Rais Mteule, Dk. Shein kupitia CCM ameshinda kwa jumla ya kura 179, 809 sawa na 50.1% ya kura zote, il hali Maalim Seif kupitia CUF amepata kura 176, 538 sawa na 49.1% na zilizobaki ni za vyama vingine.
Ilipofika zamu ya Rais Mteule kuzungumza, naye alitoa pongezi kwa Maalim Seif na kupongeza zoezi zima la uchaguzi jinsi lilivyoendeka. Pia ametoa ahadi ya kushirikiana na wote katika ujenzi wa Zanzibar mpya kwa mujibu wa maridhiano mapya ya uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar.
JUMLA YA KURA ZILIZOPIGWA ni 364,924
KURA HALALI ni 358,815
KURA ZILIZOHARIBIKA ni 6109
DK ALI MOHAMMED SHEIN (CCM) amepata 179,809 sawa na 50.1%
MAALIM SEIF SHARIF HAMAD (CUF) amepata 176,338 sawa na 49.1%
SAID SOUD SAID (AFP) amepata 480
KASSIM ALI BAKARI (Jahazi Asilia) amepata 803
HAJI AMBAR KHAMIS (NCCR-Mageuzi) amepata 363
HAJI KHAMIS HAJI (NRA) amepata 525
JUMA ALI KHATIB amepata 497
-------------
wavuti.com inakupeni HEKO WAZANZIBARI. Nakutakieni Zanzibari mpya yenye Matumaini mapya!









RSS Feed