Mbunge Mteule na mmoja wa wanaowania kiti cha Uspika wa Bunge la Jamhuri, Andrew Chenge anasema

"...kiti cha uspika nikiamini kwamba ninao uwezo wa kutibu majeraha makubwa yaliyoumiza Bunge na Taifa, wananchi na chama changu (CCM) kwa sababu tu ya kuwa kiongozi aliye tayari kujitafutia na kujitwalia umaarufu au ushujaa wake binafsi kwa njia ya kuwahujumu, kuwaumiza na kuwachafua wengine kwa kutengeneza tuhuma na kashifa za kila namna. Tiba ya uongozi wa aina hii ni kuchagua kiongozi bora wa bunge...."

Nukuu hii imetoka kwenye blogu ya Beda Msimbe "Lukwangule Ent"

Kwa taarifa zaidi, subiri chapisho la magazeti hapo kesho "...ya kuambiwa, changanya na yako"!
 


Comments

mc
07/11/2010 08:28

Watanzania msidanganyike na huyo chenga.
huyo anatafuta njia tena ya kuongeza jeraha tena ktk nchi

Reply
07/11/2010 08:32

HUYU CHENGE HASITURUDISHE NYUMA MAANA TAYARI TRAIN IPO KWENYE MWENDO. SASA NI MAKOVU GANI ANAYASEMA MAANA BUNGE LILILOPITA CHINI YA SITTA NI LA KIWANGO. EBU KAMA ANATAKA KUTURUDISHA NYUMA KUWACOVER WEZI WA VIJISETI NA AACHE MKAKATI HUO.
KUJUA KANUNI NA TARATIBU ZA UENDESHAJI BUNGE SI KIGEZO CHA MTU ALIYEKWISHA KUCHAFUKA KIMAADILI KUPEWA NAFASI HII NYETI. KWA MAANA NYINGINE CHENGE ANAYOAGENDA YA SIRI YA MAFISADI KUZUIA MIJADARA YENYE MASILAHI KWA TAIFA. HAPANA HUYU JAMAA HATA JINA LAKE LISIFIKIRIWE NA KESI ZAKE ZA VIJISETI ( UNUNUZI WA RADA) NA AJARI ZAKE ALIZOUA WATU ZILETWA WATU WAONE HUYU NI MTU GANI.
HATUWEZI KWENDA POPOTE KAMA SISI WATANZANIA WAZALENDO TUNAONA TUPO KWENYE NJIA SAHIHI KWA UONGOZI MZURI BUNGENI ETI LEO KUNA MTU ANATUAMBIA KULIKUWEPO MAKOVU , JE NI YAPI HAYO. N KAMA KULIKUWEPO MAKOVU BUNGENI NA MTU ALIONA KAONEWA KWA NINI HAKUENDA MAAKAMANI. HII SERA YAKE HAIKUBALIKI KABISA NA HAITAKIWI MAANA NI SERA MFIRISI KWA WANACHI WALIO MASIKINI. SERA YA KWENDA KUENDESHA BUNGE KWA KULINDA MASLAHI YA MAFISADI.

Reply
Ndekarisho
07/11/2010 09:28

Ryaro umesahau SERA kuu ya JK ni kulinda ufusadi? Kama nasema uongo suburi kamailivyo kawaida ya kushinda at any cost. Atampitisha Chenge at any cost ili aendelee kulinda Bunge siunajua tena ulinzi wa usiku Chenge alipata mia kwa mia. Poor Sitta asiye jua kulinda usiku, Mwenzake anataka kumzidi speed ili aongeze ulinzi.

Reply
TW
07/11/2010 16:59

Jamani, ukweli ni kwamba Lowasa & Co. walipanga kumwadhibu Sitta kwa kumvua uanachama wa CCM eti amedhalilisha viongizi wa CCM (2009), Asante kwa Mzee Mwinyi alietumia busara na hekima zake kuzima hayo mapinduzi.
Sasa wakati muafaka umefika na EL kamtuma AC kuchukua Uspika, na AC alivyomjinga anatoboa siri hadharani.
Hiki ndio chama kiliaminiwa na wengi kituongoze tuendapo........... subirini tu bunge lijalo litakuwa linathamini ufisadi kuliko!

Reply
Mnoko Makini
07/11/2010 21:40

Hayo majeraha anayoyasema chenge sijui anaongelea nini.
Walopata majeraha ni:-
1.Wakina mama wajawazito masikini wa vijijini waliokosa hata gloves wakati wa kujifungu huku dola milioni 40 zikitumika kununua rada ya mtumba.

2.Watoto wa kitanzania wasio na vitabu mashuleni,wakiwa wanakaa chini kwa ukosefu wa madawati huku yeye Chenge na Serekali ya awamu ya tatu wakiingia mikataba mibovu ya madini na kifanya nchi kubaki na umaskini uliokithiri.

3.Watanzania wa vijijini ambao mpaka leo wanavaa t-shirt za UCHAGUZI 2000 za CHAGUA MKAPA,CHAGUA CCM-Sio kwa kupenda bali kwa hali ngumu sana ya maisha.

Reply
07/11/2010 23:36

CHENGE UMEKULA SANA HELA YA WATZ ACHIA NA WENGINE ACHA UROHO WA MADARAKA

Reply
Chib
08/11/2010 00:19

Mimi kwa mtazamo wangu usio na ukomavu wa kisiasa naona ni kama kuziba pengo kwa kung'oa jino mahali pengine na kulipachika kwenye pengo la awali, ilhali unabaki na pengo jipya na maumivu juu ikiwa ni pamoja na jino lisilo imara lilipachikwa!!!.

Reply
08/11/2010 02:24

Mmmm!!!! akichaguliwa kuwa spika ni sawa na kulinda maslahi ya MAFISADI, nchi yetu itaendelea kutawaliwa na MAFISADI sijui mpaka lini, Sitta alikuwa kiongozi muadilifu na alikuwa hatetei UFISADI wao ndio maana walikuwa wanampiga vita MAFISADI WOTE BUNGENI. Mungu asaidie huyo fisadi asichaguliwe kuwa SPIKA

Reply
Dr.Mallaba
08/11/2010 03:44

hivi huyu jamaa hana hata aibu?kweli nimeamini mafisadi hawana haya ndio maana wako radhi hata kuua mtu yeyote.

Reply

Reply
08/11/2010 05:45

Kazi ipo!

Reply
Ndekarisho
08/11/2010 08:43

Jamani Chama Chetu cha Mafsadi Kazi ni moja kila anaye mnyooshea fisadi kidole si mwenzetu anatudhalilisha. Kwasababu Mafisadi lazima tulindane 'at any cost'.Tuwajali wananchi watatusaidia nini? Kama hawawezi kujijali nakujitetea wanamsuburi nani awatetee? Obama au? Kazi ipo kweli kweli.

Reply
Suzy
08/11/2010 23:13

Mimi namsifu sana huyu vijicent kwa kuwa muwazi kilichomsukuma hadi akaamua kugombania uspika. Maana asingesema kama kawaida yetu wtz tungejuaje nia yake!!!??? Maana angeweza kuvaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu kama walivyo viongozi wetu wengi rais wetu akiwa namba one!!!

So sasa kama kawaida vikao vya chama vinavyodhaminiwa na mafisadi vitampitisha chenge halafu bunge litakuwa sio bunge tena bali ni sehemu ya lulinda maslahi ya hao MAFISADI....

Mungu tusaidie!!

Reply
joseph mwandi
08/11/2010 23:29

wewe chenge hivi hujitazami au pamoja na usomi wako hujui kusoma nyakati?wewe tunajua ni fisadi wala haihitaji sita aje atudanganye tumeona wenyewe wewe ni fisadi tena papa unataka kushika kiti kulinda maslahi ya wachache akina lowasa mmechemka na huyo blaza wako

Reply



Leave a Reply