MPYA: Taarifa rasmi ya Ikulu na picha za baada ya kikao zinapatikana katika chapisho linalofuatia (bofya hapa).

---

Rais Jakaya Kikwete ameukaribisha ujumbe wa CHADEMA uliotaka kukutana naye ili kuzungumza kuhusu masuala ya muswada uliopitishwa na bunge hivi karibuni unaohusu sheria ya muundo wa tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya utaratibu wa upatikanaji wa katiba mpya ya Tanzania. 
Rais alikutana na viongozi hao saa tisa na nusu alasiri mpaka hadi kumi na mbili jioni na kukabidhiwa kabrasha la maoni ya viongozi hao kabla ya viongozi hao kupiga picha za pamoja na Rais wakiwa ndani na baadaye nje ya jengo la Ikulu na hatimaye kuendelea na majadiliano.

Kikao chao hicho cha majadiliano kilidumu kwa saa tatu na kiliahirishwa saa 12 jioni na kitaendelea kesho asubuhi saa nne, "Ndugu waandishi wa habari tumekutana na Rais na baadhi ya mawaziri na Wasaidizi wake! Kikao kilianza saa 9:30 mchana na kiliahirishwa saa 12 jioni. Kikao kitaendelea kesho asubuhi saa nne. Taarifa kamili ni baada ya kikao," alieleza Mbowe katika ujumbe wake kwa vyombo vya habari.

Mbowe aliongozana na wajumbe wa kamati hiyo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara) Said Arfi na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar) Said Issa Mohamed, Mshauri wa Masuala ya Siasa wa chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Abdallah Safari na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu ambaye alikuwa Katibu wa Kamati hiyo wakati wa mkutano, John Mrema na John Mnyika. 

Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa ambaye ni mjumbe, hakuwapo. 

Zifuatazo ni picha toka Ikulu... (bofya moja moja kuzikuza kwa mwonekano mzuri zaidi)
 


Comments

27/11/2011 23:29

Kila wakati tunawaambia watu kuwa CHADEMA ni chama makini na hawakurupuki, sasa je wadau mnaona wanavyopoleka mambo kistaarabu??? Wanaosema Chadema wanaleta fujo wao ndio wanaoleta fujo hizo! Mawazo makini na ya msingi na kupelekwa kwa kutuata taratibu!! Jambo hili tunawapongeza sana viongozi wa Chadema kwa Busara zao!
Tutafika tu tena kwa AMANI!!!
MUNGU ibariki Tanzania, MUNGU ibariki katiba mpya!!!

Reply
Salehe Mchome
23/01/2012 03:12

Mheshimiwa Kikwete ninakupongeza kwa taratibu zako nzuri za kupenda kukutana na vyama vya siasa,huu ndiyo uongozi bora.Big up Mr.President na ninakutakia mafanikio mema ya kupenda kupata ushauri wa mambo mahimu yanayoikabili nchi.Viongozi wa chadema mimi ninawakubali sana nyie ndiyo wapambanaji nawazalendo wa kweli mnaotaka haki usawa katika nchi.Ninawafananisha na Hayati Baba wa Taifa mwalimu J.K Nyarere big up Guys.

Reply



Leave a Reply