Picture
Bi. Fatma na bintiye Ashinuri
Fatma Said Sengo (41) mkazi wa Kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro, (ushungi mwekundu pichani) ametangaza kutibu magonjwa sugu ambapo, binti yake wa miaka minne, kwa jina Ashinuri (ushungi wa pinki) hugawa "dawa" kwa wagonjwa na kisha kupokea fedha shilingi 200/- tu.


Pichani ni Fatma akiwaonesha dawa viongozi waliomtembelea nyumbani kwake ili kupata maelezo ya kina kuhusu tiba yake hiyo.

Anayeonekana pembeni yake katika picha ya kwanza ni mwandishi wa habari aliyetembelea eneo hilo leo Machi 31, akiwa na viongozi hao wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu. Na picha inayofuatia Mkuu wa Wilaya akitoa msimamo wa Serikali wa kumtaka mtu huyo ajisajili na dawa yake ipimwe ionekane uzuri na ubaya wake.

Picha zinazofuatia zinawaonesha watu wakitoa fedha na kupokea 'bilauri' na kunywa kwa ajili ya 'tiba'.

credits : Juma Mtanda blog na John Nditi via Lukwangule blog


 


Comments

paesulta
31/03/2011 11:53

naona ule msemo wa ''fool me once shane on me,fool me twice.....''hau-apply kwa wa-Tanzania.inabidi nibaki kucheka tu.lakini huyu gia yake babb kubwa ,kumtumia mtoto......!and from what i get,msimamo wa serikali ni just wait sit and see,let nature run its cause...hakuna haja ya kudhibiti this madness!

Reply
Joeli mbwaga
31/03/2011 13:43

were were yaani hadi raha picha ndo kwanza limeanza na bado watajitokeza wengi!

Reply
mpekenyuzi
31/03/2011 21:19

sasa nimeamini kweli sisi wananchi ndio tulikuwa tunawaua wenzetu wenye ulemavu na si majirani zetu kama tunavyowasingizia, hapa inaonyesha ni jinsi gani akili zetu finyu na zinazidi kudumaa kila kukicha. yaani kweli hata watu kustuka hawawezi kabisa

Reply
Mughosya
31/03/2011 21:34

WACHA WAENDELEE KUTOKEA- KILA MKOA SASA- KESHO TUTASIKIA YESU KAONEKANA SINGIDA.

Reply
sudi
31/03/2011 22:15

shetani at work

Reply
Mtanzania
31/03/2011 23:21

USHENZI MTUPU NA SERIKALI INAELEKEA IKO LIKIZO KAMA KAWAIDA! NDO MAANA HATUSONGI MBELE KWANI TUMESHINDA KUTOFAUTISHA KIPI SAHIHI NA KIPI SIYO? HIVI HAPA INAHITAJI MSAADA TOKA NJE YA NCHI KUELEMISHA JAMII NA SERIKALI? KAZI YA SERIKALI NI IPI?

KAZI IPO ILA TUFIKE MAHALI TUBADILIKE LA SIVYO TUTABAKI KUWAAMBIA WAKENYA WASIJENGE UWANJA WA NDEGE KARIBU NA KILIMANJARO JAPO NI NCHINI KWAO! AMA KWELI NI SHUGHULI! RAISI, MAWAZIRI, WABUNGE NA VIONGOZI WENGINE WAKO WAPI? NCHI INAWASHINDA? SEMENI AU KWA VILE MMESHACHUKUA MAFUNGU NA MWAENDELEA?

SAMAHANINI MIMI INANIKERA PAMOJA NA UPEO WANGU MDOGO. TUMEWAPA MADARAKA MTUTUMIKIE NA KUHAKIKISHA NCHI INAKUWA NA MWELEKEO MZURI SI KAMA MFANYAVYO! HIVI HAMUONI AIBU AU NDO MKISHAKAA KWENYE HIYO MIBENZI NA MISHANGINGI MWAJISAHAU?

Reply
Mnyampaa
01/04/2011 01:32

Amakweli Taifa letu linaumwa tujipe pole kila mmoja.

Reply
paesulta
01/04/2011 02:10

natamani atokee mtu agawe kikombe,lakini masharti yake yawe kikombe kinaendana na kushika jembe au kupiga lumbesa.at least we'll gain on something,na kwa kuwa inaonekana tunawaamini sana watoa vikombe...

Reply
Mtanzania
01/04/2011 05:26

Jamani huu ushenzi utaisha lini? ama kweli Tanzania nchi ya mwisho kwa umasikini duniani kutokana na ujinga.

Reply
Mpitanjia
01/04/2011 05:28

Tanzania ina raisi na mawaziri? viongozi wote wapo na wanajua majukumu yao? Kinachoendelea wanakiona ni sawa? tumewapa dhamana ya nini?

Reply
PMN
01/04/2011 09:25

Hah hah hah, ama kweli nchi haina uongozi. Yaani hivi kweli wananchi wanapoteza muda mwingi na fedha kusafiri eti wanafuata dawa???? Huo muujiza ndio utokee Loliondo, mwezi mmoja ufike Rombo, Mbeya, huko Tabora na sasa siku uko Morogoro??? Hatuwezi hata kuwaza???

Reply
01/04/2011 22:18

Zipo dawa za kitaalamu na zipo dawa za kienyeji, na toka historia dawa hizi zipo, tatizo lilikuwa hawa wa dawa za kienyeji walikuwa hawatangazwi, kwasababu dawa hizi hazina vipimo, hazina hati miliki hazina TBS..NK, Lakini watu walikuwa wakitumia, kwa dhahiri na kwa siri...leo hii iweje ni ajabu!
Sijui, labda kwa vile imetangazwa, cha msingi ni kutathimini `imani' yako na `ugonjwa' wako, kama kienyeji inalipa usijivunge kama `kitaalamu ' ndio bora basi jimwage...! Kwani mwisho wa siku unachotaka ni nini...ni tiba, kwasababu zote ni dawa!

Reply
Igula man
01/04/2011 22:59

E waa EMU THREE unaonesha una upeo kwa mawazo yako unajua unaweza ukamcheka mwenzako kwamba hajui ,mjinga kumbe wewe ndiyo hujui na mjinga dawa za miti shamba in changamoto kwetu wa Tz tutaendelea kutumia chemicals hata lini? ndio maana cancer kibao wewe amabae hutaki endelea na ujinga wako wa kizungu. jifunze China wanatumia dawa gani kama siyo miti shamba!

Reply
06/04/2011 05:18

Yap. emu three! daima mjinga hawezi kujijua wala kujisema kuwa yeye ni mjinga. kaenda zake kashule ka dregee moja tu basi anajiona mzungu mpaka anasahau hata vilivyo wakuza babu na bibi zake. hajui kuwa hata hili swala la usajiri wa tiba au dawa ni kwaajiri ya kulinda soko la vitu vya kizungu ili technolojia ya kizungu iendelee kutawala? acha watu wajimwage kiasiri bwana kama inatibu.

Reply



Leave a Reply