
Kwenye kipindi alialikwa Langa Kileo ambaye habari yake tuliisoma wiki iliyopita katika vyombo mbalimbali vya habari (unaweza kubofya hapa kuisoma tena) pamoja na mwanamuziki kwa jina la kisanii "Kala Pina".
Katika kipindi hiki, Langa na Kalapina wanazungumzia juu ya matumizi ya dawa za kulevya, ilivyoanza, mwendelezo wa kuzitumia na hatimaye kufikia hatua ya kutaka kuachana na dawa hizo. Wanagusia magumu waliyoyapitia katika kujidahidi kuziacha dawa, mafanikio na mbinu za kuendelea kushinda.
Langa anatoa dondoo za kilichomwezesha kutimiza miezi 4 hadi sasa bila ya kutumia dawa hizo. Vile vile anaelezea malengo na mikakati yake ya mbeleni katika kuwasaidia vijana wanaotaka kuachana na dawa za kulevya.


RSS Feed