Mtanzania Mrisho Ngassa juzi alishuka dimbani kulisakata kambumbu kati ya timu anakofaniwa majaribio,  Seattle Sounders ya Marekani pale ilipocheza mchezo wa kirafiki na timu ya Manchester United ya Uingereza.

Ambao hawakupata fursa ya kumwona kijana akidundaduna uwanjani, bofya picha hapo kisha itakufungulia ukurasa ambao utapata fursa ya kupakua video yenye ngwe ya pili ya mpambano huo.

Video hiyo itaondoka baada ya siku 13 kuanzia leo! Hivyo utakapoikosa usihamaki "mbona haipo?".
Picture
 


Comments

22/07/2011 01:23

Kwangu hiyo video haikubali, lakini twamtakia jamaa huyo mafanikio mema

Reply
22/07/2011 14:05

Nime edit video na kuacha dakika 15 za mwisho alivyoingia Ngassa. Unaweza kuingalia video YouTube: http://www.youtube.com/watch?v=uZTQM8LO96o. Kama unataka kuona goli alilokosa forward video mpaka dakika ya 11. Thanks Subi for providing the video link.

Reply
22/07/2011 22:45

@emu-three, pole kwa kushindwa kuipakua video, ipo hapo tu, wameipakua wengi, ila inahitaji intaneti yenye nguvu ndipo ifunguke.

@Proches, asante kushukuru. Nilimwona 'dogo' alivyokosa goli lakini akamwacha Rio akichechemea na kuugulia maumivu, Ngassa 'hatari', namtakia mafanikio mema.

Reply



Leave a Reply