Tukio hilo limetokea majira ya saa 5:00 usiku wa Ijumaa ya Januari 20 mwaka huu katika Kituo hicho cha Mabasi yakitokea mikoa mingine.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kondakta wa basi hilo aliyejulikana kwa jina la Januari Kapinga aliingia ndani ya basi hilo lenye namba za usajili T 853 AVQ aina ya Yutong lililokuwa likitokea Dar es Salaam baada ya abiria wote kushuka ndipo alipolikurupua kwa nguvu na kumshinda hatimaye kuparamia ukuta.
Abiria aliyefariki alikuwa safarini kuelekea masomoni mkoani Tabora na wakati gari likiparamia ukuta wa mgahawa huo alikuwa akipata chakula cha jioni. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, mtu mmoja alifariki na watu watano kujeruhiwa.
Aidha kondakta wa basi hilo alitoroka na kwenda kusikojulikana na juhudi za Jeshi la Polisi kumtafuta zinaendelea. Dereva wa basi hilo anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi.
Noah Mwakatumbula, Mwenyekiti wa Kituo cha Mabasi mkoani Mbeya yaendayo mikoani amewataka madereva waliopewa dhamana ya kuendesha vyombo hivyo na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waache mara moja tabia ya kuacha funguo za vyombo vyao vya usafi.
--
taarifa via blogu ya Mbeya Yetu






RSS Feed