Akaniuliza mbona sikuandika kwenye "microsoft word" kwanza kisha nikate na kubandika ujumbe kwenye barua pepe?
Nikamfahamisha niliacha kufanya hivyo kwa muda sasa baada ya kurahisishiwa mambo na "gmail offline".
Gmail Offline ni huduma ya Google ambayo inawafaa sana watumiaji wa Gmail kwa ajili ya mawasiliano ya barua pepe.
Inawezekanaje?
Huduma hii inafanana na huduma ya Outlook ya Microsoft Windows, watumiaji wake watakuwa wanaifahamu.
Katika mazingira yetu ambapo mawasiliano ya intaneti bado ina vikwazo vya aina mbalimbali kwa baadhi ya watu, ni dhahiri kuwa kutumia Google Offline ni faida kubwa kwani unaweza kusoma ujumbe kupitia email na kuandaa majibu kwa kila ujumbe wa muhimu na kisha kuchomeka modem au kwenda kwenye mgahawa wenye intaneti ambapo unaweza kuunganisha kupitia waya wao au bila waya "wireless" na kutuma majibu ya emails zako ndani ya dakika chache.
Kwa yeyote mwenye laptop (au desktop nyumbani) lakini haiunganishwi na intaneti muda wote ili kupunguza gharama za intaneti, jiwekee Gmail Offline App kwa ajili ya kufaidi huduma ya Google Offline.
App hii inafanya kazi kwenye kirambaza wavuti cha google, yaani Google Chrome, hivyo kama computer yako haina, jipakulie kisha chomeka app hiyo na uanze kuitumia.
- Kujipakulia Google Chrome, bofya hapa
- Kujipakulia Gmail Offline app, bofya hapa.
- Kwa maelezo zaidi juu ya Gmail Offline app, bofya hapa


RSS Feed