Mwasikili ataichezea "Lüleburgaz Gücü Kulübü" inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake nchini humo.
Mchezaji huyo kiungo wa kati wa Twiga Stars aliyekuwa akichezea timu ya Sayari Women amejiunga na klabu yake hiyo mpya kwa mkataba wa miaka miwili.
Awali Mwasikili alitakiwa kujiunga mapema na timu hiyo lakini alilazimika kusubiri kwanza mechi ya marudiano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia (Brave Gladiators) iliyochezwa Januari 29 mwaka huu.


RSS Feed