TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

NDUGU WANAHABARI

Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mola wa viumbewote. Pili tuna kushukuruni kwa kuitikia wito wetu licha ya kuwa namajukumu mengi ya kutoa taarifa kwa wananchi. Kwa mara ya kwanza tumeamua kukutana nanyi. Nasi tunatoa taarifa yetu hii kwenu ilimuifikishe kwa Watanzania na wapenda amani wote duniani. Tunakuusienijuu ya ukweli na uaminifu katika kuripoti taarifa hii.Tuna kuusieni tena kuripoti taarifa hii bila ya kupotosha maana iliyokusudiwa.Kutakuwa na nafasi ya maswali ili kuuliza ikiwa kunasehemu ambayohaikueleweka.

NDUGU WANAHABARI

Tuliowaita ni viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa KiislamuTanzania yaani Tanzania Muslim Students & Youth Association (TAMSYA).Jumuiya yetu inatambulika kisheria na inafanya kazi zake kwa kufuatasheria za nchi.

NDUGU WANAHABARI

Jumuiya yetu kama inavyojieleza inashughulika na malezi ya wanafunziwafuasi wa dini ya kiislamu waliopo katika shule, vyuo vya kati navyuo vikuu na vijana wa kiislamu kwa ujumla. Jumuiya hii inawalingania waishi kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Uislamu.

NDUGU WANAHABARI

Tumeamua kukutana nanyi ili kuzungumzia mambo ambayo yanawapatawanafunzi waislamu waliopo kwenye shule na vyuo vya serikali kwa mudamrefu. Wanafunzi waislamu wamekuwa wakinyanyaswa na kuwekewa vipingamizi vya makusudi ambavyo vinasababisha kufanya vibaya katikamasomo yao pindi wakiwapo shuleni.

NDUGU WANAHABARI

Sheria ya nchi inaruhusu uhuru wa kuabudu na kuchagua dini. Kwa mujibuwa dini yetu ya uislamu ibada haimaliziki kwa kuingia msikitini nakuswali tu bali Uislamu wenyewe ni mfumo kamili wa maisha. Ibada nikila jambo analolifanya muislamu na linaloridhiwa na Mwenyezi Mungulikiwa katika muundo wa vitendo au kauli za dhahiri na kificho.

NDUGU WANAHABARI

Tumepata malalamiko kutoka kwa wanafunzi waislamu wakikatazwa kuvaa HIJABU shuleni,

Tumepata mashitaka kutoka kwa wanafunzi waislamu wakinyimwa sehemu zakusalia/kufanya ibada ya sala katika mazingira ya shule na vyuo.Tumepata mashitaka juu ya kupangwa makusudi matukio mbali mbali ya shule katika nyakati za sala za waislamu. Mfano sherehe za Mahafalizinapangwa kufanyika siku za Ijumaa muda wa sala, Ratiba za mitihanivyuo vikuu hazizingatii muda wa swala ya Ijumaa .kurefusha muda wa kusimama mstarini (Parade) mpaka muda wa swala unapita.Wanafunzi waislamu wamekuwa wakikatazwa kuvaa kofia au kanzu baada yamuda wa masomo katika shule za bweni huku wakristo wakiwa wanashinda na Rozari masaa 24.Waalimu wanaofundisha somo la maarifa ya uislamu wanawekewa vikwazo mbalimbali wakati wachungaji wanapishana katika shule bila vikwazo kwenda kufundisha baibal knowledge.

Vipindi vya dini vinawekwa katika ratiba za shule muda wa saa saba mchana siku ya ijumaa wakati ambao wanafunzi wa kiislam wanapaswa kuenda msikitini kwa ajili ya swala ijumaa.

NDUGU WANAHABARI

Tutatoa mifano kadhaa katika maeneo tofauti ambayo wanafunzi waislamwamefanyiwa madhila, manyanyaso na udhalilishwaji ikiwa ni pamoja na kutukaniwa Mungu wao,mtume wao na kitabu chao (Quran tukufu) na TAMSYA imefuatilia bila ya mafanikio.

SHULE YA SEKONDARI KIZUNGUZI WILAYANI KILOSA –MOROGORO

Mwanafunzi wa kidato cha nne, Frank Thobias Cosmas, aliandika waraka ulioukashifu uislamu, Qurani tukufu na Mtume Muhammad Sallalahu alaihi wasallam.Wakati wanafunzi wakristo wakiwa wanaubandika katika mbao za matangazo shuleni hapo na kusambaziana waraka huo Tarehe 13/05/2011 mwanafunzi muislamu Saidi Suleiman aliupata na kuufikisha kwa viongozi wa wanafunzi waislamu na hatimaye malalamiko hayo yalifika kwa mkuu wa shule.Mkuu wa shule alimpa Adhabu Yule mwanafunzi aliye peleka taarifa na

viongozi wa wanafunzi waislamu walisimamaishwa shule kwa muda wa siku 21, na Yule aliyendika waraka huo alibakishwa kufanya kazi za shule.Tukio hili liliripotiwa kwa Mkuu wa polisi Morogoro, Afisa Elimu

Mkoa Morogoro na ofisi ya mkuu wa wilaya ambao walipuuza. Hatua hiyo ilisababisha waislamu wa Mkoa wa Morogoro kuandamana kwa amani siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti, 2011.

PIA SHULE YA SEKONDARI ULONGONI – DAR ES SALAAM

Siku ya Alhamisi,tarehe 27/01/2011Mkuu wa shule hiyo aliwalazimisha wanafunzi wa kike wa shule hiyo kuvua Hijabu wakati wa zoezi la kupiga picha kwa ajili ya Mtihani wa kidato cha nne.Alifanya hivyo kwa chuki za udini kwa sababu waraka wa baraza la mitihani unaotoa maelekezo ya namna na utaratibu wa kupiga picha kila mkuu wa shule amepatiwa na haukuagiza hivyo.

SHULE YA SEKONDARI ENGUSERO KIBAYA –KITETO

Mkuu wa shule hiyo kwa kushirikiana na Kaimu katibu Mkuu wa mkoa wa Manyara kwa barua yake ya Kumb.Na.FA.58/347/01/27 aliwaamrisha wanafunzi wavunje msikiti uliopo hapo shuleni kwa madai ya kwamba katika shule za serikali hairuhusiwi kujengwa nyumba ya ibaada. Lakini sikweli kwa kuwa zipo shule nyingi za serikali zilizo na nyumba za ibada makanisa tena makubwa sana. Mfano Shule ya sekondari Ndanda,

Shule ya sekondari Umbwe, Lyamungo Sekondari, Pugu Sekondari Dar es salam na karibu shule zote kubwa za Serikali nchini. Huu ndio udini na mfumo kristo unaolalamikiwa na unaoliyumbisha taifa.

SHULE YA SEKONDARI ALDERSGATE BABATI MANYARA

Mkuu wa shule hiyo aliwanyima wanafunzi waislamu darasa kwa ajili ya kusomea somo la maarifa ya uislamu na kuwaambia kama wanataka kusoma somo la dini wachanganyike na wakristo ambao wamepewa chumba cha kusomea shuleni hapo, Jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za nchi.aidha alipiga marufuku uvaaji wa hijabu shuleni hapo kwa taarifa tuliyo letewa ya 17/03/2011.

SHULE YA SEKONDARI LUGOBA

Mwalimu aliwataka wanafunzi waislamu washerehekee Krismas walipokataa akawaambia tutaweka Taarabu maana waislamu mnapenda sana taarabu.Siku ya 21/01/2011 kwa makusudi Makamu Mkuu wa shule hiyo aliingia na viatu katika eneo la chumba wanachotumia waislamu kuswalia na kuwaamuru watoke katika chumba hicho wakati wa swala.Makamu Mkuu huyo alikwenda tena siku ya tarehe 31/01/2011 kwa hasira na kundi kubwa lililo sheheni wanfunzi wakristo kwa ajili ya kuwafanyia fujo waislamu waliokuwa wakiswali. jambo ambalo lileta tafrani kubwa shuleni hapo cha kusikitisha ni kuwa ukweli ulipotoshwa na hatimaye wanafunzi waislamu walionekana ndio chanzo cha tatizo.

SHULE YA SEKONDARI ILBORU ARUSHA

Mwanafunzi Juma Hassan alifukuzwa shule 13/01/ 2006 ikiwa ni wiki tatu kabla ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita. Sababu ya kufukuzwa shule ilidaiwa alimsukuma Mama Mkwizu mwalimu sheleni hapo alipotaka kuingia msikitini.

SHULE YA UFUNDI TANGA JIJINI TANGA

Mwaka 2006 Mkuu wa shule hiyo bwana T. Z. Kinala amekuwa na tabia ya Kutoa salamu ya HALELUYAH mstarini wakati wa PAREDI huku akijua kwamba wanafunzi walio mbele yake ni mchanganyiko wa waislamu,wakristo na watu wa dini nyingine.Lakini si hivyo tu, Tarehe 24/7/2006 mkuu wa shule alileta kikundi cha kwaya cha kanisa wakati PAREDI na kuimba nyimbo za ibada ya kikristo.

Wakati alipo kuwa akiongea na wanafunzi wa, katika hafla fupi ya kuwakaribisha kidato cha tano mnamo tarehe 28/4/2006 Pia alitamka wazi wazi kuwaambia wanafunzi waislamu kuwa hapa shuleni hakuna kuswali swala tano kwani hii siyo seminari.Mnamo tarehe 18/06/2006 aliwaambia wanafunzi wa kiislamu wanaovaa mavazi yanayotambulisha uislamu wao, kama Kofia, Kanzu na Kilemba lau kama angeliwajua asingewachagua kujiunga na shule yake.Mnamo tarehe 02/08/2006 aliwaita waislamu wanaovaa mavazi ya kiislamu kama kanzu kuwa ni Mashoga

NDUGU WANAHABARI CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

Madhila haya na manyanyaso hayawasibu wanafunzi wa kiislam waliopo mashule tu lakini hata wale waliopo vyuo na vyuo vikuu pia hawajasalimika hapa tutatoa mfano wa chuo kimoja tu cha Dodoma (UDOM) ambako wanafunzi wa kiislam chuoni hapo wamekuwa wakidhalilishwa, kwa kutukaniwa dini yao na mtume wao mfano wa haya ni mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo yalibandikwa matangazo yenye ujumbe unaowatukana na kukejeri uislam na waislam kuwa ni watu wasioweza na wasiostahiki kuongoza,jambo ambalo liliwafanya wanafunzi wakiislam chuoni hapo kuripoti katika uongozi wa chuo na vyombo vya usalama bila ya kupewa msada, hatimae waislam waliamua kujitowa katika mchakato huo wa kampeni na uchaguzi wakiwa na nia njema ya kujiepusha na uadui na uhasma baina yao na wanafunzi wa dini zingine, lakini hata hivyo baada ya uchaguzi walitukanwa na kukashifiwa wazi wazi na wakirsto wakishangilia kwa kusema Yesu ameshinda na Mohammad ameshindwa katika kona zote za chuo, bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka husika za chuo na serikali.

NDUGU WANAHABARI

Tukio kubwa na la kusikitisha kwa wakati huu ni hili la shule ya sekondari NDANDA iliyopo mkoa wa MTWARA wilaya ya Masasi tarafa ya Chikundi kata Mwena kijiji cha Ndanda. Mpaka hivi sasa tunapozungumza nanyi wanafunzi ishirini (20) wa kiislamu wamefukuzwa shule watano (5) wakiwa ni kidato cha tano na kumi na tano ni kidato cha sita ambao wanatarajiwa kufanya mtihani wa mwisho mwanzoni mwa mwezi wa pili. Aidha wengine waliosalimika kufukuzwa shule wamewekewa masharti magumu

ya kusaini ikiwa wanataka kuendelea na shule hiyo ya serikali.Miongon mwa masharti hayo ni kutojihusisha na dini yao wakiwa shuleni sharti ambalo linapora haki ya kikatiba ya kuabudu.Sababu na kosa la kufukuzwa wanafunzi hao wa kiislam likiwa ni kuuomba uongozi wa shule uwape eneo maalumu la kufanyia ibada (Msikiti) kama vile walivyotengenezewa wanafunzi wakirsto kanisa kubwa shuleni hapo, kulalamika lugha za kashfa na dharau ambazo zinatolewa na mkuu wa shule dhidi ya wanafunzi wa kiislamu uislamu shuleni hapo.

Kilichowaponza wanafunzi waislamu ni kupinga udini wa mkuu wa shule na upendeleo kwa wanafunzi wakristo, mfano kitendo cha mkuu wa shule kuteua viongozi wa serikali ya wanafunzi kiholela na kiupendeleo kwa wakirsto huku wakitoka nje ya shule wakishangilia na kusema Muhammad ameshindwa katika uchaguzi mwache bwana Yesu atawale shule!!! Haya yamefanyika mkuu wa shule akiyaona bila ya hata kukemea na kuwaadabisha wanafunzi wahusika jambo ambalo linaonesha wazi wazi kuwa ni mpango maalum ulio sanifiwa kwa mfumo maalum.

NDUGU WANAHABARI

TAMSYA mikoa, wilaya na matawi, shule na vyuo kwa muda mrefu imefanya jitihada mbalimbali za kuonana na wakuu wa shule na watendaji husikaNkatika kadhia hizi na kuishia kupuuzwa bali na kupewa majibu ya kejeli na jeuri. Na baadhi ya wakuu wa shule kuomba msamaha na kuahidikutorudia tena, lakini baada ya muda mfupi hurejea na kuendeleza dhulma na madhila kwa wanafunzi wakiislam kwa kasi ya ajabu.

Pia walimu walezi wa wanafunzi wa kiislamu au hata walimu waislamu wanao thubutu kuhoji juu ya ubaguzi wa kidini pia huonekana vioja huku wakichekwa na hatimae kupewa adhabu ya kuhamishwa kituo cha kazi kiholela mfano dhahiri ni walimu wawili pekee wakiislam wa Ndanda Sekondari ambao wamefungashiwa virago vyao na kupelekwa vijiji vya mbali kosa lao likiwa ni kutaka haki itendeke baina ya wanafunzi wote,na wakati mwingine walimu waislam hujikuta wakiambulia vichapo na vipigo kama alivyofanyiwa mwalim Halima wa Ifunda sekondari pale alipopinga dhulma, uonevu na udhalilishwaji dhidi ya wanafunzi waislam

shuleni hapo mwaka 2009 akajikuta anaambulia kipigo kutoka kwa mwalim wa kikristo.

NDUGU WANAHABARI

Hapa tumeonesha sehemu ndogo ya madhila yanayowasibu wanafunzi wa kiislam nchini kama mifano tu. kwani ni vigumu kueleza madhila ya kila shule au chuo kwa njia hii. Jambo la faraja ni kuwa kila mtanzania anajua haya hata watu wa kawaida pia Kwa kuwa tatizo hili ni la muda mrefu na baadhi ya viongozi wa serikali mfano Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mh. Benjamin Mkapa alipoulizwa juu ya hali ya uwiano wa waislamu na wasiokuwa waislam katika sekta ya elimu alikiri kuwepo matatizo na uduni kwa upande wa waislam na matatizo mengi huku akisema kuwa si kosa la serikali bali ni tatizo la kihistoria.

Sisi wanafunzi wa kiislam Tanzania tunasema wazi na tunao ushahidi kuwa hili si tatizo la kihistoria bali ni mpango maalum uliosanifiwa na serikali ya awamu ya kwanza kwa lengo la kuwadhulumu na kuwakandamiza waislam kielimu kwa mbinu mbalimali kama hizi zilizotumiwa na uongozi wa shule ya sekondari Ndanda na wanaharakati wengine wa mfumo kiristo katika sekta zote za elimu nchini.Wanafunzi wa kiislamu Tanzania tunajua kuwa kitendo kilichokifanywa na mkuu wa shule ya Ndanda na Bodi ya shule pamoja na maafisa elimu cha kuwafukuza shule wanafunzi ishirini (20) wa kiislam na wengine kuwekewa masharti magumu ya kuacha wito wa dini yao ili waruhusiwe kurudi shuleni si kitendo kipya bali ni muendelezo wa dhulma ambayo walifanyiwa babu na baba zetu ambapo walilazimishwa wachague aidha kuacha dini au kusoma, Alhamdul llah tunashukuru kwa kiasi Fulani walifanya maamuzi magumu ya kulazimika kuacha kusoma na kubaki na dini yao kwani kama wangechagua la pili basi huenda nasi leo tusingekuwa katika dini ya haki ya uislam. Ama leo hii sisi wanafunzi wa kiislamu.
 
Tunasema kusoma ni sehemu ya dini yetu kama tulivyoamrishwa na Allah (sw) Quran (96:1-5) kwa hiyo hatutokubali tena kuacha wito wa dini yetu kwa kutenganisha dini na elimu kwani ikiwa tutafanya hivyo basi itakuwa tumefanya dhulma kubwa kabisa. Hapa tunawapongeza wanafunzi wa kiislam wa Ndanda sekondari kwa kujitambua na kujua haki zao za kiiman na kikatiba kwa kutoutii uongozi wa kidhulma wa shule ya ndanda pale ulipowalazimisha kuacha wito wa dini yao ili wasome, wanafunzi wa Ndanda wamefanya jambo tukufu linalopaswa kuungwa mkono na kuigwa na kila mtu mwema. Na napenda kutoa wito kwa wanafunzi wakiislam nchini kote ya kuwa wanapaswa kuwaiga na kuungana na ndugu zao zao wa Ndanda sekondari kwa kutokubali dhulma ya namna yoyote ile.

NDUGU WANAHABARI

Kadhia ya Ndanda ni mzito sana ambayo imegusa hisia ya kila muislam na kila mtanzania mpenda amani na haki, ukweli wa hili unathibitika wazi wazi kwa kila mwenye uhuru wa kufikiri kwani vijana wale wa kidato cha sita waliofukuzwa ni nguvu kazi muhimu sana kwa ujenzi wa taifa ambao tayari kusoma kwao wangeweza kuiokomboa jamii na taifa kiujumla.Lakini jambo la kusikitisha ni kuona viongozi wenye dhamana katika wizara ya elimu wakilichukulia swala hili kisiasa kinyume na uhalisia wake. Kwa kufanya ziada na uchunguzi wa kubahatisha bila umakini hatimae kutoa taarifa zilizojaa usiasa ndani yake, kuwa eti maamuzi ya bodi ya kuwafukuza wanafunzi (20) wa kiislam ni sahihi huku akieleza kuwa amefika Mtwara na kuongea na Bodi ya shule, mkuu wa shule, walimu na serikali ya wanafunzi hatimae wanafunzi wote Paredi bila ya kuwaruhusu kuuliza maswali au kutoa maoni yao hatimae kutoa hukumu.Hukumu hii haiwezi kuwa sahihi kwani hajawashirikisha wahusika wa upande wa pili wa mgogoro ambao ni wanafunzi wa kiislam kwa kuwasikiliza hoja zao madai yao ya msingi, huku ni kuisaliti katiba ambayo wameapa kuilinda ambayo inarususu uhuru wa kutoa mawazo na kila mmoja kuheshimiwa kwa nafasi yake. Jambo zito zaidi ni kuona naibu waziri anaungana na watu madhalimu waliovunja katiba ya nchi kwa kuwalazimisha wanafunzi kuacha wito wa dini yao ili warudi shule sharti hili linavunja katiba Ibara ya (19:1-2) kinachozungumzia uhuru wa imani na kuabudu.Kutokana na uzito na unyeti wa kadhia hii na madhila haya yanayoendelea kufanywa dhidi ya wanafunzi wa kiislam nchini leo hii tunapenda tuutangazie uma kuwa sasa basi hatutaki kuendelea tena kudhulumiwa na kunyanyaswa, sisi ni watanzania na tuna haki zote kama wanajamii wengine.Kwahiyo tumeitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kufanya mambo yafuatayo;

Tunaitaka wizara ya elimu kuwarejesha wanafunzi wote walofukuzwa na wengine bila masharti yeyote ndani ya siku tano (5) kuanzia tarehe 13/01/2012.

Tunaitaka serikali kuunda Tume huru itakayo chunguza kero wanazopata wanafunzi waislamu katika shule za serikali nchi nzima.

Tunaitaka serikali kuwawajibisha watendaji wa sekta ya elimu wanaoendekeza udini ubaguzi na unyanyasaji kwa wanafunzi wa kiislamu.

Tunaitaka serikali ithibitishe au ikanushe juu ya madai ya mkuu wa shule Ndanda na badhi ya viongozi wa serikali kuwa mashule yaliyotaifishwa na serikali, serikali inamiliki majengo tu ama ardhi na mamlaka ya matumizi yake yako chini ya Taasisi zake za asili.

Shule zote za serikali zitenge maeneo malum ya kufanyia ibada kwa ajili ya watu wa dini zote.

Asilimia kubwa ya wakuu washule za sekondari za serikali ni wakristo, hivyo basi tunaomba serikali iweke mgawanyo sawa wa nafasi hizo.

Kila jambo linapaswa kuwa na mwisho, hatuwezi kuendelelea kuvumilia uonevu wa wazi wazi siku zote.Hatuwezi tena kuendelea kuishi kama wanafunzi daraja la pili katika nchi yetu.Lazima haki sawa na uhuru upatikane kwa wanafunzi wa dini zote na sio kukandamiza waislamu. Hivyo basi tunalazimika kupaza sauti zetu kwaNkuingia barabarani kuonesha hisia zetu katika hali ya unyonge wetu

NDUGU WANAHABARI

Tunakusudia kufanya maandamano ya amani nchi nzima 20 Januari 2012 ambayo yatapeleka ujumbe kwa kila kiongozi wa Elimu katika mkoa yaani Afisa Elimu Mkoa na waislam wa Mkoa wa Dar es salaam watapeleka ujumbe moja kwa moja kwa waziri wa elimu.Kwa lengo la kutaka azingatie madai yetu ya kutonyanyaswa na kubaguliwa katika shule ya serikali.Lakini hatutoishia katika maandamano iwapo hali ya ubaguzi

haitokoma.Tutatumia njia nyingine za kujikomboa katika madhila haya.Tunasema“tumenyanyaswa,tumedhaliliswa, tumebaguliwa kwa miaka 50 ya uhuru na tukavumilia na kusubiri vyakutosha leo tunasema inatosha na tumechoka tunaitaka serikali itambue haki,heshima na utu wetu kama wanavyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine mashuleni na mavyuoni.”Tunataka tuheshimiwe kama wanaadamu, kama wanatanzania huru, wanafunzi halali mashuleni na vyuoni kama wananyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine. Tumeanza muda mrefu kudai haki zetu kwa njia za kidiplomasia lakini hatujasikilizwa na leo tunatumia njia nyingine ya kidiplomasia na kikatiba ambayo ni MAANDAMANO ya amani huenda kwa njia hii serikali na jamii itasikia kilio chetu.

ACHENI KUTUDHALILISHA NA KUTUNYANYASA WANAFUNZI WA KIISLAM MASHULENI

NA MAVYUONI SASA BASI INATOSHA TUNAOMBA WAISLAM WOTE NA WAPENDA AMANI

WOTE MTUUNGE MKONO KATIKA MAANDAMANO HAYA YA AMANI.

Ahsanteni.

JAFARI SAIDI MNEKE
RAISI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI NA VIJANA WA KIISLAMU TANZANIA (TAMSYA)
 


Comments

wabusara
16/01/2012 23:00

Nimeamini nchi ikiendeshwa na watu dhaifu. Dhana za udini zitakuja.. Hapa sioni kitu zaidi ya watu kusukumwa na udini

Reply
sichone
16/01/2012 23:53

hii habari ni ya kinafiki kabisa. mimi nimesoma Tosamaganga, majengo ya shule ni ya wakatoliki na kuna kanisa la wakatoliki tu. kanisa hilo linatumika na wakatoliki tu madhehebu mengine yanasali nje ya maeneo ya shule lakini hawalalamiki. waislam wamepewa eneo shuleni. mimi nadhani huu ni unafiki mkubwa sana. Enyi TAMSYA, waambieni dini yenu mtaifishe misikiti yenu iwe shule za serikali, muajili waislam na muwanyime wanafunzi wakristo sehemu ya kuabudia. Je hakuna shule za serikali ambazo wakuu wake ni waislam na ndani ya shule kuna kanisa?
Acheni lawama.

Reply
sichone
17/01/2012 00:04

mimi nasikitika sana kujua kwamba shule ya ndanda ina waislamu. nilijua ni shule ya kidini ya wakatoliki. unajua kupe akipewa nafasi anataka kula hadi aingie mzima. watu walijitoa muhanga kujenga majengo kwa ajili ya faida yao, lakini kwa kuthamini utu wa mtu kwamba binadamu wote ni saw majengo hayo yakapelekwa serikali ili hata ambaye hakuchangia afaidi. Enyi TAMSYA iambieni serikali ayahame hayo majengo yaliyo kuwa ya kanisa ijinge shule yake yenyewe ili hayo makanisa yasiwaume roho kwani lengo lenu ni hata kutaka historia ifutike. mimi nasema sitaki na wala sitakubali.

Reply
Eli
17/01/2012 02:46

Haya madai na ya kusukumwa na vikundi vya wanaharakati wa kiislamu sidhani kama waislamu wa ukweli hawaelewi kuwa hizo shule zenye makanisa shuleni zilikuwa za wakristo isipokuwa serikali ya awamu ya nyerere kwa kutumia falsafa ya binadamu wote ni sawa, basi shule zote za wakristo zilitaifishwa ili hata mtoto wa kiislamu aweze kupata kusoma. Mimi nimesoma na wanafunzi wa kiislamu hata sikujua kama kulikuwa na waislamu mpaka wakati wa mfungo ukifika ndio unajua kuwa wapo wanapewa special diet kwa ajili ya daku. Hata wakati wa daku walikuwa wanatuamsha sote kula nao, sasa haya mambo ya udini yanaanzaje katika shule za serikali. Nadhani kosa kubwa ambalo serikali imefanya ni kuruhusu mavazi ya kidini kuvaliwa mashuleni.Zamani hakukuwa na kitu kama hicho, na haikuwafanya wanafunzi wa kiislamu wasiwe waislamu. Sasa hizi mwanafunzi wa kiislamu akifanya kosa akafukuzwa kisingizio ni ubaguzi wa kwa waislamu. Jamani shuleni ni sehemu ya kusoma siyo sehemu ya ibada, kama mnataka dini haizuiliwi waislamu kwenda msikitini siku ya ijumaa, ukichagua dini kuliko shule huo ni uamzi wako, siku za masomo ni j3-ijumaa. Dini sio priority katika mfumo wetu wa elimu bali ni chaguo la mtu binafsi. Mbona sijawasikia waislamu wamegoma kufanyakazi kwa vile wanafanyishwa kazi siku ya ijumaa au waislamu wanaacha biashara kwa vile ni ijumaa? Shime shime waislamu msitafute uchochezi usio na sababu, makanisa mnayoyaona mashuleni yalikuwepo tangu shule zilipotaifishwa yasingeweza kuvunjwa, sasa waislamu mkitaka kujenga msikiti eneo la shule huo ni ugomvi, madarasa ya kuswalia yapo, ombeni mtapewa. Km mnataka geuzeni misikiti iwe shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu mvitawale kwa sheria zenu wenyewe km ilivyo kwa chuo kikuu cha waislamu morogoro ambacho mlipewa bure na mkiristo Mkapa bado hamna shukurani. Wakristo wameanzisha seminari kwa sheria zao nanyi fanyeni hivyo, tatizo lenu mkifika shuleni mnaendekeza udini zaidi badala ya kusoma, matokeo yake mkifeli mnasingizia dini. Acheni unafiki tumieni welevu wenu kujisome kujua ukweli wa historia ya elimu kwa waislamu na wakristo Tanzania.

Reply
amran
20/01/2012 13:10

umemaliza,think before

Reply
mimi
17/01/2012 05:12

Kuhusu Lyamungo kuwa na kanisa huo ni uongo mm nimesoma pale hakuna kanisa wala msikiti. Tuache kupandikiza chuki zisizo na msingi

Reply
Amin
17/01/2012 06:01

Huyu anaidhalilisha dini ya kiislamu, anataka uislamu uwe ni muhimili wa taratibu katika sekta ya elimu, yaani watu wa dini zote tumepigika kishenzi badala ya kudai haki za msingi kwa wote, mtu eti unahangaika na malalamiko ya jinisI ya kuabudui mashuleni!

Reply
Evans
17/01/2012 06:48

Mi huwa sielewi kwanini uhangaike na jinsi gani ambavyo mtu anaabudu ilihali haikugusi wewe wala mtu yeyote? Dini huwa ni kitu cha kujitakia na kila mtu ana chake.Kwanini kitugawe wakati utofauti wetu waaminio na wasioamini ni sawa? Inabidi tubadilike

Reply
MKWELI
17/01/2012 09:03

Jaman huu ni msukumo wa kiharakati usiokuwa na ukweli wala kuzingatia kuwa kunawatu walisoma na wanasoma ktk shule mbalimbali za serikali na kutambua shule nyingi Tanzania Bara zilianzishwa na mkoloni kwa njia za Dini ya kikristo,na kweli tenda wema nenda zako Baba wa Taifa akazitaifisha mfano.Pugu ni ya wakatoliki na waisilamu wamejengewa msikiti,waluteri pia ila madhehebu mengine hawana kanisa hawalalamiki,Minaki shule ya angilikana wajengewa msikiti etc,just mention few nataka kuuliza SWALI hizi shule zingekuwa za KIISLAMU je mkristo wangejenga makanisa?wakati mwingine tuache Unafiki Ukweli BARA hosptali nyingi kubwa shule kubwa zimejengwa na Mkoloni(mkristo) na tunatumia wote.NAJUA JUMUIA ZA KIKRISTO ZIMEOMBA SANA SERILIKALI KURUDISHIWA SHULE ZAO LAKINI SERIKALI HAIJAJIBU MPAKA LEO!JE wakristo waandamane kwa hilo mimi nahisi wanaharakati wasitufikishe sehemu tusiyo itaka,YOU GUYS THINK IN DETAILS PLSE.

Reply
AHMED
17/01/2012 20:10

Nasikitika huyu Kiongozi wa sijui kitu gani anavyotudhalilisha sisi Waislamu. Kwanza nadhani hayo ni mawazo yake yeye binafsi na marafiki zake wamepita wakapata fedha za Wafadhili toka Uarabuni sasa wanataka kutuletea fujo hapa nchini. Mimi nimesoma Dakawa Morogoro, pale Wakristu hawana pahala pa kuabudia lakini sisi Waislamu tumepewa sehemu ya kuabudia na kila wakati wa kuswali tulikuwa tunaruhusiwa sisi Waislamu kwenda kuabudu?Nadhani ndugu yangu amekosa cha kumfanya aingie barabarani, ni aibu kuingia barabarani kudai kitu ambacho hauna haki nacho!! utadaije msikiti katika shue ambayo wewe haukujenga?... sina cha kuongea na wajinga kama hao...

Reply
Evans
17/01/2012 23:01

Naanza kupata picha kuwa kuna jambo fulani hapa linataka kufunikwa kijanja kwa kuleta majadiliano mengine.Nachelea kuamini kuwa mhusika alilenga kuleta huu ujumbe ilhali wengi tu wamekuja na kupinga hayo madai.Nahisi ni suala la Madaktari labda ndio linataka lichomekwe ili watu wapate hisia tofauti na hivi kujigawa.Ni mawazo tu najaribu kuwaza nje kidogo ya mada labda

Reply
JAPUONY
17/01/2012 20:17

... naombeni kuwataarifu kuwa zipo pesa chafu katika nchi hii zinamwagwa kutoka nchi za Kiarabu kutuvuruga sisi Watanzania.Fedha hizo zinaletwa katika Misikiti na katika vyama vya siasa kama CUF na pia ndo maana hata sikuhizi Waislamu wanahubiri misikitini kuwa Baba wa Taifa ndiye aliyechangia kuwarejesha nyuma maendeleo ya Waislamu.. Hawana hata aibu ..na waambia kwa hili la Baba wa Taifa wasome historia ya Waislamu katika elimu Vs Wakristu wataona tofauti kubwa sana na jinsi Mwl.Nyerere alivyochangia kuwavuta ndugu zetu Waislamu hata pale ambapo hawakustahili.

Ushauri. Waislamu jengeni shule, somesheni ndugu na watoto wenu. Dini hiyo mnayoing'ang'ania ni ya Waarabu si ya Kwenu! Mababu zenu hawakujua Uislamu hata kidogo sawasawa na Ukristu tumeletewa na WAZUNGU zisitupiganishe na tuwaambie watoto wetu hivyo...

Reply
Ng'wanamvanga
17/01/2012 20:32

Hili ni tatizo la kuwa na viongozi wasio wabunifu katika kuibua na kushughulikia matatizo ya msingi ya wananchi. Hivyo wanajikuta wanahangaika na hoja dhaifu wakati vijana wa Tanzania wana matatizo kibao.

Tumeona viongozi wa namna hii walivyozipeleka vibaya nchi zao, lakini pale wananchi wa nchi hizo wanapogundua kuwa viongozi wao ndio tatizo, basi mchezo umebadirika ghafla (e.g. Arab spring). Kama kijana wa Tanzania ya leo anakaa chini na kuja na hoja kama hii, basi wanaomtegemea kama kiongozi wao wajitazame mara mbili, maana maisha ya sasa yana changamoto nyingi na DINI kwa sasa haina nafasi ya kutatua changamoto hizo.

Reply
Bakari
17/01/2012 20:40

Huku ni kudhalilisha dini, waislam wa Tanzania hawana sababu yoyote ya kulalamika hivi maana hata uwiano wa viongozi kwa sasa ni mkubwa kuliko wenzetu. Lazima tujiulize, hawa waislamu walio kwenye nafasi za uongozi sasa hivi walisomea wapi?

Reply
violet
17/01/2012 23:31

jaman jaman waislam acheni lawama makanisa yapo kwenye shule za kidini ,na shule za serikali amabazo awali zilikuwa za kidini.jengeni zenu,za kwenu waislamu hamjengi halafu mnaleta lawama.

Reply
sichone
18/01/2012 01:46

nashukuru sana wote mliochangia, hawa TAMSYA wanamawazo mafupi sana, badala ya kuhimiza wanafunzi wasome wawo wanahimiza ugomvi. mimi nimekasirika sana na maneno yao. hivi hawajui kwamba shule zenye makanisa, makanisa hayo yalikuwepo kabla hazijawa shule??????. Kama wanaona ni mbaya kwa imani yao, kwa nini wasbomoe misikiti iwe shule za serikali? ama kweli fadhila mfadhili mbuzi, mwanadam mmmmm.

Reply
Kilimba Magidingi
18/01/2012 04:10

Kaka na dada zangu, chonde, chonde! Waacheni waendelee kulalamika si tukipaa1 Kwani shida iko wapi? Mtu mvivu huwa na muda wa kulamu na kutokuwa na shukrani hata pale anapokuwa maevaa vazi alilohisaniwa na mhisani! Malalamiko mema acheni wakrito tuendelee na Yesu! Mat.5:13" Ninyi(Sisi Wakristo) Ni NURU ya Ulimwengu)

Reply
Kilimba Magidingi
18/01/2012 04:10

Kaka na dada zangu, chonde, chonde! Waacheni waendelee kulalamika si tukipaa1 Kwani shida iko wapi? Mtu mvivu huwa na muda wa kulamu na kutokuwa na shukrani hata pale anapokuwa maevaa vazi alilohisaniwa na mhisani! Malalamiko mema acheni wakrito tuendelee na Yesu! Mat.5:13" Ninyi(Sisi Wakristo) Ni NURU ya Ulimwengu)

Reply
kb
18/01/2012 21:53

jamani huo ushahidi ulielezwa na TAMSYA hamuooni msisome kwa ushabiki someni muelewe hiyo taarifa vizuri sio kukurupuka tu.

Reply



Leave a Reply