Ni kisa ambacho kila anayejali utu wa binadamu anapaswa kukisikia ili kupata changamoto ya namna atakavyotumia juhudi binafsi kuzuia ukatili huu ambao unaweza kumpata mwanaye, mdogo wake, mkewe, mama yake, bibi yake, shangazi yake, mkwewe, shemeji yake, wifi yake, au ndugu yaye yeyote wa kike, zaidi sana, matukio haya yamekuwa yakiwahusisha hata vijana wadogo wa kiume. Jamii hujengwa na sisi.
Kisa kimemtokea Binti wa miaka 16 alipofukuzwa toka nyumbani kwa Mama Mwenyenyumba ambaye alikuwa amemwajiri kwa ajili ya kumfanyia shughuli za ndani.
Binti anaeleza kuwa chanzo cha kufukuzwa siku hiyo pamoja na kuwa alishafanyiwa ukatili mara kwa mara, ilikuwa ni kosa la kutumia mafuta ya marashi "lotion" ya Mwajiri wake.
Binti anatokea Kigoma. Anaelezea historia yake ya kuwa kitinda mimba na mtoto pekee wa kike kati ya 11 waliozaliwa na Mama mmoja na kwa Baba (ambaye alikuwa na wake wawili).
Binti huyu alikwenda Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kumtafuta Dada yake baada ya kushindwa kuendelea na masomo alipokuwa kidato cha Pili kwa kile kilichoelezwa kuwa ni "kurukwa na akili katika mazingara" na hivyo kushindwa kumalizia masomo ya Sekondari. Kwa bahati mbaya, binti hakufanikiwa kumpata dada yake na hivyo akaishia kutafuta pa kufanya kazi za ndani na ndipo alipojikuta ameajiriwa huko alikofukuzwa.
Dk. Isaac Maro katika kipindi cha Njia Panda kinachorushwa na Clouds FM radio siku za Jumapili mchaa saa 8 alasiri hadi 10 jioni , alikuwa na binti huyu ambapo alimhoji na kupata maelezo ya jinsi alivyoshambuliwa kikatili katika tendo la ubakaji. Kwa bahati mbaya, kutokana na histori ya yaliyomtokea maishani, binti huyu anashindwa kueleza kisa na mkasa lakini kwa usaidizi wa Dk. Isaac, anaweza kuelelezea kilichotokea siku ya tukio. Ni kisa cha kusikitisha na kukerehesha sana. Alinitoa machozi aliposema kwa huruma, "walinibaka mdomoni"....! Bofya kifute cha pleya iliyopachikwa hapo chini usikilize kipindi hiki ambacho hakijahaririwa.
Studioni walikuwepo wataalamu wa Afya, Saikolojia na Sheria waliozungumzia madhara ya tendo hili na adhabu ya sheria iliyopo na inayowakabili wahusika kuhusiana na tendo hilo.


RSS Feed