Ni ujumbe kutoka kwa mdau wa afya, unajieleza! Tafadhali tuachane na kuuliza "nani mjumbe" tukazie "nini ujumbe"!

It is very possible that, private practice in India is driven by pay back system, you refer a patient to Apollo you get paid.

I just don't have evidence but I am sure move za hospitali kukusanya wagonjwa na kuwapeleka India zitakuwa driven by this payment system, I bet our officials may also be involved.

And these people are serious about that business, Apollo wanaanza kuwapa huduma wagonjwa Dubai, so from the airport you start getting services.

And the practice is made in such a way unafanyiwa vipimo vingi kadiri inavyowezekana, including those you don't need, the aim being to maximize the cost.

I am posted at Christian Medical College Hospital in India, this is a hospital which is not business oriented, but it is the best cardiology centre in India, it is one of the best nephrology centre in India also, iko Tamil Nadu km 120 kutoka Chennai.

The cost of services here is 1/3 ya gharama za Apollo and the like, the cost is even cheaper as compared to cost of some services in Nairobi (kuna mgonjwa alikuwa na leukemia Nairobi, gharama ya matibabu Nairobi ilitosha kulipia usafiri, matibabu gharama za kuishi hapa Vellore na akabaki na change), but guess what, no one is referring patient to CMC even in India itself because this hospital does not entertain the system of pay back!!!!!

It is very sad in deed!

YATOKANAYO...

Upo msemo mmoja ulivuma siku chache zilizopita, unasema, "ukiona manyoya, basi ujue keshaliwa"

Kwa hivyo, ujumbe huu unaweza ukawa umetufungua macho wengine tuliokuwa tukikuna vichwa kujiluliza kulikoni? Vipi  "kutiririka" kwenda India kwa matibabu kwa viongozi wetu kunashamiri na kushika kasi hivi? 

Mimi kwa mfano nilijiuliza:

Je! Hii inatokana na wagonjwa hao kukosa imani na tiba toka kwa wataalamu wetu? Kwamba, wanahisi wanapewa tiba isiyo na kiwango?

Au ni imani ya kasumba ya kujitakia au kufuata mkumbo tu kwamba matibabu ya "mzungu" au "mhindi" ama "mchina" yanaponesha vyema na haraka zaidi kuliko yale ya "mbantu" mwenzetu?

Hatuamini wala kuuthamini utaalamu wa wataalamu wetu?

Ikiwa madai yao kwamba wanakwepa huduma hafifu na mbovu, je, hawa viongozi wanaokuwa wepesi kutaka matibabu nje ya nchi, wanakosaje akili ya kuwawezesha wataalamu wetu kwa vifaa na mazingira bora ya kazi kwa kutumia fedha hizo hizo wanazozipeleka "India" ili nasi Watanzania tujivunie Watalaalamu wetu, wananchi wa kipato cha chini nao wasioweza kwenda "India" nao wapate nafuu ya tiba nzuri? Mbona tunadharauliana hivi? Umewahi kujiuliza ni kwa nini Watanzania wengi wanaohama nchi na kuajiriwa nchi nyingine wanasifika kwa uchapa kazi wao lakini wakiwa Tanzania walidharauliwa hata pale waliposhauri yaliyo ya haki? Ama ndiyo "Nabii hakubaliki kwao?"

Fedha wanazolipwa viongozi wetu hawa si zinatokana na kodi za wananchi na rasilimali za mumu humu ndani jamani? Sasa badala ya kuzizungusha humu ndani, ni kwa nini zinapelekwa kunufaisha mataifa ya nje?

Ama yote hayo hayana maana kwa kuwa fedha zenyewe, haziendi "nje" kweli bali zinazunguka na kurudi mifukoni mwao?

Hii nchi hii, ukisikia "pa" ujue ndiyo hivyo tena...!
 


Comments

Ng'wanamvanga
31/01/2012 13:00

Ukiongea na madaktari wa Tanzania, suala kubwa katika ufanisi wa tiba ni vifaa vya kuchukua vipimo <period>. Madaktari wa TZ wanafanya vizuri nje kwa sababu wanakuta vifaa vya kutosha kuwapa majibu sahihi na haraka.

Nina hakika gharama zinazotumika kupeleka wagonjwa nje kwa mwaka, zinaweza kuifanya hospitali moja ya rufaa ya TZ kuwa kama hizo za India (wanakokimbilia viongozi wetu)

Reply
EDDY
31/01/2012 22:35

your massage is delivered.

mdau ulietoa maada upo sahii kwa mawazo yako hata kama hakuna ushahidi wa kimaandishi kwa usemayo.

mdau uliyetangulia kutoa maoni pia upo sahihi kwani tukiamua tunaweza ila sio kwa mfumo wa serikali uliopo kwa sasa.

watanzania kwa ujumla kuanzia viongozi, wananchi hadi walalahoi tuna mapungufu mengi ya kiakili, wazito kufikiri, wavivu kuchambua mambo, wagumu kuelewa, wepesi kusahau, hatupendi kujifunza nk

tunauwezo wa kuboresha hosipitali zetu hata mbili tu na zikawa na wataalam wa nyanja zote, vifaa vya kutosha na mazingira bora kabisa ya tiba ila "HATUJATAKA KUFANYA HIVYO"

Reply
Mashingo
01/02/2012 04:02

1. tatizo la watanzania walio wengi ni kufuata mkumbo bila kutumia angalau dakika kadhaa kufikiri. kwa nini India? kwani hakuna nchi nyingine ya afrika ambayo ina huduma bora zaidi? sasa hivi mpaka internet wameanza kutangaza hospitali maalum kwa ajili ya watanzania. hamjiulizi mbona wahindi tulio nao hapa hawarudi kwao?
ni ukweli kwamba ukireffer mgonjwa kuna commission. nikiwa kama mmoja wa waliopata 'bahati' ya kusindikiza wagonjwa India, niliahidiwa
kupewa sponsorship na 'wenyeji wetu' iwapo ningefacilitate more refferals. Hawajifichi,hawa ni wafanya biashara sio ndugu zetu,so i don't blame them.Iits our own stupidity.
kwenda kutibiwa nje sio kosa au dhambi. Lakini iwe kweli imeshindikana hapa kwanza. Sio hali ilivyo hivi sasa ambapo viongozi wa juu wana haki ya kwenda 'KUCHEKIWA AFYA' nje ya nchi wao na familia zao. Amiin nawaambia,kama hili halitapigiwa kelele na kufutwa,hali ya hospitali zetu hasa hizi ambazo ndio wengi wetu tunakwenda itazidi kuwa hovyo. Umeona wapi mtu akahangaika kuboresha nyumba asimolala! Hivi tunaonekanaje huko nje?

2. Sikatai kweli kuna vitu wametuzidi, lakini tungeweza kuvifanya hapa kwetu kama tukiamua. Na serikali zinazojali na kufanya kazi kwa kutumia akili na kuona mbali huwa unaleta wataalam au unapeleka wa kwako huko unakodhani wamekuzidi kimaarifa ili watu wajifunze sio kupeleka wagonjwa. Mbona kenya walikuja kujifunza tunaendeshaje Mfumo wetu wa bima ya afya.

3. Kingine ni kuingiliwa kwa fani ya utabibu. Leo hii Tanzania kila anayejisikia kujiita daktari anajiita tu na bila kujali uwezo wake anatibu watu. Sijui kama Watanzainia hata wanajua kutofautisha. Na hii matokeo yake ni kugeneralise kuwa hii fani ni ya wasanii. Ni nchi pekee ambayo mgonjwa akifika kwa daktari anamkabidhi kila kitu na kumuachia afanye maamuzi yake,bila hata kuulizia matokeo yatakua yapi. Ni wagonjwa wangapi huwa hata wanauliza aelezwe anachoumwa na wajadili njia za matibabu na pengine kukataa njia moja na kuchagua nyingine! Ni wangapi wamefanyiwa upasuaji bila hata kuuliza kama ndio njia pekee,au hata kujua kwa juu juu tu kinachoenda kurekebishwa au kutolewa? Na hili ni tatizo,kwani hata mgonjwa anapoelezwa tatizo lake na options za matibabu wengi huwa wanaona kama wapotezewa muda.
Haya,with all due respect, hawa madaktari wanajeshi wanaopelekwa muhimbili wanatokea wapi? huko walikokua walikua wanareffer wagonjwa muhimbili kwa madaktari bingwa, sasa leo aliyekushindwa Lugalo ndio unamkuta muhimbili kitengo ambacho hata walio muhimbili kwenyewe sio wote wana utaalam nako. Ni kweli mtu yeyote anaweza akaitwa kutoka alikokuwa (jeshini, wizarani, mstaafu) na akaziba pengo! Sitaki kuamini kwamba ni rahisi hivyo. Na sidhani kama ni lazima sana wavae magwanda,ni wanajishi sawa, lakini pale ni hospitali,kuna maadili yake. Hata hospitali za jeshi huvai magwanda unapokua unatoa huduma. Au hawataonekana kuwa ndio waliopelekwa na serikali?

4. Dharau kwa vituo vyetu vya afya. Ni kiongozi gani alishawahi kwenda kwa mfano mwananyamala,au hata Muhimbili kwenyewe akapigwa picha akiwa kwenye foleni ya kusubiri tiba? lakini ni wangapi walipiga picha kwa babu wakinywa kikombe ambacho hata tafiti zake zimefanyika baada ya watu mamia kuwa wameshakunywa? na waziri wa ujenzi, Mh magufuli akatangaza kutenga tsh billioni 10 kwa ajili ya kumjengea barabara ili mkwanywe vizuri? ile ilipangwa kwenye bajeti? kama waliweza kumtengenezea mazingira mazuri ili mkanywe msichokijua,kwa nini wasifanye hivyo huku ambako wengi tayari angalau mna ufahamu nako na hata wasio na imani wanapona?
Ili kupitisha dawa mpya inabidi ifanyiwe utafiti si chini ya miaka 10! hii ni kwa sababu kila dawa ina madhara ya muda mfupi na yale ya muda mrefu. Leo hii wangapi wamejitokeza kuelezea madhara yaliyowakuta baada ya kunywa kile kikombe? Ni kweli hakuna,au ndio kila mtu na mzigo wake kwa sababu ulienda mwenyewe?

Mwisho kabisa, ningependa kutoa mifano michache.
Iwapo umelipia kampuni ya ulinzi ikuletee mlinzi,unatarajia mlinzi nyumbani kwako kama mlivyokubaliana. pale mlinzi asipotokea, utakachofanya ni kwenda kwa meneja au mwenye kampuni kudai mlinzi kama mlivyokubaliana.
Timu yetu ya taifa hatupangi sisi watazamaji. Tunakabidhi majukumu yote kwa kocha na kamati yetu ya ushindi. Na kama haikutuletea matokeo mazuri, tutalaumu mchezaji fulani lakini anaebeba lawama zote na kuwajibishwa ni kocha kwa kuchagua watu ambao hawakutufikisha pale tulipotaka.

Sasa kwa nini Watanzania tunaoteseka hatujaiuliza wizara na serikali kwa nini haiwawajibishi hawa watabibu ambao hawatoi huduma wanayotakiwa kuitoa?

Reply



Leave a Reply