Lazima kuna kitu katika picha kubwa ya jumla katika matukio haya yote (the big picture). Je, tunaiona?
Matukio haya yamenisababisha juzi nikumbuke Darwin's Theories!
|
|
Ninapozitizama picha hizi, watu mamia kadhaa, wakijumuishwa wote wa Loliondo, Rombo, Mbeya na sasa Tabora wanafika maelfu kama si makumi elfu. Najiuliza, hii ni jamii ya watu waliojawa na matumaini au waliokata tamaa? (Hopeful vs Hopeless) ama yote mawili? Lazima kuna kitu katika picha kubwa ya jumla katika matukio haya yote (the big picture). Je, tunaiona? Matukio haya yamenisababisha juzi nikumbuke Darwin's Theories! Picha : KeroNyingi blog CommentsEvan 30/03/2011 06:45
huu ujasiri wa ajabu.Nahisi chanzo cha imani kipo Tanzania maana tuko tayari kuamini chochote na kukipa nguvu..Watu tunaamini kila kitu na kwa moyo mkunjufu.Matatizo yamekuwa mengi mpaka yameathiri uwezo wetu wa kupembua mambo.Neno 'nasikia' ndo linaanza mara linapewa mwili na kuuishwa ghafla linakuwa ''nimeona kwa macho yangu' niajeniaje 30/03/2011 13:20
Kwani kipimo cha imani ni kipi? Pengine wewe ndio hujaamni, Kumbuka imani ya ndio itakuponya...! galauka 30/03/2011 22:26
SHETANI YUPO KAZINI. Jogholokeka 30/03/2011 23:44
Woote hapo juu hamjaumwa bado, hata muda wa kuchallenge msingekuwa nao na nyinyi sasa hivi mngekuwa kwenye foleni. tabora 31/03/2011 02:07
Kuna neno kwenye bible na msaafu kuwa kabla ya siku ya mwisho kuna miujiza ya kina masihi dajali itakuwa mingi sana mimi naamini siku zimekaribia z mwisho wa dunia, nawashauri watu kabla ya kunywa wafikiri kwanza, Neema 31/03/2011 07:28
Jamani adha ya ugonjwa au shida yake anajua mwenye maradhi! Ni rahisi sana ku coment negatively kama ile kitu haikugusi sehemu! Kumbuka ni shida ngapi umekutana nazo na ulihangaika jinsi ya kusolve mpaka kieleweke! Mie kwangu ni lazima utafute uponyaji ili kuweza kujinusuru! We panadol kutibu maumivu si umewasikiliza wanasayansi na ukaamini na unaitumia mara zote? Sasa iweje dawa ya asili tunaibeza sio fresh wala nini, ni kweli janga la maradhi ni kubwa mungu tu aingilie kati Mtango 03/04/2011 23:32
Watu wanywe ili mradi sio sumu..! Magonjwa yanasumbua, ukienda kwenye mahospitali ya wilaya na mikoa misururu na rushwa ndo zinaendelea. Hata hivyo dawa ya magonjwa kama ukimwi kisukari presha bado hazijapatikana kwenye mahospitali. So mi sioni problem watu kujaribu kujitibu...! Labda changamoto ni pale inapohusishwa na imani ya dini, kwa hiyo usipopona unaambiwa imani yako ni kiduchu/haba hivyo inazidi kumnyong'onyesha mgonjwa na inafikia anakata tamaa kabisa.Anajisikia kama mungu ameshamkataa. Dawa kama panadol, asprini, valium, piriton hata kama ni mchawi/mpagani/kafiri/mzinzi totoro/firauni etc ukiimeza lazma itafanya kazi..! Tena jaribu valium uone..! Mtizamo..! Leave a Reply |