Kipindi cha Njia Panda kilichorushwa hewani siku ya Jumapili tarehe 31 Julai 2011.

Ni kipindi ambacho kimefanya mahojiano baina ya mwendeshaji wa kipindi Dk. Isaac Maro na Mama Mdogo wa Binti ambaye alibakwa na baba yake mzazi na kupata ujauzito. Binti alimzaa mtoto, mtoto ambaye naye alibakwa na baba/babu. Ndiyo kusema, Baba alimbaka mwanaye, akampa ujauzito, kilichozaliwa katika ujauzito huo, miaka 10 baadaye, akakibaka. Kambaka mtoto na mjukuu damu yake.

Aliyelivalia njuga suala hili, ametishiwa kuuawa na Baba mbakaji.

Baba aliyebaka ametoroka nyumbani na hivi sasa anatafutwa na Polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.

Mwanasheria naye alikuwepo studioni kutoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na suala hili.

Bofya kifute cha play usikilize, dakika 18 za mwanzoni utasikia kipindi cha spoti na habari za michezo kikifikia ukingoni ndipo kiache nafasi kwa kipindi cha Njia Panda kuanza, hivyo vumilia hadi dakika ya 19.

Kipindi hiki kitaendelea tena wiki hii kwa kuwashirikisha Mama mzazi wa Mtoto, Mjumbe wa mtaa na Polisi. Ukitaka kusikiliza basi usikose kuwa kando ya redio siku ya Jumapili tarehe 7 Agosti 2011 kuanzia sasa nane alasiri hadi kumi jioni. Unaweza kusikiliza redioni au (bofya hapa).
 


Comments

julie
08/08/2011 14:33

tumrudie Mungu jamani ili awalinda watoto wetu.

Reply



Leave a Reply