Ujumbe huu umenifikia kupitia anwani pepe, na kwa kuwa unaihusu jamii, ni vyema kuuchapa hapa ifuatavyo: 

Kumezuka wimbi jipya la uhalifu.

Unakuta mfuko wa nylon (maarufu kama mifuko ya condom, rambo, plastic) barabarani . Ukiukanyaga tu lazima utapata puncher maana ndani yake kuna kibao kilichopigiliwa misumari zaidi ya unavyofikiria wewe. 

Ukishuka garini kuangalia kulikoni wimbi la vibaka linakuvamia na hakuna utakachobakia nacho zaidi ya gari maana litakuwa halina upepo baadhi ya Magurudumu.Vibao ni vingi kwa umbali mfupi mfupi. Hii imetokea jana Tabata Kisukuru maeneo ya makoka mida ya saa tatu usiku. Waliopata pancha ni pamoja na mke wangu na magari mengine kibao, waliolifanikiwa kuibiwa sijapata taarifa bado ila tuliji-organise na kupita njia zote na kuvikusanya.

Watakupiga kiasi gani hiyo inategemea kiwango cha bangi walichovuta na unajeuri kiasi gani.
 


Comments

Baba T
21/01/2012 03:06

asante kwa taarifa, ila sasa Hali ishakuwa mbaya na uwezo wa kufikiri wa hawa wezi wetu nao umefikia mwisho, watatuuwa, ukimbahatisha bora umuwahi wewe

Reply



Leave a Reply