Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Sauti ya America, (Voice of America - VOA) wachunguzi wametafiti zaidi ya tweet milioni 11.5 kutoka maeneo fulani ya Afrika katika miezi mitatu iliyopita ya mwaka 2011 na wamegundua Afrika Kusini imetuma zaidi ya tweet milioni 5, ikiwa ni mara mbili zaidi ya watu katika nchi nyingine. Kenya ilikuwa ya pili ikiwa na karibu tweet milioni 2.5, ikifuatiwa na Nigeria, Misri na Morocco.
Katika uchunguzi huo iligundulika kuwa asilimia 80 ya wale washiriki wa utafiti huo walitumia twitter kuwasiliana na marafiki zao, karibu 70% walitumia kupata habari na watu zaidi kidogo ya 20% walitumia mtandao huo kujitafutia kazi.
--
via SundayShomari.com


RSS Feed