Audio iliyopachikwa hapo ni ya kipindi cha Njia Panda kilichorushwa na redio Clouds FM kila siku za Jumapili.

Kipindi kilichorushwa hewani tarehe 27 Machi 2011, kilihusu "uponyaji" unaotamkwa kuwa unapatikana Loliondo kijijini Samunge kwa Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Ambilikile Masapila ambaye anasema alioteshwa na Mungu ndotoni kuwa tiba hiyo itaponya magonjwa sugu ya VVU/UKIMWI, Kisukari, Pumu na Shinikizo la juu la damu.

Mahojiano katika kipindi hico kiliwashirikisha wataalamu wa Afya, Mmoja wa wagonjwa aliyekunywa dawa na kudai anajisikia kupona na Wachungaji wawili wa madhehebu tofauti ya Kikristo.

Mwendesha kipindi ni Dk. Isaac Maro.

Bofya kifute cha play hapo upate kusikiliza. Ikiwa huwezi kusikiliza, tafadhali bofya hapa kujipakulia audio.

NB: Kipindi kimewekwa vivyo kilivyorushwa, hakuna editing yoyote iliyofanyika ili upate picha kamili ya kilichojiri siku hiyo.
 


Comments




Leave a Reply