bhoke
Hakuna ubishi kuwa jamii yetu ya kitanzania inazidi kuwa ya kipuuzi kadri siku zinavyokwenda na kundi linaloonyesha kuzidiwa nguvu na ujinga ni kundi la vijana huku ujinga wao wakiubatiza jina la “mambo ya kisasa” lakini ukitazama kiundani unabaini kuwa ni ulimbukeni wa kupenda tamaduni za kimagharibi na pengine uzuzu wao na mdumao wa ubongo ikiwa ni matokeo ya kutopenda kufikiri.

  Nimelazimika kutumia maneno makali sana leo kutokana na jambo ninalotaka kulizungumzia hii leo kuwa ni zito sana na hili si lingine bali ni kitendo cha mtanzania mwenzetu mwanadada Bhoke kufanya ngono na mshiriki mwenzake Ernest huko nchini Afrika kusini katika jumba la Big Brother Africa, naam! ni kitendo kilichovuta hisia za watanzania wengi walio ndani ya nchi na walio nje ya nchi, nataka kumshauri Bhoke kama kijana mwenzangu tena hadharani ukizingatia kitendo chake hiko kimeonekana hadharani na zaidi ya yote nataka kumwambia ukweli pasipo kupindisha neno kwa kiwango ambacho na uhakika marafiki zake hawawezi kumwambia kwa kumwonea aibu, mimi nitamwambia leo pasipo kumung’unya maneno.

    Baada ya kurejea nyumbani Bhoke amenukuliwa akisema kuwa hakutumwa na watanzania Afrika kusini bali alienda mwenyewe , ingawaje mara ya kwanza nilivyosikia upuuzi huu nilidhani ni maswala ya kuuza gazeti tu lakini kutokana na kusubiri kuona iwapo Bhoke mwenyewe atakanusha na hakufanya hivyo basi hakuna ubishi kuwa Bhoke amesema upuuzi huu ambao bilashaka badala ya kumjenga unazidi kumharibia yeye na mabinti wengine lakini mbaya zaidi unazidi kuwachafua vijana wa taifa hili, naam! Bhoke amefanya upuuzi na sasa ameongea ujinga.

    Kwanza kabisa Bhoke hana sababu ya msingi ya kujitetea kutokana na kitendo cha aibu alichokifanya, ikumbukwe kuwa alipokuwa Afrika kusini Bhoke alitambulika kuwa anatoka Tanzania na tangu akipanda ndege kuelekea huko hakuna ubishi kuwa alikwenda kuwakilisha nchi yetu kwenye tasnia ya burudani kama wafanyavyo wasanii na wanamichezo wengine hivyo kauli yake kuwa hakutumwa na watanzania haina mashiko na zaidi ni ya kitoto kuliko uhalisia, labda nimwulize Bhoke swali moja tu rahisi, je kwanini Richard aliposhinda alipokelewa kama shujaa? Au kwanini Mwisho naye alipongezwa na watanzania? Au basi iwapo yeye Bhoke angeshinda je angekataa kupokelewa na kupongezwa na watanzania? Kwasababu hawakumtuma? Natoa changamoto kwa Bhoke ajifunze kuongea mambo yenye mantiki sio kutujia na vijisababu vya kitoto ambavyo havijai hata kwenye kiganja.

  Hivi Bhoke anataka kutuambia kuwa yeye yuko sahihi? Na sisi tunaolaani kitendo chake ni washamba? Au tuna mambo ya kizamani? Au basi nani kamwambia Bhoke usasa ni kujidhalilisha na kutuvua nguo watanzania kama alivyotufanya? Nani kamwambia Bhoke kuwa kufanya ngono hadharani ni jambo linalokubalika kwa mila zetu? Mbona Bhoke anataka kutuchezea akili kwa kutetea ujinga? Tena mchana kweupe! Bhoke anapaswa kutambua kuwa watanzania sio watumwa wa mila za kishenzi za kufanya ngono hadharani za watu wa magharibi?

    Uzito wa jambo alilolifanya Bhoke hauwezi kuelezewa kwa misamiati wala methali , hata tujitahidi kuupaka mafuta kwa kiasi gani bado utabaki ni utumbo wa aina yake kwa mwaka huu wa 2011 na pia itabaki katika kumbukumbu za watanzania kama aibu kubwa huu ndiyo ukweli ambao naona Bhoke anataka kuupindisha kwa hoja nyepesi mno tena zilizopwaya sana za “sikutumwa na watanzania”. Chukulia mfano video ya Bhoke ya huko Afrika kusini niliulizwa na rafiki yangu aishiye nchini Finland kuwa nimeshaiona? Mimi kwa kuona aibu nikaficha na kusema hapana sijaiona, rafiki yangu hakuchukua muda akanitumia, hiki ndicho alichotufanya Bhoke duniani kote sasa wanamtambua kwa aibu yake hiyo!

  Watanzania ni watu tuliokuzwa katika utu ikiwa ni pamoja na kuvumiliana na kusameheana ila ni kwa wale waliotayari kukiri makosa yao , kujutia na kuomba msamaha sasa tulitegemea Bhoke ajutie kosa lake na kuomba msamaha kwa watanzania lakini sasa yeye anataka kutupanda kichwani huku akijua wazi kuwa ametuaibisha, hili halikubaliki hata kidogo ni lazima tumkemee vikali tena kwa maneno makali pasipo huruma, baada ya kujidhalilisha yeye na kutuaibisha watanzania sasa Bhoke anataka kutudhihaki? Hili halikubaliki kabisa!

    Ikumbukwe kuwa Bhoke sio binti tu wa kitanzania bali ni msichana wa kitanzania aliyejijengea heshima kubwa kutokana na harakati zake kuhusu vijana kupitia kipindi cha 5 connect katika kituo cha EATV si hivyo tu kuna baadhi ya mabinti wadogo walikuwa wakimwona Bhoke akiendesha kipindi hiko walijisemeza moyoni kuwa na wao siku moja wangetamani kuwa kama Bhoke naam! Bhoke alikuwa msichana wa kupigiwa mfano miongoni mwa wasichana wenzake na vijana wa kitanzania kwa ujumla.  

    Bhoke nayemjua mimi sio Bhoke huyu anayejibu upuuzi wa kitoto wa “sikutumwa na watanzania” mimi namfahamu Bhoke jasiri ambaye ni aina ya mabinti ambao hata ukienda naye hotelini hataki ofa za bure bali wewe utalipa nusu nayeye atalipa nusu, huyu ndiye Bhoke nayemfahamu mimi ambaye kila jumatano nilikuwa naacha shughuli zangu kumwangalia naam! ni Bhoke niliyetamani siku moja nimhoji au nifanye naye kipindi. Lakini sasa Bhoke anazidi kujibomoa kwenye mioyo ya watanzania, Bhoke anajaribu kutikisa kiberiti afahamu hasira za watanzania, Bhoke anafanya mzaha na mila zetu na hisia zetu.

   Namtaka Bhoke afikirie tena juu ya kosa lake na matamshi yake nayoyaita ni ya kipuuzi kabisa“sikutumwa na watanzania” natoa changamoto kwa Bhoke ajaribu kuomba ushauri kwa viongozi wake wa dini juu ya kitendo chake na kisha ajipange kwa hoja zenye mashiko na zitakazopooza hasira za watanzania , aachane na porojo za kitoto kama ambazo ameanza kuzitetea badala yake namtaka Bhoke akumbuke yeye ni nani? thamani yake ni nini? na amefanya nini? naam! natoa wito kwa dada yangu Bhoke alitazame kosa lake kwa jicho la tatu na akili ya kiutu uzima……….Tafakari!

Alluta continua!

Nova Kambota Mwanaharakati,
june 23, 2011,Tanzania East Africa
0717 709618 au +255717 709618
novakambota@gmail.com
www.novakambota.com

 


Comments

Paesulta
25/06/2011 04:41

Mi nadhani upuuzi wote ulianzia pale tulipofikiri kuwa na "mwakilishi wa Tanzania" kwenye upuuzi huu wa Big Brother.Labda hatujui dhana nzima ya mchezo huu.Yale aliyofanya Bhoke ndo hasa wanayotaka waandalizi wa mchezo huu,kuprovoke ili kupata watazamaji wengi zaidi.
Kwa upande wangu mimi kama Mtanzania sijawahi kutuma mwakilishi kwenye upuuzi unaoitwa Big Brother, na wala sitarajii binti yangu kuwaangalia hawa "wawakilishi" kama real model.
Mi nadhani alisema sahihi kuwa hakutumwa na Tanzania.Mtu anakwenda kule kwa utashi wake binafsi.Kama tumefikia mahali tunataka watoto wetu wawe na ma-real model kutoka Big Brother basi vichwa vyetu havina akili.Inabidi tuchague nini tunataka wanetu waangalie na nini wasiangalie,na kwa maoni yangu Big Brother sio sehemu ambayo utataka mwanao ajifananishe kuwa kesho anataka kuwa kama hao washiriki wake....

Reply
Anonymous
26/06/2011 23:30

Kwa maoni yangu naweza kusema ki maadili sio Bhoke tu, Hata Richard na upande mwengine Mwisho hawakuwa na maadili yeyote, sio richard aliyekuwa anatembea na yule demu wa Angola na huku alikuwa ana mke nyumbani? Jee kaka Nova uliliongelea vipi hili? kama ungeweza kulikemea hili na wengine wangekemea then washiriki wa TZ wanaofuata wangelizingatia but after Richard kushinda uovu wote alioufanya haukuonekana na tulimpokea kishujaa. Upande mwengine hiyo BB Brother kwa asilimia fulani naweza kusema ndio inayochichea kwanini waonyeshe uwovu kama huo? maan bb brother its for Africans na maadili ya humo ndani are not Africans at all. Sasa kama game yenyewe inaruhusu je participants wafamyeje? Hapo hapo Bhoke apart from being the game alichofanya sio proper kabisaaaa its about time Tanzania to say no to Big Brother as a whole, haswa ukizingatia watoto wetu na vijana wetu wanaangalia hiyo program kwa ushabiki mkubwa.

Reply



Leave a Reply