Taarifa Habari TBC na BBC Swahili - Dkt. Mponda na Dkt. Ulimboka kuhusu mgogoro wa Madaktari31/01/2012 Audio ya BBC Swahili kipindi cha Dira anasikika Dkt. Ulimboka na Waziri, Dkt. Mponda wakizungumza kuhusu mgogoro wa Madaktari na Serikali Taarifa ya Habari TBC leo ikizungumzia suala la mgogoro wa Madaktari na suala la posho ya Wabunge. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda (kushoto), akizungumza na baadhi ya madaktari toka vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Dar es Salaam jana, walipofika kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ili kutoa huduma kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea nchini. (Picha: Rajabu Mhamila) Madaktari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiangalia maiti iliyoletwa ili kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es salaam jana, Serikali imeagiza madaktari wa vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama kuhudumia wagonjwa ili kuziba pengo la madaktari waliogoma. (Picha: Rajabu Mhamila) CommentsLeave a Reply |


RSS Feed