Yafuatayo ni maoni aliyoyatoa katika kundi la WanaMabadiliko kufuatia majadiliano mbalimbali yaliyoelekea kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba upo uadui binafsi baina ya Rais Kikwete na Dkt. Slaa.  Mwalimu, Dkt. Lwaitama anasema:

Kwa uchambuzi wa kina HAKUNA ugomvi wala uhasama kati ya Ndugu Kikwete  na Ndugu Slaa; kama binadamu HAKUNA KABISA. 

Wapambe wachache wa Mh Kikwete kama Rais ambayo  ni taasisi wanajaribu kutengeneza hii taswira ya eti ugomvi na uhasama ili waweze kuhalalisha kuweza kumdhuru Ndugu Slaa vile wanahofia sana umaarufu wake unaozidi kufunika hicho wanachodhani ni umaarufu wa Ndugu Kikwete... Ni siasa uchwara kama alivyoziita Ndugu Rostam Aziz...

Ni siasa ambazo hapo nyuma nchini Kenya zilizaa siasa za kuuliwa kiongozi yeyote aliyeonekana kuwa kipenzi cha wananchi zaidi ya Rais...ni siasa zilizozaa mauwaji ya Tom Mboya, JMKariuki, na Robert Ouko. Dr. Slaa alisimamishwa na Chadema kugombea Urais 2010 na kama wizi wa kura ulizuia ushindi wa Dkt. Slaa  kuwa Rais bado hiyo si kisa kati ya Dkt. Slaa na Dkt. Kikwete... Hapana... hilo ni tatizo kati ya CCM na Chadema; kati ya CCM na Watanzania waliochoka ukiritimba wa utawala wa chama kimoja kwa nusu karne...HICHO NI  KISA KATI YA  CCM NA WATANZANIA KILICHOIMBUA KASI YA  KUDAI KATIBA MPYA NA TUME YA UCHANGUZI ILIYO HURU... SI SWALA BINAFSI KATI YA Dkt. SLAA NA Dkt. KIKWETE LAKUMALIZWA NA  ETI KWA KUNYWA CHAI PAMOJA IKULU... Rais Kikwete asijiruhusu kushawishiwa kukubali dhana potofu kuwa eti Dkt. Slaa ni adui yake... Hakuna kitu kama hicho
 
Adui wa Dkt. Kikwete ni kupanda kwa bei ya sukari na kuongezeka kwa bei ya umeme; ni kuzidi kudorora kwa uchumi kwa ujumla; na mawazo ya Rais yaelekezwe kwenye adui hao na wala hana haja ya kukutana na Dkt. Slaa eti kuyamaliza.. Kumaliza yepi? Bei ya sukari, mchele, mafuta ya taa na umeme au?  

Tuachane na dhana hizi za kijinga za wanasiasa na wanausalama uchwara wanaojikomba kwa Mh Rais ili awapatie ulaji kwa kumwambia eti adui yake mkuu  ni Dkt. Slaa vile eti Dkt. Slaa anakinyongo kushindwa kuwa Rais shauri ya wizi wa kura... Huo ni ujinga utokanao na kukataa kukubali ukweli   ulio wazi kuwa mwaka 2010 Dkt. Slaa  katu hakujipanga kwa mtandao wa miaka kumi wa kuusaka Urais  ulioundwa na ndugu na marafiki (ambao hawakuwa wale waliokutana barabarani) na uliogharamiwa na pesa za wizi kama ule wa EPA  ...Si hulka ya Dkt. Slaa na hana sababu ya kuyatafisiri matokeo tata ya uchaguzi wa 2010 kama mambo binafsi kati yake na ndugu yake Mtanzania mwenzake Dkt, Kikwete.  

Hoja hii ya eti Rais Kikwete amwalike Dkt. Slaa Ikulu wayamalize inatia kinyaa na kudhalilisha dhana nzima ya taasisi ya Urais.

Mwl. Lwaitama 
 


Comments

Kilimba Mgidingi
22/01/2012 07:12

Mwalimu uko sahihi naona Wtz wengi ni waoga wa kukubali hali halisi na ni wepesi wa kujipendekeza ndoo maana wakitishiwa kidogo tu wananywea!Maisha ya Tz yanakatisha tamaa hadi basi! Huwezi amini bei ya mafuta ukilinganisha na nchi ambazo wanapitishia biadhaa hiyo Bandari ya Dar bado bei yaoniko chini! Haya ndoo maisha bora kwa kilia Mtz au kila kigogo?

Reply
Kilimba Mgidingi
22/01/2012 07:12

Mwalimu uko sahihi naona Wtz wengi ni waoga wa kukubali hali halisi na ni wepesi wa kujipendekeza ndoo maana wakitishiwa kidogo tu wananywea!Maisha ya Tz yanakatisha tamaa hadi basi! Huwezi amini bei ya mafuta ukilinganisha na nchi ambazo wanapitishia biadhaa hiyo Bandari ya Dar bado bei yaoniko chini! Haya ndoo maisha bora kwa kilia Mtz au kila kigogo?

Reply
hamdu
22/01/2012 08:15

mafuta si kigezo nchi kama malawi na zambia bado wananchi wanaishi maisha magumu Tz bado wapo juuu

Reply



Leave a Reply