyusa, liaaaaaaaa Sophia Simba Umechemshaaaa baba

Reply
Mkereketwa
25/11/2010 13:02

Hivi inakuwaje kumpa nafasi Sophia Simba na kuwaacha waadilifu kama Prof.Mwakyusa na Prof.Msola?ambao kiutendaji walikuwa juu na uadilifu pia walikuwa juu?Hapo Rais liangalie kwa upya maana isiwe ndiyo kuiuza CCM kwa wapinzani bila wewe mwenyewe kujua.

Reply
cloud
25/11/2010 13:18

nampongeza mheshimiwa raisi kwa kuteua baraza iamara na makini na imani litaweza kutatua matatizo ya wananchi

Reply
Lenga
25/11/2010 14:26

Nashauri baada ya uteuzi wafanyakzi wa Wizara watoe msukumo katika kuwasaidia kwa dhati Wah. Waziri na Wah. waliobaki wote washirikamane katika kutafutia maisha bora Watanzania kwani mwisho wa siku sote tutapimwa kwa michango tuliyoitoa kwa Watanzania . mafanikio yetu yapimwe kwa waajibikaji wa kila mmoja wetu na wala si Mawaziri pekee. kengele imepigea na Mh. Rais hivyo wote GET READY GO Ifikapo kipindi cha tathimini tupimiane sote BIG UP RAIS - "OBEJA"

Reply
U S MAMUYA
25/11/2010 14:54

HoAsante kwa kumwona Mr Teu

Reply
ISSA
25/11/2010 16:43

MAWAZIRI NI WALE WALE SO HAKUNA MABADILIKO NDIO WALE WALE

Reply
Big Foot
25/11/2010 16:46

Wahusika!Mheshimiwa Rais ana mengi ya kupitia kuliko wasaa wa kupitia kurasa hizi,mjitahidi kuhudhurisha maoni haya kwake kwa ufupi ili naye ajivunie umahiri wake katika uteuzi alioufanya.Pombe na Mwakyembe mnaonekana kung,ara, tafadhali msimwangushe Rais wananchi wanategemea ukombozi wenu.

Reply
Elly
25/11/2010 18:02

Huyu jamaa bado ajajifunza kabisa ,umeongeza mikoa kibao na ahaadi tele bado unakuwa na baraza lenye watu lukuki,je ni kweli tutakuwa katika maisha bora????
Kaka acha hizo,unatuweka pabaya.

Reply
tuse
25/11/2010 19:45

huyu mary Nagu wa nini tena jamani? amechosha naona na bibi wa mipasho karudi sophia simba

Reply
subuga
25/11/2010 21:44

Hongera JK
Kujikwaa sio kuanguka na kosa ni kurudia kosa. Nakushuru kwa kumteua Magufuli kwa wizara uliyomueka, hapo 100%. Tunamtakia kila la kheri pro, Anna, atatupa uzoefu wa Umoja wa Mataifa.wale ambao hawakupata tunaomba tuwape ushirikiano mzuri, shida yetu ni Tanzania inayosonga mbele na sio ubingwa wa kukosoa tu.
JK Tunakutakia mafanikio mema.
Ushauri- Tuanze sasa kuandaa viongozi wa kwenda ikulu 2015 watakaoshinda Upinzani kwa 70% na zaidi

Reply
monica mwalutanile
30/11/2010 16:26

Nakupongeza mhe rais kwa uteuzi makini wa baraza la mawaziri hasa kwa magufuli kumpa nafasi inayomfaa zaidi

Reply

Your comment will be posted after it is approved.


Leave a Reply