Kwa masikitiko Makubwa, Ofisi ya Bunge inawatangazia Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wote kuwa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 19 Januari, 2012 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia na Chama chake imeandaa shughuli ya kuaga rasmi mwili wa Marehemu siku ya Jumamosi, tarehe 21 Januari, 2012 katika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 5 asubuhi na baada ya hapo atasafirishwa siku ya Jumapili asubihi kuelekea Kijijini kwao Akeri, Meru, Mkoani Arusha kwa mazishi yatakayofanyika siku ya Jumatatu tarehe 23 Januari, 2012. Kutokana na msiba huo, shughuli za Kamati kwa siku za Jumamosi tarehe 21 Januari, 2012 na Jumatatu tarehe 23 Januari, 2012 zimesitishwa na zitaendelea tena siku ya Jumanne tarehe 24 Januari,2012 baada ya maziko. Marehemu alikuwa anaumwa Saratani ya Ubongo ambayo ilimsumbua kwa muda mrefu na mnamo mwaka 2010 alipelekwa nchini India kwa upasuaji na alirejea nchini na hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri. Hata hivyo mwishoni mwaka 2011 hali yake ilibadilika ghafla na kuanza kuwa mbaya alirejea nchini tarehe 9 Januari, 2012 na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alifariki dunia tarehe 19 Januari, 2012. Marehemu ameacha mjane na watoto wanne (4). MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMEN Imetolewa na: Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge S. L. P. 9133 DAR ES SALAAM 9 Januari, 2012 SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb.,) kutokana na kifo cha Mhe. Jeremia Solomon Sumari, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CCM na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 19 Januari, 2012 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu. “Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mheshimiwa Jeremia Solomon Sumari kwani alikuwa kiongozi aliyewatumikia vema wananchi wa Jimbo lake la Uchaguzi la Arumeru Mashariki na Taifa kwa ujumla katika wadhfa wake wa Waziri kwa umahiri na uhodari mkubwa”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake. Rais Kikwete amesema kutokana na kifo chake, wananchi wa Arumeru Mashariki wamepoteza kiongozi wa kutegemewa sana huku Taifa likiachwa na pengo kubwa ambalo si rahisi kuzibika ikizingatiwa kwamba alikuwa kiongozi katika Wizara ambayo ni mhimili muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu. “Kwa dhati ya moyo wangu, natuma salamu za rambirambi na pole nyingi kwa familia ya Marehemu Jeremia Sumari kwa kumpoteza kiongozi na mhimili madhubuti wa familia. Ninawahakikishia kwamba nipo pamoja nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa, na namuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema aipumzishe roho ya Marehemu Jeremia Solomon Sumari mahali pema peponi, Amina”, ameongeza kusema Rais Kikwete. Ameiomba familia ya Marehemu kuwa na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni mapenzi yake Mola. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM. 19 Januari, 2012 Mbunge wa jimbo la Arumeru Chama cha mapinduzi (CCM) Jeremiah Sumari amefariki dunia leo katika kitengo cha mifupa kwenye hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dar es Salaam. Apumzike pema marehemu Jeremiah Sumari. Awafariji nyote mlioguswa na msiba huu. CommentsSalehe Mchome 19/01/2012 8:44pm
Poleni sana wana Arumeru kwa msiba uliotupata,Mungu amweke mahali pema peponi Amina.
Reply
Kusanya Shindika 19/01/2012 10:04pm
"Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa" ! We have lost a Man we needed him more at this time of economic crisis he was dedicated man from Tareto Bureau de Change when I knew him to Member of Parliament, I know he went through terrible time of his problem! Mungu Amuweke mahali pema na Ndugu mtegeeni Bwana!
Reply
ELINAMI NOE LEMBUKI NNKO 20/01/2012 3:18am
My beloved Mb,Jeremiah Sumarry,we shall remember you forever,May God keep you in peacefull resting place.
Reply
Comments are closed. | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed