Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea Januari Mosi mwaka huu huko katika kijiji cha Litisha kilichopo nje ya mji mdogo wa Peramiho.
Amesema kuwa usiku wa siku hiyo, Jota alikwenda nyumbani kwao ambako alimkuta mama yake mzazi akiwa amelala na baadaye alianza kutafuta namna ya kuingia kwenye nyumba hiyo ambayo mlango wake ulifungwa na komeo kwa ndani.
Jota baada ya kuona hivyo akaamua kuuvunja mlango wa nyumba hiyo kuingia ndani na kwenda moja kwa moja kwenye chumba alicholala mama yake mzazi (jina limehifadhiwa).
Imeelezwa kuwa, baada ya kufika chumbani, Jota alianza kumtisha mama yake kwa kisu alichokuwa ameshika mkononi na baadaye alimkaba shingo na kufanikiwa kumvua ngo ya ndani aliyokuwa amevaa kisha kumbaka.
Wakati Jota akiendelea kubaka, watu waliokuwa jirani na tukio walisikia kelele za mtu akipiga mayowe na walipofika kwenye eneo hilo la tukio waliingia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta Jota akitoka kwenye chumba alicholala mama yake.
Jota alipowaona watu alijalibu kukimbia lakini majirani hao walifanikiwa kumkamata na kumpeleka kituo kidogo cha polisi cha peramiho.
Kamanda Kamuhanda ameeleza kuwa polisi walimhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kulitenda kosa hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapokamilika.
---
habari imeandikwa na mwandishi wa blogu ya Stephano Mango


RSS Feed