...katika karne ya 21 wanayokuzwa wakiamini kuwa nchi tayari ina mkongo wa mawasiliano na hadi ifikapo 2010, eh, samahani, nadhani mwaka 20,100, shule zote za Tanzania zitakuwa zimeungwa katika mkongo wa mawasiliano... kwa sasa wavumilie tu kuvunzwa SIPIYU kwa nadharia. Akitoka hapo atakuwa na ujuzi wa kupambana vilivyo katika kutuma maombi ya kazi kwa njia ya barua pepe. Ataweza tu! Ajitahidi.

Na, tusitarajie shule kuungua moto pia ati tu kwa vile wanatumia vibatari, koroboi na mishumaa.

Vile vile madhara ya kupumua moshi wa koroboi kwa saa 2 - 4 mfululizo si mkubwa, tutafanya utafiti, wataalamu wetu wataona kama kuna madhara yoyote, watatushauri, tutajua la kufanya!

Hivi moshi unafika ubongoni? sipati picha ambavyo ubongo ungekuwa unajaa weusi na ukungu wa moshi, hebu tusubiri wataalamu wetu watatufahamisha
Picture
picha credit: KanujaSon/Habari na Matukio blog

Sijui Bill Gates na Steve Jobs au Michael Dell ama Linux hawana mpango wa kutengeneza SIPIYU za mafuta ya taa? ah,  nimesahau, mafuta ya taa yamepanda bei ni ghali pengine kuliko ya petroli/dizeli, ni vile watumiaji wa mafuta ya taa ni wachache kuliko wenye magari Tanzania lakini wenye maamuzi ya nchi ni wengi kuliko raia... I am sorry nime-mix huo mstari wa mwisho wengi ndiyo wachache na wachache ndiyo wengi... hebu pindua hapo utanielewa, nchi yenyewe tunasonga mbele kwa gia ya rivesi, n'shadata mie!
Kwenda mbele kwa mwendo wa "reverse gear" nayo ni hatua jama! Kwanza tunajitahidi sana, ila ninyi hamuoni mazuri tunayofanya, mnalalamika tu! Hatuwezi kuwa na ufumbuzi wa matatizo yote, eenh, HAIWEZEKANI, kwanza matatizo yatakaa yaishe siku moja duniani? Likitoka hili, litakuja hili, na jingine na jingine, hayaishi! Ila sisi tunajitahidi kuyatatua kwa kadiri ya uwezo wetu. Huo ndiyo ukweli, hakuna ukweli mwingine zaidi ya huo. Wengine ni wabishi tuu, kwa kuwa wamezoea kubisha kila kitu. Eh, kwani sisi malaika bwana? Mnafikiri tungekuwa na uwezo wa kutatua matatizo yote tungeacha wananchi wateseke? Sisi tunasema hivi, eenh, kama kuna mtu anaona anao ufumbuzi wa haya matatizo, atuletee maelezo yake, sisi tutayafanyia kazi, sawa? eh eh e eh.
 


Comments

eric
01/08/2011 21:58

zilizopita zilikuwa sifuri zilizopikwa kwa shule za kata this time zaja sifuri za uhaba wa umeme!wataalum wa kutengeneza sifuri serikali ya awamu ya nne si haba!

Reply



Leave a Reply