Prof. Mbele anasema, Mwaka 2002 nilisajili kampuni katika jimbo la Minnesota ambayo niliita Africonexion. Nilichagua aina ya usajili iitwayo "sole proprietorship" yaani mmiliki na mhusika mkuu ni mimi. Nilianzisha Africonexion kama chombo cha kushughulikia elimu kuhusu tamaduni duniani, kwa kuandika, kuchapisha, na kuuza vitabu, na kutoa mihadhara na ushauri kwa watu binafsi, mashirika, taasisi, makampuni, na kadhalika, kama ninavyoripoti katika blogu zangu. Africonexion ni kampuni ndogo sana kwa wakati huu, kwa maana kwamba sina timu ya wafanyakazi au washiriki. Lakini nimeitumia vizuri kama fursa ya kujielimisha, kwa kuzingatia kuwa elimu ni mtaji bora kuliko hata fedha. Shughuli zote ninazofanya, iwe ni kuandika au kutoa mihadhara au ushauri kwa watu binafsi, ni kama shule kwangu. Nimejifunza mengi sana, na bado najifunza. Maelezo na picha vimenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Profesa Mbele. Unaweza kupata maelezo zaidi ya kampuni hii kwenye tovuti ya africonexion.com au kwenye blogu yake ya hapakwetu.blogspot.com au wasiliana naye kupitia barua pepe: info@africonexion.com Comments27/01/2012 8:06pm
Shukrani, Da Subi, kwa kuiweka taarifa yangu hapa. Ni kweli kwamba kikampuni hiki kimejizatiti kutoa fursa kwa wajasiriamali wenye kupenda yale niliyoelezea. Labda niongezee tu kipengele maalum cha mkakati wote ni kutoa elimu kuhusu namna ya kuzitumia fursa zinazotokana na utandawazi wa leo. Hilo ni suala ambalo nimelitolea mihadhara mara kwa mara.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed