Nadhani kazi anayoifanya Isaac Kireti kama inavyoonekana kwenye picha hizo hapo, ni nzuri na sahihi kwa kutia changamoto na kuhamasisha umma kuyatunza mazingira ya maeneo wanamoishi na kufanyia shughuli zao za kila siku.

Inaonekana kama vile anaifanya kazi bila usaidizi hali watu wameketi wengine wakiwa wameshika tama, wengine kuikunja mikono katikati ya miguu na kusimama mbali kabisa kana kwamba kinachofanyika ni kituko. Pengine wana sababu, sijui.

Ninachodhani ni kuwa, mambo mengine hufanywa na watu wenye akili za tofauti na ingawaje huwa vigumu kueleweka wakati huo, matunda ya kazi hiyo yakiwa mema, hukubalina na kuonekana yenye manufaa baadaye sana ama pengine na kizazi kingine kabisa. Shughuli nyingine ili zifanikiwe, inahitaji mtu mmoja mwenye nia na azma kwanza, ili kulishawishi kundi kubwa.

Pongezi kwa juhudi hii ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira! Kwa hili nakuunga mkono!
 


Comments




Leave a Reply