Picture
Baada ya taarifa ya juzi ya Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo, kukosa huduma ya X-Ray, sasa inaripotiwa kuwa:

Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) ambayo imeadhimisha miaka 40 toka kuanzishwa kwake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uharibufu wa mara kwa mara wa mashine za CT-Scan pamoja na X-ray na kusababisha ugumu wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

Uharibifu wa mashine hiyo tangu Septemba 2010 umesababisha kusitishwa kwa huduma hiyo ambapo wagonjwa wanaotakiwa kufanyiwa kipimo hicho cha  CT–Scan hulazimika kusafirishwa hadi katika hospitali za Muhimbili au KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, mkurugenzi wa hospitali hiyo, Charels Majinge alisema kuwa pamoja na kukusanya Sh200 milioni kwa mwezi kama mapato ya hospitali hiyo, bado wameshindwa kutengeneza mashine hizo kwa wakati kutokana na gharama kubwa zinazohitajika.

Hata hivyo alisema kuwa kati ya mashine mbili za CT-Scan walizonazo wanatarajia kutengeneza moja mara tu kifaa cha UPS ambacho kinauwezo wa kupima wingi wa umeme kufungwa katika haspitali hiyo, “Matatizo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na ndiyo chanzo cha kuungua kwa mashine hizo ambayo kila moja inagharimu Sh4 billion fedha ambazo ni nyingi sana ”alisema dk Majinge.

Aidha hospitali hiyo inakabiliwa pia changamoto za ununuzi wa madawa ambayo yanaandikwa na madaktari bingwa ambayo hayapatikani katika bohari ya madawa ya MSD.

zaidi, soma gazetini: Mwananchi 

 


Comments




Leave a Reply