Waziri Vuai alisema Serikali inasikitishwa na tukio hilo na kwamba iliacha "hali tete" kuendelea bila kuingilia kati kwa kuwa katika "Nadharia na Taaluma ya Migogoro", kabla ya mgogoro wowote ule haujatatuka, ni lazima uachwe hadi ufike mahali ambapo wahusika wakuu wataamini kuwa lipo tatizo linalohitaji kutatuliwa, kwa kuwa, mgogoro ukianzakutatuliwa mapema, basi ile furaa ya kusikilizana huwa haipo kwani upande mmoja huwa hauoni wala kukubali kuwa lipo tatizo.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Siasa cha Wananchi, CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akitoa tamko kuhusu kilichotokea Arusha amesema kuwa, Polisi wangetumia taarifa za kiitelijensia kuzuia vurugu ambazo 'huenda zingetokea kwenye maandamano hayo' na siyo kutumia nguvu kuzuia maandamano yenyewe.
Watuhumiwa 31 wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, sita kati yao wamesomewa mashtaka yao wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Mount Meru. Shitaka kuu linalowakabili watuhumiwa hao ni "kufanya mkusanyiko bila kibali na kusababisha uvunjifu wa amani". Baada ya kusomewa mashitaka, Hakimu aliruhusu Watuhumiwa kupewa dhamana na Watuhumiwa wote 31 walitimiza masharti ya udhamini na kutoka korokoroni.
Jingine katika taarifa hii ni kutajwa kwa Wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd., ambao ni Dowans Holding S.A, Costa Rica na Portek Systems and Equipment (PTE) Ltd. Barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (BRELLA) inawataja wakurugenzi kuwa ni Andrew James Tice - Canada, Guy Picard - Canada, Gopalakrishnan Balachandaran - India, Stanley Munai - Kenya, Hon Sung Woo - Singapore na Sulaiman Al Adawi - Oman.
1. Bofya kifute cha 'play' usikilize taarifa ya habari ambapo pia Serikali imezungumzia suala la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala Tawi la Tanzania.
2. Sehemu ya taarifa ya habari ya Dira ya BBC kuhusu hali ilivyo mkoani Arusha, siku moja baada ya rabsha.





RSS Feed