Picture
L-R: Prof. Issa Shivji, Dk. Kitila Mkumbo na Jenerali Ulimwengu (picha ya maktaba)
...wakati kila kitu kimeondoka na kila kinga imemtoka mwanadamu, kinga ya mwisho inayosalia kabla hajavua nguo na kuingia mtaani akiwa mtupu, ni soni au haya. (Naomba kwa mara nyingine tusichanganye haya na aibu. Nimesikia na kuwasoma watu wakichanganya dhana hizi mbili. Napenda kurudia kwamba aibu ni fedheha inayotokana na tendo linalomvunjia mtu staha, kama kujikojolea hadharani au kumbaka mbuzi. Haya ni sifa ya kila mwana aliyelelewa vyema, mpole na mwenye heshima, staha na adabu).

Sasa inaelekea tumebadhiri haya zetu kiasi kwamba tofauti yetu na kila kitoto kilichopitishwapitishwa maishani ‘fasta-fasta; bila kutoka jasho wala kutumia ubongo wake, ni kidogo sana. Hii inatokana na kuiga mambo ya hovyo kutoka kwa watu wa hovyo na utamaduni wao wa hovyo wakati tungeweza kuiga mambo ya maana kutoka kwa watu wa maana na utamaduni wao wa maana....

Tumbo liliovimbiwa linamdhuru binadamu kwa njia nyigi, mojawapo ikiwa ni kumpunguzia uwezo wa kufikiri. Ye yote aliyewahi kuvimbiwa (niliwahi kuvimbia nikiwa mtoto, kwa uroho) anaijua hali hiyo. Gesi zinazovurugana tumboni na kuzaa harufu chafu za mbweu, si tu zinakufanya usijisikie raha, ujihisi mchovu, lakini pia zinaondoa uwezo wa kufikiri....

Sijaelewa ni nini kinawafaya watu ambao wameapa kwamba dhamira yao ni kuwatumikia wananchi wazione ofisi zao kama mahali pa starehe. Kinachonishangaza zaidi ni kwamba inaelekea hakuna mkubwa ndani ya Serikali mwenye uwezo wa kuwaambia wenzake: Basi, inatosha, kifayyah! Rwanda alifanya Rais Kagame, lakini Kenya hawakumhitaji rais; alifanya Uhuru Kenyatta. Sisi hatunao watu kama hawa?

Soma makala nzima yenye kuunganisha vionjo hivyo kupitia raiamwema.co.tz (bofya hapa)
 


Comments




Leave a Reply