Jioni yaleo, Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbrod Slaa pamoja na viongozi na wajumbe wengine wa CHADEMA wamekutana Ikulu kwa mwendelezo wa mazungumzo ya mchakato wa muundo wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania. 

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Freeman Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika, Said Arfi, John Mrema, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari. 

Katika mkutano wa awali ambapo Rais alikutana na baadhi ya viongozi wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa hakuhudhuria.

Zifuatazo ni picha za Ikulu za mkutano wa leo. (Picha za mkutano uliotanguli aunaweza kuziona kwa kubofya hapa).

Mkutano huo ulihitimishwa saa tano na robo usiku! 
 


Comments

rehema
26/01/2012 06:09

HUO NDIYO UZALENDO WA KWELI NA SISI SOTE NI NDUGU, WATOTO WA BABA MMOJA.

Reply



Leave a Reply