mtoto huyo ambaye kwa sasa ameathirika kisaikolojia kutokana na tukio hilo,inadaiwa na wasamalia wema kuwa,mwanamke huyo amekuwa akimpa vipigo mara kwa mara kwa kutumia waya.
Taarifa ya jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro iliyotolewa kwa vyombo bya habari imedhibitisha ukatili dhidi ya mtoto huyo na kwamba mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Anna John(28)mkazi wa mtaa wa Kiusa katika Manispaa ya Moshi, bado anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni matokeo ya wanawake wanaojihusisha na uuzaji wa mboga mboga na matunda wa mtaa wa Kiusa mjini Moshi kuamua kufuatilia nyerndo za mtoto huyo baada ya kutumwa sokoni na mtuhumiwa na kisha kurejea tena sokoni akiwa analia na kuwapa hofu kina mama waliokuwa sokoni na kuhoji kulikoni.
Kamanda wapolsisi mka wa Kilimanjaro Absalom Mwakyoma katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi amedai kwua,baada ya kina mama hao kuhoji kulikoni mtoto huyo alidai shangazi yake asiyek uwa na chembe ya utu hata kidogo alimpiga kwa madai kuwa vitu alivymtuma sokoni si vile alivyonunua.
Kwamba mtoto huyo alipewa sh,2,000 ili akanunue ndizi mbichi,nyanya na nyama robo lakini mtoto huyo alinunua ndizi mbivu pamoja na nyanya na kupeleka nyumbani akiamini kwamba ametimiza kile alichotumwa.
Wasamalia wema ambao ni kina mama wauzaji wa mbogamboga pale Kiusa moshi wlailazimiak kumwongeza mtoto yule pesa ili anunue nyama robo pamoja na ndizi mbichi na kumpa ili apelike nyumbani kuepuka vipigo tena.
Mtoto huyo alirejea sokoni kwa mara ya pili akilia tena hali ambayo lishtua kina mama hao na kuamua kuhoji kulikoni?,hapo wakaanza kumchunguza mwilini na kubaini unyama uliofanywa na shangazi yake na hapo wakaamua kwenda polisi wakiwa na mtoto huyo na hapo polisi wakaingia kazini na kumtia mbaroni mtuhumiwa.
baada ya kuchunguzwa zaidi mtoto huyo amebainikak uwa ma makovy ya zamani na makovu mapya tumboni,ubavuni pamoja na mgogoni na baadhi ya makovu mapya hadi jana yalikuwa yakitoa damu kuonyesha ni jinsi gani alivyoteswa.
Mtalamu mmoja wa masuala ya kitabibu katika Hospital ya mawenzi (jina limehifadhiwa) amesema mtoto huyo kisaikolojia ameumia, atakuwa mwoga na hata shule hawezi kufanya vizuri kwa maana nyingine ni kwamba anakabiliwa na msongo wa mawazo ambao unaumiza kuliko hata ungonjwa wenyewe.
Katika Hospital ya Mawenzi alikolazwa mtoto huyo,umati mkubwa wa watu uijaza hapo ukiongozwa na mbuge wa Viti maalumu (CHADEMA), Lucy Owenya na waliokuwapo hapo wamelaani unyama huo na kutaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya mtuhumiwa.
Hata hivyo wengi wamehoji kama unyama huo unatendwa na mtu aliyeenda shule mwenye taaluma ya mwalimu ambaye siku zote jamii inaamini mwalimu ni mlezi wa watoto,huko kwingine hali ikoje?
Kama mwalimu anamtenda hivi mtoto ambaye ni damu yake kwa maana ya mtoto wa kaka yake,itakuwaje kwa watoto wa wengine hasa anaowafundisha darasani ?


RSS Feed