Wafanyabiashara wawili mtu na mkewe, wamepigwa risasi na kumwagiwa tindikali huko Zanzibar kwa kuuza pombe. 

Katika uvamizi huo uliofanyika Jumatano iliyopita mwanamke Bimal Alvind (36) alinusurika kupoteza ujauzito wake wa miezi minne baada ya kupigwa risasi ya tumbo na kumwagiwa tindikali. 

Risasi hiyo ilitolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kuathiri ujauzito huo lakini tindikali hiyo ilimjeruhi mwilini kuanzia usoni, kifuani kwenye matiti, mikono yote miwili na tumboni. 

Mumewe, Alvind Asawla (42) alipigwa risasi kichwani kwenye paji la uso katikati ya macho iliyotokea nyuma chini ya shingo na sasa amepooza upande mmoja. 

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwa ndugu yake Upanga wiki hii, Asawla alisema walivamiwa Jumatano iliyopita saa 10:30 jioni katika Mtaa wa Hurumzi Mji Mkongwe.
Alisema wakati wakivamiwa, yeye na mkewe aliyeishi naye kwa miaka 17 sasa na kujaliwa watoto wawili; Priyanka (14) na Nidh (12), walikuwa wakitoka katika biashara yao wakirudi nyumbani eneo la Kiponda. 

Alisema ghafla watu wawili walimvamia mkewe na kummwagia tindikali na yeye alipokuwa akijaribu kumsaidia, watu hao walimmwagia tindikali usoni. 

Kwa mujibu wa Asawla, wakati wakitaharuki kwa hali hiyo, ghafla alitokea mtu mwingine na kumpiga risasi katika paji la uso akadondoka chini huku damu zikimtoka. 

Alisema alijaribu kujikongoja kwa nia ya kuendelea kumsaidia mkewe lakini mtu huyo wa tatu alimpiga risasi ya pili mgongoni na mkewe akapigwa risasi ya tumbo.  

Asawla alisema baada ya hapo hakujua kinachoendelea mpaka alipozinduka Kituo cha Polisi cha Malindi walipopatiwa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja walipopigwa picha za x-ray na kugundulika wana risasi mwilini. 

Baada ya kipimo hicho, Asawla alisema hospitali hiyo haikuwa na vifaa vya kutoa risasi hizo, ndipo ndugu zake waliwasaidia usiku huo na kuwasafirisha kwa ndege hadi Dar es Salaam ambapo walikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Alisema mkewe alilazwa katika wadi ya Kibasila namba tatu na yeye akahamishiwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya kipimo cha CT-Scan ambacho hakikupatikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Kwa mujibu wa Asawla, mke wake alitolewa risasi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na yeye kufanyiwa upasuaji wa kumtoa risasi ulifanyika katika Hospitali ya TMJ. 

Alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa ni mzima hadi sasa kwani alipigwa risasi sehemu mbaya na kukaa nayo kwa saa zaidi ya 12 ndipo ilipotolewa kichwani jambo lililowashangaza hata baadhi ya wauguzi. 

“Nimepooza upande mmoja wa kichwa changu, sihisi jambo lolote lakini madaktari wameniambia nitarudi katika hali yangu ya kawaida polepole baada ya kufanya mazoezi,” alisema. 

Alisema aliambiwa kuwa risasi hizo hazikupita katika mishipa mikubwa ndiyo maana yuko hai hadi sasa na mshipa mdogo uliomwaga damu, umefanya jicho la upande uliopooza kuwa jekundu licha ya kuona vizuri. 

Mfanyabiashara huyo alisema kuwa watu hao wamempa ulemavu wa kudumu bila kutegemea huku akiamini siyo majambazi ingawa walichukua pochi ya mkewe iliyokuwa na fedha kidogo. 

Alisema hospitalini wameambiwa tindikali waliyomwagiwa ni aina ya asidi sulfuriki (sulphuric acid) inayotumika katika magari. 

“Unajua mwizi anataka fedha na siyo kumwagia tindikali au kukupiga risasi na sisi hatukuwa na silaha yoyote; nia ya watu hawa ni kutuua kwani tumekuwa tukipata vitisho vya mara kwa mara kutokana na biashara yetu ya kuuza pombe Zanzibar,” alidai.

Alidai mara kwa mara wamekuwa wakipata vitisho ikiwemo kukuta karatasi inayomtaka kuacha biashara hiyo vinginevyo utauawa; na wamekuwa wakitoa taarifa katika vituo vya Polisi vilivyopo karibu na biashara zao. 

Alilalamika kuwa licha ya wafanyabiashara wengi wa pombe kufanyiwa vitendo vya kumwagiwa tindikali, kupiwa risasi na hata kuchomwa moto, hakuna aliyewahi kukamatwa na kuchukuliwa hatua. 

“Sisi tunafanya biashara na mahoteli makubwa ya kitalii na tunalipa kodi zote stahiki, Serikali iseme wazi kama haitaki biashara hii Zanzibar au wawadhibiti watu hawa,” alisema. 

Alidai kuwa matukio kama hayo ni ya muda mrefu na mwaka 2007 wakati wa Jumatatu ya Pasaka, baba yake mzazi, Ahandillal Asawla aliyekuwa akifanya biashara hiyo alimwagiwa tindikali usoni akafariki dunia. 

“Hata baba yangu aliuawa lakini hakuna hata mtu aliyekamatwa na Serikali haikufanya jambo lolote, sasa umefika wakati Serikali itulinde tunaofanya biashara hii au itangaze kusitisha kwa manufaa yetu,” alisema Asawla. 

Alisema cha kushangaza tangu ukoloni babu zake waliuza pombe kwa amani lakini sasa wanatumia pombe kama sababu za kisiasa ili kuangusha uchumi wa Zanzibar. 

Gazeti hili liliwasiliana na uongozi wa Polisi katika Mkoa wa Mjini Magharibi bila mafanikio. 
Kwanza Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi, ACP Azizi Mohamed simu yake iliita bila majibu na simu ya Kamisha wa Polisi Zanzibar, CP Musa Musa haikupatikana pia. 

Baadaye gazeti hili lilifanikiwa kumpata Ofisa Uhusiano Polisi Zanzibar, Asha Mzule lakini alisema kuwa ni mgonjwa kwa muda kidogo hivyo hajui kinachoendelea na kutoa namba ya simu ya OCD wa Wilaya ya Mji Mpya. 

Hata hivyo OCD huyo alikataa kuzungumzia uvamizi huo wala kutaja jina lake lakini akashauri atafutwe ACP Azizi ambaye alidai yuko Uwanja wa Ndege akimsubiri Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein anayetokea nje ya nchi. 
Namba ya ACP Azizi ilipopigwa kwa mara ya pili, haikupatikana kabisa.  
--

Picha via blogu ya Lukwangule, habari via HabariLeo
 


Comments

Ng'wanamvanga
23/01/2012 11:09

Haya ni matokeo ya unafiki wa viongozi wa Zanzibar; wanajua biashara ya pombe kupitia utalii ndio inaendesha Zanzibar kwa sasa maana karafuu hakuna tena. Lakini wanawadanganya wananchi wasio na elimu ya kuchambua mambo kupitia upofu wa dini.

Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi wawe wa kweli maana haiwezekani matukio ya kuchomwa nyumba za kuuza pombe na haya mashambulio wasiyajue. Wahache unafiki, kama hawataki kodi ya pombe basi waweke wazi kuwa pombe hairuhusiwi ZNZ.

Reply
Ifude
23/01/2012 21:13

Hakika wa kulaumiwa ni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo visa kama hivi vimedumu kwa muda mrefu huko Zanzibar. Watalii watakuja vipi huko Zenji bila kuwapatia mahitaji yao? Kama utalii unakubalika ni vyema uhuru wa kibiashara halali ukapewa nafasi yake. Tamko la serikali ya Zanzibar hususan Jeshi la Polisi itolewe kuhusu uonevu na ukimya huu.

Reply
Bingu wa Kilasi
23/01/2012 21:21

CUF wanakuja kwa mtindo mwingine wa kuiyumbisha serikali, du waislamu sasa wanatupeleka Nigeria! maana na bara si shwari, eti wanataka misikitiktk mashule ya serikali

Reply
mussa
06/02/2012 04:12

una mawazo mgando dogo

Reply
Jo
24/01/2012 01:20

Loooo kusema ule ukweli, waislam ni watu wa fujo (sijui kama ni wote, ila sijawahi kuonana na mpenda amani) . Yaani Mungu wao hana nguvu mpaka wanaingia uwanjani wenyewe na tindikali. Imefikia point nawachukia, am sorry for this but that is the truth.

Reply
K.L
24/01/2012 06:23

Bw. Jo nimependa ushujaa wako wa kueleleza kinaga ubaga rai yako. Nami pamoja na kupenda ushujaa wako natofautiana nawe katika msingi wa hoja yako. Mimi ni Mwislamu, NAPENDA AMANI NA NAPENDA SANA WATU WA DINI ZOTE NA HATA SIKU MOJA SISEMI KUWA DINI YANGU NI BORA KULIKO DINI NYINGINEZO.
Chuki iliyojengeka kwako ambayo kwa upande fulani imesababishwa na vitendo viovu vya baadhi ya waislamu ndiyo iliyokufanya UWACHUKIE WAISLAMU(you are somehow right) LAKINI katika maisha yetu ya sasa si busara kuwachanganya wooote kwa kosa la baadhi ya watu wa kundi fulani.Nakwambia hivyo kwa sababu mimi kwa sababu ya rangi yangu MTU MWEUSI nilibidi kulipa kosa la mtu mweusi aliyemfanyia ubaya mtu fulani mweupe na huyo mweupe alipokutana nami kwa ile chuki ya kile alichofanyiwa na mweusi nisiyemjua aliimalizia chuki yake kwangu.(by the way mimi naishi nje ya bara la Afrika)
Tangu siku ile nimejifunza jambo HALITOFUTIKA KATIKA MAISHA YANGU HADI NAKUFA. SI SAHIHI KULICHUKIA KUNDI FULANI KWA SABABU YA KOSA LA MTU FULANI WA KUNDI FULANI

Reply
i b
24/01/2012 10:11

Weweee.... Chunga mdomo wako...

Reply
suhail Daud
24/01/2012 12:05

Kuwa na heshima! Unaonesha wazi kama Ni mtovu wa adabu...ungelikua mstaarabu ucngeliongea maneno haya

Reply
SAMIR HAMDAN
24/01/2012 21:59

WE JOO PUMBAVU SHIKA ADABU YAKO U BETTER WATCH EVERY SINGLE WORD THAT COMES OUT OF YOUR MOUTH

Reply
mussa
06/02/2012 04:14

naomba ukausome uislamu ueelewe vizuri hakuna dini inayojali amani zaidi ya uislam na ukome kusema waislam ni watu wa fujo.

Reply
lupa mwalufuna,au josephlupa.
24/01/2012 02:30

mmh jaman ,mnavyofanya sio vizuri maisha ni magumu sana haswa katika swala zima la kipato,mtu akijitafutia na havunji sheria nchi,ninyi shida yenu nini,au hajlipa ushuru,au mnatakawote tuuze urojo0,uoo si ubinadamu,mbona uku bara hakuna ata siku moja umesikia et kule temeke mlipo mjaa,mmevamiwa au mmeshambuliwa,acheni ubinafsi na muendelee kusoma kwa bidii,msije mkauwa na watalii wano changia pato la taifa lenu maskini,mnaboa.

Reply
mussa
06/02/2012 04:20

hayo mawazo yako ya kibaguzi wewe josephlupa bakia nayo mwenyewe inaonekana wazi unutanganyika na uzanzibari sisi hatuko huko tunachokataa ni pombe zanzibar twaweza ishi bila pato lolote kutoka kwenye pombe na wala hatukuangalii unatoka wapi once unakuja na pombe sisi ni kwamba hatutaki hicho kitu ni baba wa maasi,unawaambia watu wakasome wewe mwenyewe unaonesha wazi si msomi

Reply
Kilimba Magidingi
24/01/2012 05:48

Nyie ya huku Nigria yasikieni tu! Huku Waislamu tayari wameshatangaza Wakristo wote wahame Majimbo yote ya Kaskazini! Zanzaibar watengwe na waachwe wajiendeshe wenyewe na Waislam wa Tz wajue kuwa wakianzisha sisi tutalimalizia!

Reply
mussa
06/02/2012 04:21

humtishi mtu we

Reply
Saleh
24/01/2012 06:21

Unaposema waislaam wote wabaya au din ya kiislamui ni mbaya unakosea sana kwani dini ya kiislamu haijawatuma au kuwafundisha watu wawatendee wenzao ubaya au kuwamwagia watu tindikali na hao wanaofanya vitendo hivyo wanatumia dini ya kiislamu kwa masilahi yao na sio kwa ajili ya masilahi ya kidini, hakuna dini duniani inayotangaza fujo au vita.dini zote zinatangaza amani na upendo.Je tuseme wale mapadri waliowalawiti waumini wenzao haina maana wanawawakilisha wakristo wote kwa staili ile au ina maana na sisi waislaam tuuchukie ukiristo kwa matendo ya watu wachache kama hao mapadri?pia kumbuka kuna wachungaji wamekamatwa na madawa ya kulevya na silaha je kwa matendo ya hao watu wachache tuwachukie wakristo wote? Wacha kupandikiza chuki zisizo na maana.dini zote ni sawa.

Reply
Baba Bright/Asie penda Makuu ila Ukweli!
24/01/2012 10:04

Poleni sana wahanga wa tukio la kinyama kama hilo huku vyombo vyote vya dola vikishuhudia na kujificha kwenye msitu wa visingizio visivyokuwa na uhalisia. Ila mtazamo wangu ni huu: ninyi wavamizi inaonesha bado hamjajua nani adui yenu hasa, kwangu mimi wauza pombe sio adui zenu ila adui zenu ni waliotunga sheria kuhalarisha uuzwaji wa pombe zanzibar, hivyo pambaneni na serikali ipeleke mswaada bungeni kutengua sheria inayo halarisha uuzwaji pombe huko zbr kwanza, ndipo hatimaye mpambane na hao wanaharamu watakao endelea kuuza pombe hata baada ya serikali kupitia sheria halari ya bunge kuharamisha vitendo hivyo.
Pili mimi naona ninyi mnao wadhuru wauza pombe mnahatia ya unafiki! kwani mnajifanya kuchukia wauza pombe na pombe, ilihali hata fedha mlizo lipwa kwa kazi hiyo ya kinyama zina tokana na pombe na ndio maana mkaamua kuondoka na pochi yenye fedha kidogo ya wahanga ambayo kimsingi imetokana na pombe, hivyo na washauri acheni unafiki wakujifanya mnachukia kinyesi ilihali maisha yenu kwa zaidi ya 90% yantegemea funza wanaokulia kinyesi. Kwangu mimi kama kuuza pombe ni dhambi na kumwaga damu ya mtu ni dhambi hivyo nyie wavamizi mnayo hatia kwa umwagaji damu mlioufanya!

Reply
babu
24/01/2012 10:15

"Alilalamika kuwa licha ya wafanyabiashara wengi wa pombe kufanyiwa vitendo vya kumwagiwa tindikali, kupiwa risasi na hata kuchomwa moto, hakuna aliyewahi kukamatwa na kuchukuliwa hatua".

SERIKALI YA MAPINDUZI IPO NYUMA YA VITENDO HIVYO NDIO MAANA WAPO KIMYA. HIVI KUNA HAJA YA KUENDELEA KUWABEBA HWA WAZANZIBARI? KWANN HUU MUUNGANO USIVUNJIKE NA KILA WATU WACHUKUE USTAARABU WAO, WABARA WARUDI HUKU NA WAO WARUDI KWAO.

Reply
safia
24/01/2012 21:34

Reply
safia thabit
24/01/2012 21:38

hey kwa wote waisilam na waiksistuuu jst nataka kusema mr jo kwa kusema la kweli tabia unayoo sio nzurii wala sio heshma unapo kua na hasira na watu sio lazima uingize dini wala mungu hakuhusu kama ww mungu wako ananguvu mbona hajaja kuwasaidia hao watu so stop ur silly comments and keep it to ur self hp imekufikia

Reply
kidas
27/01/2012 05:03

kwnza nawapa pole wale wote uliofanyiwa ukatili wa kumwagiwa tindikali.............lkn tuelewe kitu kimoja.... tusichanganye dini ktk maswala hayo hayo ni mambo ya siasa au la . uislamu hausemi kumdhuru binadamu mwenzako au la

Reply
mr shayo
29/01/2012 04:52

Lazima tujitambue ya kwamba hatupaswi kuwadhuru wenzetu kwa jambo lolote. Nawapa pole sana hao wenzetu waliojeruhiwa.

Reply
10/02/2012 05:19

ni jukumu la serikali kuwa makin ktk maswala kama haya hususani jeshi la pole na pindi tunaposema itikadi za kidin tunakosea kwan kila nchi inakuwa taratibu zake din haiwez kutawala nch ni serikali kuwa makini la sivyo tutazidi kupoteza umoja ktk jamii

Reply
10/02/2012 05:21

ni jukumu la serikali kuwa makin ktk maswala kama haya hususani jeshi la polisi na pindi tunaposema itikadi za kidin tunakosea kwan kila nchi inakuwa taratibu zake din haiwez kutawala nch ni serikali kuwa makini la sivyo tutazidi kupoteza umoja ktk jamii

Reply



Leave a Reply