Akizungumzia tatizo hilo, Fundi Sanifu wa Mionzi na Radiolojia katika hospitali hiyo, Fabiani Mataba alisema mashine hiyo iiliyoharibika tangu Julai mwaka huu inafanyiwa matengenezo na Kampuni ya Mokasi Electronics and Medical Systems ya jijini Dar es Salaam.
Kwa wastani wagonjwa kati ya watano hadi sita kwa siku ndio walikuwa wakipata huduma hiyo hospitalini hapo kabla ya kusitishwa.
Picha za X-ray zilizokuwa zikipigwa ni kwa ajili ya wagonjwa wenye matatizo ya kibofu cha mkojo, mfumo wa uzazi, figo, vidonda vya tumbo na magonjwa mengine.
“Baada ya mashine yetu hiyo kukorofisha utendaji wake mwezi Julai mwaka huu tulichukua hatua ya kuipeleka matengenezo Kampuni ya Mokasi iliyopo Dar es Salaam, lakini mpaka sasa hakuna mwelekeo wowote wa matumaini kwa mashine hiyo kupona mapema,” alisema Mataba.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo, Dk. Fredy Mtatifikolo amekiri kuharibika kwa mashine hiyo ingawa alisema jitihada zinafanywa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambao ndio walioingia mkataba wa matengenezo na Kampuni ya Mokasi Electronics and Medical Systems.
via HabariLeo



RSS Feed